Bunge Halina Ubavu wa Kuilazimisha Serikali - Chikawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge Halina Ubavu wa Kuilazimisha Serikali - Chikawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngisibara, Dec 18, 2009.

 1. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Date::12/17/2009Waziri wa Sheria adai Bunge la sasa halina ubavu kwa serikaliNa Leon Bahati

  WAZIRI wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe amezidi kutoa kauli tata baada ya kuligeukia Bunge la Jamhuri ya Muungano, akisema halina nguvu ya kuilazimisha serikali kufanya mambo na kwamba kazi yake ni kuishauri.

  Hiyo ni kauli ya pili ya waziri huyo katika kipindi kisichopungua wiki moja baada ya kukaririwa Jumatatu akisema kuwa Rais Jakaya Kikwete hana uwezo wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi kwa kuwa mfumo wa utawala wa sheria hauruhusu vitendo kama hivyo.

  Kauli hizo mbili zinazohusu mamlaka ya kisheria zimetolewa katika kipindi ambacho mjadala mkubwa wa hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa katika kashfa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) ukiwa umemgeukia rais.

  Pia Chikawe ametoa kauli hiyo wakati Bunge likiishinikiza serikali kutoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio yake 23 dhidi ya wahusika kwenye kashfa hiyo kubwa iliyotikisa nchi baada ya Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu kutokana na ushauri uliotolewa na kamati teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo.

  Serikali ilipiga chenga kuwasilisha taarifa hiyo kwenye Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri, hali ambayo inawafanya watunga sheria kusubiri kwa hamu maelezo kuhusu kashfa hiyo wakati wa mkutano ujao.

  Lakini wakati hayo yakitokea, Chikawe ameibuka na maelezo mengine ambayo hakuna shaka kwamba yataibua mjadala mwingine mkali na hasa mamlaka ya mihimili mitatu ya nchi katika kipindi ambacho Bunge linaonekana kuanza kupata nguvu ya kuhoji na kuchunguza mambo ya serikali ambayo awali yalionekana kuwa nyeti.

  Chikawe alisema kuwa hakuna namna ambayo Bunge hilo linaweza kuweka mguu chini na kusema lazima serikali itekeleze jambo fulani kutokana na nguvu ya chombo hicho kumezwa kisiasa.

  "Katika mazingira haya ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, Bunge halina madaraka ya kulazimisha serikali itekeleze jambo," alisema Chikawe kwenye mahojiano na gazeti hili juzi.

  "Hata pale yatakapotokea mazingira magumu kwa serikali, nguvu ya siasa itachukua mkondo wake na kuokoa jahazi."

  Waziri huyo mwenye taaluma ya sheria alisema katika mfumo wa vyama vingi, wabunge wanawajibika kwa vyama vilivyowaptisha na kwa wananchi tofauti na mfumo wa chama kimoja ambao huwajibika moja kwa moja kwa wananchi.

  "Hata serikali iliyo madarakani inawekwa na chama na inatekeleza sera za chama hicho kilichopewa ridhaa na wananchi," alisema Chikawe.

  Alikiri kwamba wabunge wanaweza wakapandwa na munkari kama ilivyotokea katika suala la kashfa ya Richmond na kuibana serikali, lakini akasema mwisho wa siku watajikuta katika mazingira ya kuwajibika na kuwa kwenye msimamo wa kichama.

  Chikawe hakuweka bayana kwamba CCM inaweza kumaliza vipi suala la Richmond, lakini CCM imekuwa ikitumia nguvu yake ya idadi kubwa ya wabunge kutuliza masuala ambayo yanaonekana kuwa magumu kwa serikali. Pia CCM iliwahi kutumia nguvu yake ya kisera kuzima mjadala wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ulioibuliwa na wabunge 55 mwanzoni mwa miaka ya tisini.

  Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaita wabunge wote wa CCM katika mkutano wa pembeni na kuwaeleza kuwa sera ya chama hicho si kurejea kwenye serikali tatu, bali kuundwa kwa serikali moja na hivyo kuwataka kufuata sera za chama hicho wanapokuwa kwenye chombo hicho cha kutunga sheria kwa kuwa CCM ndiyo iliyowapa fursa ya kuchaguliwa kuingia bungeni.

  Katika Bunge la sasa lenye watu 318, CCM ina wabunge wapatao 278 na hivyo kuwa na nguvu kubwa katika kufanya maamuzi yanayoibeba serikali.

  Tangu kufikiwa kwa maazimio 23 ya Bunge dhidi ya kashfa ya Richmond mapema mwaka jana, serikali imekuwa ikisita kutoa taarifa ya utekelezaji wake zaidi ya kueleza kuwa Lowassa na mawaziri wengine wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha walijiuzulu na kwamba watendaji wengine waliandikiwa barua za kujieleza na walishafanya hivyo.

  Hata hivyo, bado serikali haijaeleza kama imeshawawajibisha watendaji hao, akiwemo mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hoseah ambaye mamlaka yake ya kumwajibisha ni rais, huku watendaji wengine wakistaafu kwa mujibu wa sheria.

  Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema serikali inatarajia kutoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio hayo katika mkutano ujao wa Bunge, lakini akasema binafsi anaona kitendo cha Lowasa kujiuzulu pamoja na mawaziri wawili kilichosababisha serikali kuvunjwa, ni hatua tosha kwa tatizo hilo.

  Tatizo kubwa katika kashfa hiyo, alisema Chikawe, ni uzembe uliofanywa na watendaji wa serikali wa kutofanya uchunguzi wa kutosha ili kujua uhalali na uwezo wa kampuni ya Richmond.

  Lakini akasema anaona suala hilo linakuzwa sana kutokana na kutumika kama silaha ya kukomoana kisiasa kwa kigezo cha mapambano dhidi ya ufisadi.

  "Siasa nyingi zimeingia; watu wanatumia (Richmond) kumalizana kisiasa na ndio maana yamekuwepo malumbano yasiyoisha... sasa neno ufisadi linatumika kumalizana kisiasa," alisema Chikawe.

  Kuhusu uwezo wa Bunge kuwa na mamlaka ya kuweza kumuondoa rais madarakani pale inapotokea kutokuwa na imani naye kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 46(A) ambayo inaelezewa pia na ibara ya 121 ya kanuni za kudumu za Bunge, Chikawe alisema:

  "Katika mfumo wa vyama vingi nenda kokote duniani hata Uingereza, chama kilichounda serikali hakiwezi kikaachia na hadi kuona serikali yake inaondolewa na wabunge wake. Wataitana watawekana sawa (ili kuokoa jahazi)."

  Alisema katika mazingira hayo ya vyama vingi, chama tawala kinaweza kuwachukulia hatua hata za kumfukuza uanachama mbunge au wabunge wanaoendesha shinikizo la kuiondoa serikali madarakani.

  Alieleza kwamba hayo ni mazingira ambayo hayawezi kuepukika kwenye mazingira ya uendeshaji wa Bunge la vyama vingi, hasa ikizingatiwa kwamba mara nyingi wabunge hujikuta wakilazimika kukutana kivyama ili kuwa na msimamo katika jambo zito.

  Alielezea mazingira hayo kuwa ndiyo yanakipa nguvu chama kilichounda serikali kuwa na nguvu bungeni na hasa pale kinapokuwa na wabunge wengi. Hata hivyo, Chikawe alisema chama kilicho madarakani kina wajibu wa kuhakikisha kwamba mambo yanaenda vizuri kwa manufaa ya wananchi wote, hivyo kila jambo la ukosoaji linapimwa na kuchukuliwa hatua kulingana na uzito wake lakini siyo kwa kushinikizwa.

  Jamani naomba anayemjua kwa undani huyu waziri atupe background yake kwanza
   
 2. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Date::12/17/2009
  Waziri wa Sheria adai Bunge la sasa halina ubavu kwa serikali

  Na Leon Bahati

  Alielezea mazingira hayo kuwa ndiyo yanakipa nguvu chama kilichounda serikali kuwa na nguvu bungeni na hasa pale kinapokuwa na wabunge wengi.
  Hata hivyo, Chikawe alisema chama kilicho madarakani kina wajibu wa kuhakikisha kwamba mambo yanaenda vizuri kwa manufaa ya wananchi wote, hivyo kila jambo la ukosoaji linapimwa na kuchukuliwa hatua kulingana na uzito wake lakini siyo kwa kushinikizwa.

  Ndugu wana JF, Bila shaka huu ndiyo ukweli wa mambo. Mh Chikawe amakuwa mkweli juu ya namna serikali wanavyo liona bunge letu na ndiyo maana mambo huenda kama serikali ipendevyo. Yote haya yatabadirika iwapo bunge la halitakuwa na chama cha siasa kimoja chenye majarity kuamua mambo kinavyotaka.

  Kwa mtizamo wangu, nadhani bunge safi ni pale ambapo anagala chama kimoja hakizidi asilimia 30 ya wabunge, ili ili kiunde serikali basi lazima kishirikiane angalau na vyama vingine.

  Kazi ya kuiendeleza bongo bado ni ngumu na nisafari ndefu kuifikia.
   
  Attached Files:

 3. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wananchi ndiyo wanaweza kuamua idadi ya wabunge bungeni na si vinginevyo.
   
 4. G

  Genda Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chikawe, this time you are right!

  Wakati uliopita ulitapikia Katiba!
   
 5. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tuwasubiri kwenye uchaguzi mwakani!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kama mtu anatumia kichwa chake vizuri, kuna wakati wa kuvuta pumzi na kusema wait a minute..let me think! Chikawe ameanza kujaribu kuutafuna mfupa ambao umewashinda mbwa magwiji.Hakika asipoangalia ataishia kutoa meno na kuwa kibogoyo!
  By the way kuna mtu alitoa suggestion hakuna sababu ya kuwa na waziri wa sheria maana AG anatosha!Kwa mwendo huu naungana naye hakuna sababu ya kujaza watu wasioelewa kazi wanazozifanya wawe viongozi wa wizara
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  This is no brainer.... hatuhitaji maelezo marefu... kazi ya bunge ni kutunga sheria na kuishauri serikali. Ingawa pia inaweza kuisimamia serikali kwa maana wakiona hawaridhiki... wanatumia rungu lao la kutokuwa na imani na waziri mkuu.
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  PERIOD!!!!!

  But is it Possible? kwa hawa wabunge wetu tulionao?
   
 9. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  I think we are missing the point here. Tuangalie Chakawe alianzia wapi. Alisema hawezi bana mafisadi. Si kazi yake. Ni kazi ya jurisdiction. Watu wenye akili zao wakampinga sababu waliona katumwa kutetea. Sasa hivi kaja na Bunge haliwezi ibana Serikali. WHAT IS HE UP TO? ANATETEA NINI? Simple. Mafisadi. Mumewahi msikia Chakawe akipinga ufisadi? Yeye, Makamba, Sofia Simba, Chiligati etc hawajawahi pinga ufisadi hata siku moja. Wanachofanya nikupinga wale wanaetaka mafisadi wachukuliwe hatua.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Chikawe hawezi kupinga ufisadi kwani yeye mwenyewe ni fisadi; alikatiwa pochi ya EPA akaanzisha Petrol Station ya BP iliyopo kwenye junction ya Mwenge kuelekea Lugalo na Ubungo!! Anaindesha rafikiye ambaye ndio boya lake!! Kwa wale wanaokumbuka, chikawe alifukuzwa Ikulu alikokuwa anafanyakazi kwa tuhuma za utovu wa maadili leo hii bila kucheck background yake anapewa uwaziri tena wa wizara nyeti ya sheria kwa qualification ya uanamtandao!! What a disgrace.
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa katiba hii tuliyo nayo CCM wataendelea kujidai sana...
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hata sisi chadema tungeingia madarakani tungehakikisha tunatengeneza katiba itakayofanya TUJIDAI!
   
 13. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wewe umeleta kijimwanga ndani ya kiza kinene, kweli haiwezekni msomi mwenye akili timamu abwabwaje na kujaribu leta mgongano wa kikatiba akijua wazi kuwa anaongea na watu wenye akili,
  Iaelekea huyu bwana kapewa uwaziri kwa kazi hii anayoifanya sasa na si vinginevyo
   
 14. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Naomba wana JF tusiingie mtegoni. Tuache ubora au udhaifu wa Chikawe na binadamu. Tujadili hoja aliyoitoa. Naamini kuwa na matatizo huko nyuma hakumuondolei uwezo wa kutoa hoja yenye maana au mbaya.

  Je, alichosema Chikawe kinaukweli??? Yaweza kuwa si kweli kisheria, lakini naamini kisiasa za CCM na taasisi zake hoja yake inaweza ikawa na ukweli. Pia yawezekana haya ndiyo yanoaminika serikalini kuwa bunge lao la CCM halina ubavu wa kuibana serikali yao. Bila shaka ushahidi wa mazingira unonesha hivyo.

  Inawezekana vipi bunge linapigwa danadana na serikali na hakuna linalofanyika.

  Mimi naamini chikawe ametupasulia kidogo tu lkn point nzito sana.
   
 15. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  naamini chikawe kasema ukweli mchungu.
  kwani amesema bunge halina ubavu na ameelezea kwa nini
  amesema hivyo.

  hata hivyo kauli yake ingekuwa na utata kama angesema "bunge halina mamlaka" ya kilazimisha serikali.... naamini hapo ungehitajika
  msaada wa waliobobea katika masuala ya katiba na masuala
  ya sheria zinazoelezea mamlaka ya bunge.
   
 16. b

  bigilankana Senior Member

  #16
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Huyu Chikawe hakuna lolote katika hili. Sema la CCM halina nguvu
   
 17. b

  bigilankana Senior Member

  #17
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  he, ndio mpango wenu huo kuingia madarakani kuweka katiba inayowafaa nyiye na sio wananchi? duh, sema haupo serious tafadhali unatania
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mnyika, Zitto, Dr. Slaa, Mbowe, Lipumba, Ruhuza na wengine mlioko Upinzani hata wale mlioko ndani ya CCM, ni nini maoni yenu kuhusiana na senteso hii?

 19. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Wananchi wanapaswa kutambua kuwa wanao uwezo wa kuwaondoa viongozi wasiofaa kwa kuwapigia kura wengine.

  Vivyo hivyo wanaweza kukiondoa Chama kisichofaa tena na kukipa kura Chama kingine. HII INAWEZEKANA TU KWA KUPIGA KURA.

  Kamwe wasije KUSUSIA UCHAGUZI wakidhani ni dawa. Hii ni hatari sana.

  Mfano wakazi wa Kipawa walilalamikia malipo ya fidia na wakasema wataususia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Viongozi waliwapuuza na kuwakejeli tu. Matokeao yake wakatetewa Polisi na kutawanywa kutoka barabara ya Mwl. Nyerere walipokuwa wamekusanyika.
  Ila kama wangesema kuwa madai yao yasipotekelezwa basi watahamasishana wote KUKIPIGIA KURA CHAMA FULANI CHA UPINZANI, Serikali ingewasikiliza.

  Ukidhani ukisusia unaikomoa Serikali na Chama kilichopo madarakani, unajidanganya. Watacheka tu, na watabaki madarakani, kwani ina maana ukipiga kura unawachagua wao (watawala), na ukiwa na hasira na machungu nao wala wauwachagui wapinzani/washindani wao, ila UNASUSIA UCHAGUZI, badala ya kuchagua Viongozi mbadala, ili kukiondoa Viongozi wasiofaa, na Chama kisichofaa.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijui nianze kupiga watu makonzi?

  hivi mmesema preamble ya Katiba yetu? NI wazi waziri wa Katiba hajasoma preamble wala Katiba yenyewe..
   
Loading...