Bundi aingia ndani ya ukumbi wa Bunge leo asubuhi

Amepita pitaje?? Kwenye nyufa au kwenye kuta??..
Ila kama mdau hapo alivyoelezea, bundi kisayansi wako very sensitive to the smell of dead cells..
Wanasayansi wa wanyama na ndege kupitia vipindi kama Nat Geo Wild wanafanya tafiti deep sana za hawa viumbe wanaotuzunguka na kwa kweli kuna vitu vingi sana muhimu vya kujifunza kupitia wanyama, ndege na hata wadudu.. Natamani tungeweza kuipata hiyo sayansi na vifaa kupata maarifa yaliyo wazi lakini yote kheri..

Sent using Jamii Forums mobile app

Amanizzle,
Hapa ndipo unapoweza kugundua Ukuu wa Mungu kwa namna alivyowaumbe viumbe tafauti tofauti ili waweze kuyatawala mazingira wanayoishi. Kwa asili ndege na wanyama wengi bado wana asili ya uumbaji ambayo huwapa taarifa ya tukio fulani liwe baya au zuri. Tofauti na binadamu ambaye AMEJICHAFUA kwene DHAMBI kiasi kwamba Mungu hawezi kuwapa taarifa wanadamu kupitia kwa MANABII, NDOTO au SAUTI. Ndiyo maana ndege kama TAI anaweza kujua mzoga ulioko Zambia akiwa Tanzania na akaruka mpaka kwenda kula!!. Kuna kitu kinaitwa INSTINCT kiko kwa wanyama/ndege ambacho huwa kinawapa ISHARA/DALILI(stimulus) wh ya kugundua kuwa kuna jambo fulani litatukia sehemu fulani whether ni baya au zuri...!!!.
 
Bunge mpaka limekuwa na bundi
Hapo ni zile samaki za kupima kwa rula na kusababisha Panya wajae hapo.
Hakuna uchawi wala nini bali ni uchafu tu

Sent from my SM using Tapatalk
 
Yeah ndio ilivyo ...wataalamu wanasema kwamba anauwezo mkubwa " wakugundua wakunusa kiasi kwamba never zake huwa zinampatia taarifa Kwamba kiumbe fulani kimepunguza chembe chembe hai mwilini na Muda sio mrefu kitakufa ...so bundi huwa anaenda mpaka karibu na makazi ya hicho kiumbe akitumaini kwamba kikifa anaweza kujipatia mzoga .... kuna thread ambayo imewahi kueleza kwakina kuhusu hilo humu .....

Ila sio kweli kwamba kila wakati ambao bundi huwa anaonekana basi patakuwepo na kiumbe ambacho kitafikwa na umauti

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua kwa kushirikiana na baadhi ya viumbe tunaweza kutatua matatizo mengi sana kwenye jamii. Mnyama pekee anaye tumiwa vilivyo zaidi ya mashine ni mbwa, anaye weza kunusa dawa za kulevya kwa ufasaha lakini wapo weingine chungu mzima wanaoweza hata kugundua chanzo cha kansa.

Nafahamu Sua wametumia panya kunusa mabomu ya kutegwa ambapo wameweza kuokoa maisha huko Angola kwa kutegua mabomu na pia kuna wale wanao nusa chembe chembe za kifua kikuu kwa haraka na ufasaha zaidi kuliko kusoma X-ray
 
We ndio sasa unataka kuwatisha watu zaidi ya kuwafariji. Unataka kumaanisha kuwa tayari ameletwa hapo mjengoni na harufu ya kifo? Ni nani humo bungeni aliyekwisha kuwa na dead cells? Ili ikiwezekana awahishwe India??!!
Hakuna cha dead cells ni ujinga mtupu na aliyewafundisha wanajf huu ujinga kawaokota kindezi mno
 
Unajua kwa kushirikiana na baadhi ya viumbe tunaweza kutatua matatizo mengi sana kwenye jamii. Mnyama pekee anaye tumiwa vilivyo zaidi ya mashine ni mbwa anaye weza kunusa dawa za kulevya kwa ufasaha lakini wapo chungu mzima wanaoweza hata kugundua chanzo cha kansa. Nafahamu Sua wametumia panya kunusa mabomu na chembe chembe za kifua kikuu.
Naam nikweli " Hiyo Ya sua kutumia panya hawakuanza leo mkuu ..mimi nimeishi karibu na kile chuo mnamo miaka ya 95s. ..hizo project walizianza kitambo kidogo.... wanyama .wadudu., huwa wana jua vitu vingi sana ambavyo kama wasomi wetu wa africa wangejikita zaidi katika tafiti kuhusu wao basi nasisi tubgekuwa miongoni mwa watu wenye technology kubwa sana ", tungeiuza na sisi kunufaika na hilo "... Imagine pasingelikuwa na uwepo wa treni bila wazungu kuiga umbo LA mdudu tandu".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulimuona mchana ila sikumbuki kama alikuwepo usiku pia ni miaka mingi sana imepita.

Kwani alifika Kitandani kwa Mgonjwa au? Kwa sababu kama Bundi ana uwezo Wa kumnyofoa mgonjwa Roho yake ni kwa nini ahiyari kutoka huko mbali aje karibu na nyumbani halafu aogope kutua kwenye kitanda cha mgonjwa?

Kama Bundi anaogopa kuuawa basi hana uwezo anaodaiwa kuwa nao. Bundi, angalikuwa na uwezo wowote Wa kipekee,Wa kutoa Roho ya mtu angalijiamini kwa kuja moja kwa moja na kutua hata kwenye Tumbo la mgonjwa na yeyote ambaye angejaribu kumdhuru naye angenyofolewa Roho yake vile vile au huyo Bundi angetoweka tu ghafla na asionekane amepitia wapi kama ambavyo anadaiwa kunyofoa au kumchukua mgonjwa bila watu kumuona mgonjwa amechukuliwaje.
 
Kwa hiyo,Bundi ni Mnyama Wa Shetani? Na kama ndivyo,huyo shetani amejichagulia tu Bundi Wa Afrika na wa sehemu zingine Duniani anawaogopa?

''Soma hiyo'' kama una fikiri imani hizo ziko Bongo na Africa tu...!!
1548752980145.png

Owl Symbolism
Symbolic meanings for the owl are:
  • Intuition, ability to see what others do not see
  • The presence of the owl announces change
  • Capacity to see beyond deceit and masks
  • Wisdom
  • The traditional meaning of the owl spirit animal is the announcer of death, most likely symbolic like a life transition, change
Native Americans associated the meaning of owl with wisdom, foresight, and keeper of sacred knowledge. ... To this day the owl is considered a witch's familiar (an animal soul-spirit linked to a spiritual person via a unique, communicative bond). The owl is a creature of the night.

Kazi kwenu na Matonya wako!
 
Kwa kawaida ndege aitwaye bundi hufanya shughuli zake wakati wa usiku na anapoonekana mchana huleta tafsiri zenye hofu.
Kwa mujibu wa Spika leo bundi ameonekana bungeni majira ya mchana hali iliyosababisha Spika achanganye mambo. Lakini Ndugai amesema yeye anamhofia bundi wa usiku siyo yule wa mchana.

Sasa najiuliza kama bundi wa mchana hana madhara ilikuwaje Spika Ndugai akachanganya mambo?!

Mshana jr karibu tafadhali
Maendeleo hayana vyama!
 
Kwani alifika Kitandani kwa Mgonjwa au? Kwa sababu kama Bundi ana uwezo Wa kumnyofoa mgonjwa Roho yake ni kwa nini ahiyari kutoka huko mbali aje karibu na nyumbani halafu aogope kutua kwenye kitanda cha mgonjwa?

Kama Bundi anaogopa kuuawa basi hana uwezo anaodaiwa kuwa nao. Bundi, angalikuwa na uwezo wowote Wa kipekee,Wa kutoa Roho ya mtu angalijiamini kwa kuja moja kwa moja na kutua hata kwenye Tumbo la mgonjwa na yeyote ambaye angejaribu kumdhuru naye angenyofolewa Roho yake vile vile au huyo Bundi angetoweka tu ghafla na asionekane amepitia wapi kama ambavyo anadaiwa kunyofoa au kumchukua mgonjwa bila watu kumuona mgonjwa amechukuliwaje.

We hujaelewa somo...!!.
Kinachosemwa hapa siyo kwamba BUNDI ndo ana uwezo wa kuua mtu. No. Kwani ukisikia KAKA KUONA ameonekana mahali na watu wakamwekea maji na nafaka unafikri yeye ndo analeta mvua na chakula? Yeye ni kama ISHARA(A sign) kwamba kutakuwa na mvua nyingi etc.
Bundi naye akionekana siyo ataua mtu baali anaonyesha dalili kuwa kuna kitu kibaya kinaweza tokea kama ni kifo, ugonjwa, ajali n.k.
 
Kwani alifika Kitandani kwa Mgonjwa au? Kwa sababu kama Bundi ana uwezo Wa kumnyofoa mgonjwa Roho yake ni kwa nini ahiyari kutoka huko mbali aje karibu na nyumbani halafu aogope kutua kwenye kitanda cha mgonjwa?

Kama Bundi anaogopa kuuawa basi hana uwezo anaodaiwa kuwa nao. Bundi, angalikuwa na uwezo wowote Wa kipekee,Wa kutoa Roho ya mtu angalijiamini kwa kuja moja kwa moja na kutua hata kwenye Tumbo la mgonjwa na yeyote ambaye angejaribu kumdhuru naye angenyofolewa Roho yake vile vile au huyo Bundi angetoweka tu ghafla na asionekane amepitia wapi kama ambavyo anadaiwa kunyofoa au kumchukua mgonjwa bila watu kumuona mgonjwa amechukuliwaje.

Da! haya yote sijui yanatokea wapi...mimi sijasema chochote kuhusu bundi kusababisha kifo cha mdogo wangu nilichosema ni matukio mawili kutokea pamoja na haya yalitokea zaidi ya miaka 30 mimi nikiwa mdogo kwahiyo sikumbuki kila kitu kwa kina.
 
Back
Top Bottom