Bundi aingia ndani ya ukumbi wa Bunge leo asubuhi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Nilichanganya kidogo mambo, unajua leo asubuhi palikuwa na bundi, bundi ‘original’ hapo juu hapo, lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wahusiku ndo shida".Job Ndugai JAN 29,2019-Dodoma

bunge.jpg


======

Dodoma. Huwezi amini lakini ndivyo ilivyokuwa kwamba bundi leo Jumanne Januari 29, 2019 amefungua mkutano wa Bunge.

Ni ndege aliyeonekana leo asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge ambako kila mbunge na watumishi wa chombo hicho cha Dola waliowahi kuingia walimuona ndege huyo.

Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.

Ndege huyu hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, haikujulikana muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.

"Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa," amesema Ndugai.

Kauli ya Spika ni kama iliwapoza watumishi ambao walionekana kuwa na hofu juu ya ujio wa ndege huyo ndani ya jengo la Bunge.

Chanzo: Mwananchi
 
Nilichanganya kidogo mambo, unajua leo asubuhi palikuwa na bundi, bundi ‘original’ hapo juu hapo, lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wahusiku ndo shida".Job Ndugai JAN 29,2019-Dodoma

View attachment 1007609
Hahahaa...... Yule Jah People wa Njombe yupo mjengoni?

Hapa Njombe WALAWI wanafunga na kuomba ili pepo mchafu arudi hukohuko alikotokea!
 
Akiwa amejawa na hali ya uoga spika Ndugai amesema amelazimika kutolea maelezo hali iliyojitokeza bungeni baada ya kuchanganya baadhi ya mambo bungeni na kujitetea kuwa amemuona bundi juu ya majengo ya bunge.
Kumbe wanaamini ushirikina hao watu
FB_IMG_1548747047320.jpeg


In God we Trust
 
Back
Top Bottom