Bundi aingia ndani ya ukumbi wa Bunge leo asubuhi

Nilichanganya kidogo mambo, unajua leo asubuhi palikuwa na bundi, bundi ‘original’ hapo juu hapo, lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wahusiku ndo shida".Job Ndugai JAN 29,2019-Dodoma

View attachment 1007609

======

BUNGE: Ndege aina ya Bundi ameingia ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma asubuhi ya leo wakati Mkutano wa 14 wa Bunge la 11 ukianza kikao chake cha kwanza lakini Spika wa Bunge Job Ndugai aliwatoa hofu wa Bunge kuwa Bundi wa mchana hana madhara kama wa usiku.
BUNDI NI NDEGE KAMA NDEGE YEYOTE WA KAWAIDA..WALA HANA MADHARA YOYOTE KWA MAISHA YA BINADAMU....NCHI YETU WANAOAMINI UCHAWI NA USHIRIKINA NI ASILIMIA 93. PAMOJA NA USOMI WOTE WA KUTENGENGEZA VIBIRITI NA VYUMA WATANZANIA BADO WAOGA WA NDEGE ASIYEONGEA AU ASIYE NA MIKONO??? USOMI WA WATANZANIA UPO WAPI? SPEAKER UNALIABISHA BUNGE NA NCHI YETU.
 
Bundi ni ndege wa kawaida mwenye aibuaibu sana.Hupenda kupumzika mchana na usiku kujitafutia chakula.Ndege huyu ana sifa nyingi.Lakini moja wapo ni uwezo wake wa kunusa na kuhisi harufu hasa ya vitu vilivyooza.Kwa mfano:Iwapo nyumbani kuna mzoga basi bundi huipata harufu hiyo kutoka masafa ya mbali na kusogea karibu ili atwae mzoga huo.
Vivyo hivyo,hata kwa binadamu mgonjwa wa muda mrefu ambaye mwili wake huanza kutoa hadi harufu ya uvundo,bundi huwa anaipata harufu hiyo.Sasa basi,mule bungeni yawezekana kuna mzoga au kuna mgonjwa anayetoa harufu ya uvundo kiasi cha bundi huyo kuvutiwa nao.Je,ni nani amevunda pale bungeni aidha kwa ugonjwa au vinginevyo?Kuna mtu anaumwa kavunda mule.Tuchunguze kabla bundi hawajajaa mule.That's where we will articulate our parliament as the Parliament of owls!Sitanii.
 
Nani kakudanganya kuwa bundi hula mizoga?. Bundi hali mizoga. Bundi huwinda wanyama wadogo wanaotembea usiku. ( panya, nyoka, vyura, paka , Hata sungura, ndege wlio ndani ya viota.).
Wanaokula mizoga, ni mwewe, tai,na kunguru,
Huyo bundi kaleta noma hapo bungeni, tena mchana kweupe. Huo mswaada wa vyama hauwaachi salama. Ngoja wajidanganye eti bundi wa mchana hana madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajabu yake huyo bundi anapenda harufu ya mizoga.Na ana uwezo wa kuitambua harufu ya uvundo na mizoga akiwa mbali sana.Ajabu!!
 
Atulie si kazoea kutafutia wabunge wenzake mwarobaini

Ndugai alikuwa anacheza na CAG anafikiri anacheza na wagogo wenzie wanaofuga fisi; onyo lilitolewa humu na mzee mmoja maarufu humu JF kuwa professa Assad sio mtu wa mchezo kwani amesoma sana Elimu Dunia na Elimu akhera licha ya Kuwa gwiji wa accounting!! Kazi unayo BLAI!!!!
 
We hujaelewa somo...!!.
Kinachosemwa hapa siyo kwamba BUNDI ndo ana uwezo wa kuua mtu. No. Kwani ukisikia KAKA KUONA ameonekana mahali na watu wakamwekea maji na nafaka unafikri yeye ndo analeta mvua na chakula? Yeye ni kama ISHARA(A sign) kwamba kutakuwa na mvua nyingi etc.
Bundi naye akionekana siyo ataua mtu baali anaonyesha dalili kuwa kuna kitu kibaya kinaweza tokea kama ni kifo, ugonjwa, ajali n.k.
Mkuu jamaa ana kichwa kizito sana. Huwa namuona mada zake za kiwaki humu jamvini. Dini zimem-blind. Kuna mambo mengine lazima ufungue akili na kuweka pembeni utashi wa kutanguliza imani.
 
Hahahaha hahahaha.....
Nilichanganya kidogo mambo, unajua leo asubuhi palikuwa na bundi, bundi ‘original’ hapo juu hapo, lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wahusiku ndo shida".Job Ndugai JAN 29,2019-Dodoma

View attachment 1007609

======

Dodoma. Huwezi amini lakini ndivyo ilivyokuwa kwamba bundi leo Jumanne Januari 29, 2019 amefungua mkutano wa Bunge.

Ni ndege aliyeonekana leo asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge ambako kila mbunge na watumishi wa chombo hicho cha Dola waliowahi kuingia walimuona ndege huyo.

Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.

Ndege huyu hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, haikujulikana muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.

"Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa," amesema Ndugai.

Kauli ya Spika ni kama iliwapoza watumishi ambao walionekana kuwa na hofu juu ya ujio wa ndege huyo ndani ya jengo la Bunge.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom