Bulembo: Hatutawaruhusu upinzani kwenda Ikulu

Bulembo: Hatutawaruhusu upinzani kwenda Ikulu

Mbona Lowassa alisema ukawa itaingia ikulu asubuhi kwani yeye ndio mwenye maamuzi na ikulu.?
Acha chuki binafsi. Kauli ya huyo Bulembo ni ya kichochezi tofauti na ya Lowassa.Kusema wapinzani hawataingia ikulu ni vitisho na uchochezi tume ya uchaguzi hatua kwa huyu mtu.
 
Aisee hawa ndo waliokuwa wanafikiri tz ni yao, kama huo ndo msimamo wao kwanini tutafanya uchaguzi, kwanini tutumie gharama kubwa kwaajili ya vitu ambavyo wao tayari wana majibu na misimamo?
 
Kama walidiriki kuiba sera za Chadema, Elim bure mpaka chuo kikuu, vifaa vya ujenzi kushushwa bei, mikoa ya ziwa kunywa maji ya ziwa. Unaona ajab gani kuiba M4C??
CCM weshachanganyikiwa. Bulembo anasema tena kwa sauti kuubwa (ITV habari saa 2 usiku leo) atii; Hatuwezi kuwapa Ikulu watawale hao wapinzani. Kwa vyovyote vile hatuwapi.
Hivi ingelikuwa ni ukawa wamesema tu kwamba hata iweje hatukubali kushindwa hata tukishindwa, leo NEC wangelisema nini???
Viongozi wa ccm mmekwisha habari. Chama chenu mmekiua wenyewe. Hakuna yeyote anayesema mlifanya nini bali ni ahadi kwa sababu mmejua kuwa ahadi zenyu tangu Mkapa, HAZITEKELEZEKI. Lakini mmezoea kuwadanganya Watz kama watoto wadogo tu. Mwaka huu 2015 ni tofauti. Ikulu mtaitoa tuu kwani nguvu ya umma imeamua kuwatoa

mikoa ya ziwa???? ndo mikoa gsni hiyo mkuu???
 
nasikitika sana kumjadili mtu duni kama bulembo , Mungu nisamehe .
 
Kiboko yake ni kijana mmoja anaitwa ulole ulole,alimwangusha kwenye udiwan kata ya makumbusho dar na ngoma kwenda ukawa,hana mvuto hata kidogo huyo
Aisee nakumbuka ilikuwa 2010 jamaa tulilila hela zake then tukali chenchia mbaya, ujanja wake ilikuwa kununua mawakala, dadadeki vituo vyote tukaweka mawakala wanachuo na home boys kibao wenye uchungu mbona alinyooka.... Juma uloleulole mtoto wa uchungu wa mwana ajuae mzazi....
 
Bulembo ni jina alilopewa huko mara kwakuwa alikua muuza urembo "BULEMBO".

Anashika rekod kwa jumuiya ya wazazi kama mwenyekiti duni sana kielimu katika wote waliopita jumuiya hiyo. (STD VII).

Amejaliwa sana kuongea japo huwa hapimi na kutafakari anachoongea.

Ni mzigo ndani ya CCM kama jumuiya anayoifilisi ilivyo, So yuko tayari kuongea lolote akiamini analinda CV yake ndani ya Chama!

Hiri rimjaa vipi?
Wakti tuko shule kuna jamaa mmoja wa kipare alikuwa anaitwa Mbwambo.Jamaa alikuwa mtu wa Kilaji sana na akilewa alikuwa akichekesha watu anapoeleza kwanini wazazi wake walimpa jina la Mbwambo!Akiwa amelewa alikuwa akienda ubaoni na chaki yake anaandika neno MBWA peke yake halafu anaunganisha na neno MBO akimalizia na O na anatamka kwa madaha kabisa MBWA-MBO**!
Nikirudi kwa Bulembo naweza kumfananisha na Mbwambo kwa kulitaja jina la
Bulembo kwa kuanza na BURE na kuunganisha na MBO**7 ili tumwite BURE-MBO**OOOOOOO!!!!!!
 
Mbona lowasa na sumaye ni watoto wa ikulu kitambo kuliko kikwete na bulembo?
Hiyo moja pili yeye ni nani nchi hii mpaka aseme hivyo?
Tatu atatumia njia gani kuwazuiya hawa watoto wetu wa kitanzania ambao wanaijua ikulu vizuri?
 
Mwigulu kafukuzwa? Kweli wamedata, tunaomba hiyo clip ya Bulembo jamani, hivi ndio vitu vya kutuma ile mahakama ya Bensouda huko the Hague.. Tuweke evidence zote manake hawa watu wanafikiri hii nchi mali za mama zao

Huyu Bunini sijui.....anaweka peupe ile kitu kinaitwa JOINT CRIMINAL ENTERPRISE (JCE). Ataisaidia sana ICC hapo baadae.
 
kweli ccm washaona kuwa ukawa wameisha shinda hivyo nikuwaogopesha wapinzani.Alafu kesho nepi atakuja kupingaa
 
Nimekuwa nikikuona na kukusikia ukimnadi mgombea wetu wa CCM Dr. Magufuli kwenye kampeni zinazoendelea. Unafanya kazi kubwa ukizingatia kuwa wewe ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Mjumbe wa Kamati Kuu na kada wa CCM.

Ndugu Abdallah Bulembo,chunga kauli zako. Leo,umesikika ukisema kuwa CCM haiwezi na haijawahi kuwaruhusu wapinzani kwenda Ikulu. Huu ni ufínyu wa kisiasa,kidemokrasia na kauli hatari. CCM haina mamlaka wala haki ya kuruhusu washindi kwenye uchaguzi.

Kauli hiyo itazua shaka na matayarisho ya kupambana. Hakuna haja hiyo. Chunga sana. Achana na fikra za chama kimoja. Kidemokrasia,wananchi ndiyo wanaowachagua na kuwaruhusu wa kwenda Ikulu. Si CCM. Epuka kukiangamiza chama chetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Huyu jamaa ni STD 7 mkuu! Hata hajui ni kipi aongee, ni wakati gani na ni wapi. Hawa ndio wanaoiua CCM! Mwangalie Mwigulu na Lusinde walivyoigharimu CCM kule Arumeru Mashariki na almanusura Igunga. CCM hawako makini.
 
CCM wangekuwa wametawala vizuri muda huukazi yao ingekuwa rahisi sana wangekuwawanazunguka kwa wananchi na kuwaambia;ONENI mahakama ya rushwa inavyofanyakazi.ONENI reli ya kati ilivyoimara na usafiri watreni kwa ujumla.ONENI elimu bora tuliyoianzisha.ONENI elimu bure tunayowapatia.ONENI sekta ya viwanda inavyoshamiri.ONENI walimu walivyo na maisha bora.ONENI wanafunzi wote wana mikopo namabumu hayachelewi.ONENI zahanati katika kila kata.ONENI uzalishaji ulivyokuwa.ONENI tumekuwa tukitoa milioni hamsini kilakijiji.ONENI kilimo cha kisasa.ONENI bandari zetu zilivyobora.ONENI sarafu ya Tanzania ulivyopandathamani.ONENI maisha bora kwa kila mtanzaniatulivyofanikiwa.ONENI flyovers dar es salaamONENI madini yetu yanavyonufaishawatanzania.ONENI hakuna fisadi anayezunguka mtaaniwote wapo jelaONENI kilimo cha mkonge kilivyokuwa.ONENI wakulima wa pamba walivyo namaisha bora.ONENI wakulima na wavuvi walivyo na maishaboraONENI hiki ONENI kile, hii ndiyo ingelikuwakazi ya CCM kila sentensi wangeanza naONENI halafu ndiyo wanafuata na ilani mpyalakini kutokana na utawala wao mbaya kilakitu hapo juu wanaanza na TUTAFANYAkanakwamba nchi hii miaka yote ilikuwaikiongozwa na nyani vitu vyote alivyovianzishaNyerere ikiwamo viwanda elimu bure nkwamevivuruga sasa wanataka kuvirudishamliviharibu kwanini kama si kupotezeanamuda?Mambo yote waliyovurunda wamemtuma mgombea wao kushangaa, ANASHANGAA hiki ANASHANGAA kile anamalizia kutoa ahadi tumsubiri miaka mitano ijayo aje kushangaa tena
 
Nimesikia hii kauli ya Bulembo, mwanzo nilisikitika sikujua shule yake. Huyu si ndiye yule alishindwa udiwani kule knyama na yule baba wa kijiweni. Ndo kapewa majukumu makubwa hivyo na CCM, very interesting
 
Aisee nakumbuka ilikuwa 2010 jamaa tulilila hela zake then tukali chenchia mbaya, ujanja wake ilikuwa kununua mawakala, dadadeki vituo vyote tukaweka mawakala wanachuo na home boys kibao wenye uchungu mbona alinyooka.... Juma uloleulole mtoto wa uchungu wa mwana ajuae mzazi....

Haaaaa haaaaaa,mm nilikuwepo pia aisee,yule bwana mdogo wa ali maua alimnyoosha bulembo,wasiomjua wanadhani ni jembe kumbe kimeo,yaani ccm wameishiwa mbinu mpaka wanamtegemea bulembo!!!
 
Akiongea kwenye kampeni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM amesema chama hicho hakitawaruhusu wapinzani kwenda IKULU.

NB;Hivi CCM ndo inaruhusu watu kwenda IKULU kauli hii inaashiria kuwa hata kama upinzani utashinda hawatakubali washike madaraka.

Ninaomba wanasiasa wachunge ndimi zao wakati huu wa uchaguzi kwani hata CCM wakishinda wapinzani wataamini kuwa wameibiwa hali itayoleta machafuko na kupelekea mauaji acheni vitisho vyenu maana wanaoamua nani aende ikulu ni wananchi na sio CCM.

ndio taasisi anayoitetea Mzee Mwanakijiji ...
 
Last edited by a moderator:
Ata mm niliskia pia, asa nkafkiria wao hawawez kuwaruusu wapinzan kwenda ikulu wakiwa kama akina nan? Manaake mm mwananch ndo naamua nan aende ikulu na nan asiend, sio bao la mkono ilo kwel?
 
hatutaibiwa kura, vijana indeni kura zetu, Lowasa Ikulu lazima, hizi hazikukushutua ila ya upande wa pili, usitoe kibanzi kwa mwenzio kabla yako
Kauli hii imenistua kidogo. Akihutubia umati wa wananchi waliofika kusikiliza kampeni za chama cha kijani, mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi amesema wao watakuwa tayari kufanya yote ispokuwa hawataruhusu mtu kuingia ikulu. Mimi ninavyojua wananchi kupitia kura zao ndio wenye mamlaka ya kuamua nani aende ikulu.

Kimsingi sijaelewa ana maana gani, kwa kuwa kauli hii ni tata. Wataalamu wa methani mjaribu kuidadavua kauli hii.

Source of the quote> ITV Habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom