Bulaya adai ripoti ya Machi 8 ya Simba na Yanga bungeni

Bulaya adai ripoti ya Machi 8 ya Simba na Yanga bungeni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,380
Reaction score
18,750
Mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya ameibuka bungeni na kuuliza swali la kutaka kujua ni nini kilitokea hadi kuahirishwa kwa mechi ya dabi kati ya Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 ambapo ameomba kupatiwa majibu.

Baada ya kuuliza swali hilo, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson aliagiza ajitokeze mbunge ambaye ni shabiki wa Simba ili ajibu swali hilo ambapo mbunge wa viti maalumu, Esther Matiko amejibu kwa kumnukuu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) kuwa ni lazima kanuni za mpira ziheshimiwe.

Hayo yamejiri wakati Naibu Waziri Mwinjuma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Hassan Kungu aliyetaka kujua ni upi mkakati wa Serikali wa kuandaa timu ya Taifa ya soka madhubuti itakayowakilisha Taifa katika mashindano ya AFCON 2027, Tanzania ikiwa mwenyeji.

 
Hao kina Mdee na Matiko nilikuwa nawakubali sana ila sasa hivi nikiwaona au kuwasikia naona kinyaa tu. Ni mashahidi wanaotukumbusha kuwa hii ni nchi ya hovyo na ina siasa za hovyo.
 
Gwajimanized ponjorozi 🚮🚮🚮🚮

IMG-20250611-WA0040.jpg
 
Back
Top Bottom