Bukoba sirudi tena ng'o

Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,

Hiyo inategemea na mtazamo wako ulikuwa unahitaji nini? Binadamu hatufanani,unaweza ukamtoa mtu hapo Bukoba na kumpeleka Dubai au Tokyo na asipapende! The Soul isn't where it lives but where it Loves.
 
Nimekuwa nikifuatia mada hii tamu na ningependa kuchangia mawazo kidogo hapa.

Mimi ni stronger believer wa democracy na market economy, ila niko against na western liberal democracy na western market economy, na kwa mtazamo wangu Africa haitaondokana na umasiki kamwe kama itaendelea kukumbatia liberal democracy na market economy iliyokuwa designed na western countries...nafafanua.

Democracy tuliyonayo sasa Tz na Africa kwa ujumla ni ile tuyorithi kutoka kwa wakoloni na sasa wakoloni hawa wamekuwa waki-imodify democracy hii kadri watakavyo na huku sisi tukiimbiza na kwenda na mabadiriko hayo pasipo kujali utofauti wetu na west. Kwa maana nyingine tunajikuta lazima tukimbie kabla hatujaanza hata kutambaa. Matokeo yake ni umasikini husio kifani.

Liberal democracy inafanya kazi west sio kwasababu ya uongozi imara wa west, wala sio kwasababu ya uchumi imara. Kwa sababu nature ya west ina support liberal democracy. Tofauti na Tz au nchi nyingine za Africa zilizokuwa na mfumo wa socialism uliokuwa na umuhimu katika kuyaunganisha makabila na watu wa dini/imani mbalimbali, nchi za magharibi hazina makabila, na hivyo partisan haiwi affected na ukabila bali na sera za chama husika. Tz na Africa tuna political culture tofauti na nilazima tuende kwa uangalifu sana katika kui-shape democracy tunayoiona inafaa. Congo, Sudan, Iraq, Burundi, Rwanda, Uganda, Somalia, na kwingineko tumeona liberal democracy inavyochukuwa sura ya shetani na kusababisha umwagaji wa damu. Kwanini??? Kwasababu democracy sio zaidi ya jumuisho la dini, ukabila, social class, na maisha ya kila siku ya binadamu. ...Hivyo basi demokrasia ya magharibi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wetu,,,tunatakiwa tuirekebishe democrasia hii ili ichukuwe shape ya tamaduni zetu, mila zetu, imani zetu, makabila yetu na kila kitu kinacho affect uzalishaji nk.

Markert economy: Market economy ilikuwapo Tz na Africa kwa ujumla kama ilivyokuwa democracy kabla ya wakoloni. Wakati ule mbuzi alikuwa anabadirishwa na gunia la mpunga at a price determined by the market. Kukiwa na mavuno mengi ya mpunga, mbuzi alikuwa anabadirishwa kwa magunia kadhaa, kukiwa na mbuzi wengi basi mpunga ulikwa na thamani na hivyo gunia la mpunga lilikuwa lina command karibu zizi zima la mbuzi. Hizi ni forces za supply na demand ambazo wachumi wa sasa wanajidai kutuletea Tz na Africa, wakituambia kwamba ni magic forces katika allocation za resources.

Sasa tunapokumbatia liberal makert economy mana yake tunakumbatia na upumbavu wake, ambao ni assumption kwamba kila kitu kina market value, na kwamba market value hii ni bora kuliko social value. Mfano, nchi za magharibi ukiunguliwa nyumba yako moto, jirani yako na familia yako wote wanafurahia, na hakuna atakayekupa pole? Kwanini?? Kwasababu moto ulionguza nyumba yako tayari una market value, ambayo ni bima ya nyumba. Sasa sisi waTz nyumba inapoungua ndio kwanza jamii inapoungana na wewe katika kuhakikisha unapata makazi, huu ni wakati ambao social fabric zinaunganishwa katika kuleta maendeleo ya jamii....Sasa tunapokumbatia liberal market economy manake social values ambazo ni muhimu katika kuleta huduma za jamii na upendo katika jamii zinamong'onyoka.

Matokeo yake, mwenye bima ndio atapeleka mtoto shule,,,,kama huna bima na unazeeka basi ni bora mtoto wako abaki nyumbani akuletee kuni, mana mtoto wako sasa ndio bima yako,,,,jamii iliyotakiwa iwe bima imekumbwa na liberal market economy inayosema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!!

Liberal market economy haikujali kama wewe huwezi ku-affect market, kadhalika liberal democracy haikujali kama wewe huwezi ku-convince. Hitimisho ni kwamba vitu hivi viwili lazima viangaliwe kwa undani zaidi ili kupata aina ya democracy na market economy inayotufaa watanzania.

Buoba hamna bahari....bali kuna ziwa Victoria....
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,

SOKONI UMEFIKA; UMEKOSA NN
soko-bukoba.jpg

ndizi.jpg
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,

Kiongozi mi nilijua umezaliwa Tokyo na umekulia huko.....kumbe umetoka Mwanza???!!lol sasa tofauti ya Mwanza na Bukoba sio kubwa saaaana....bahati nzuri nilisoma Mwanza na niliwahi kuishi Bukoba na kufanya kazi pia kwa hiyo sidhani kama kuna ubaya huo ambao wewe unaisema....Bukoba mjini pako salama pengine kuliko miji yote hapa nchini,nilikaa miaka mitatu sijawawi kusikia ujambazi pale wala mlio wa risasi,ndizi za buku mnakula zaidi ya mashababi watatu kwa maana ya kwamba kama una chanzo cha mapato maisha yapo kawaida sana.
 
umetokea mwanza wilaya gani mkuu? mwanza ni jiji sasa utalifananisha na mji? pamoja na kuwa mwanza ni jiji na wewe ndo unatokea mwanza, mimi tanzania hii yote sidhani kama kuna pahara utanidanganya, mwanza ni sawa na mtu aliye vaa nguo nzuri akapaka mafuta usoni, kumbe nguo zake za ndani chafu!! mfano huu unalenga mwanza town ni pazuri sana ila je wilaya zake umefika na ukaona kukoje? kwanza niambie ni wilaya gani mwanza unatoka, au una angalia town to kwa kuwa ni jiji? mfano umeenda wilaya ya ukerewe? kila mzawa wa pale akijenga nyumba nzuri anapigwa chini na mahuti nikiwa mtumishi wa selikari nimeenda kikazi kule, yaani kwa wiki hukosi kukutana na vichaa wasio pungua 20! watu wapigwa koba tu bila sababu! sasa hivi baada ya wagen kuingia ndo angalau.

umeenda kisiwa cha ukara mkoa wa mwz ukaona wachawi wanavyo loga kweupeee!!!! yaani ni bora ungesema umetokea mikoa mingine si mwanza kabisaaa!!! shukuru Mungu wahaya wakupikie matoke na senene +sangala ukale na urudi salama. mwanza kuna maeneo mengine ukienda vibaya kurudi mpaka MUNGU AWE NAWE!!!

Mtoa mada kasema bukoba sio kagera, habari za ukerewe zinatoka wapi!!
 
bwanae mtu kwao wewe urudi usirudi kwani huko ni kwenu ? waache wenye kwao wewe angalia kwenu kunani.
Inawezekana wewe unatabia mbaya ya kudharau wenzako. una taabu sana wewe
Mimi sio mleta mada.

Nafikiri umeniquote kimakosa bila shaka jamaa amekufanya uchape kwa jazba matokeo yake badala ya kufikisha ujumbe kwa mlengwa ukanifikia mimi.

Ila hakuna tatizo ujumbe kaupata bila chenga.

Na kwa niaba yako nawasilisha
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,
Ni kweli wahaya ni watu wanaoongoza miongoni mwa makabila yanayoongoza kwa watu wake kuwa na elimu ya juu na pia uwezo wa kiuchumi. Tatizo lao mimi naona wanawekeza zaidi nje yaani kwenye mikoa ya nje ya kwao kuliko kwao. Angali majumba ya kifahari yaliyopo Dsm na sehemu nyingine za nchi, angalia mashule yanayofanya vizuri, angalia mashirika mbali mbali ya binafsi nk. Wahaya ni matajiri lakini wamewekeza utajiri wao nje ya mkoa wao na wengi ni kama wamehama kabisa kwao ambapo huenda mara moja moja hasa wakati wa misiba tofauti na wachagga ambao wamewekeza kwao vizuri na hurudi kwao kila mwaka kufanya maendeleo ndio maana ukienda vijijini utakuta majumba ya nguvu kuliko hata yaliyopo mjini Dsm na kwingineko
 
We mi nimekaa Bk, miaka miwili, kwa kweli ni pazuri sana, kwanza hali yake ya hewa tu utapenda na maeneo ya kutembelea yapo ingawa si kivile ila kwa Mji kama Bk. ukilinganisha na mingine bado ni pazuri sana, mimi nilikuwa nakaa Kashai, National Housing, karibia na TEMESA, kwa kweli ni pazuri sijui wewe ulitegemea nini hasa mkuu?
 
Wacha tusema ukweli Bukoba ni kubaya tena ni kubayaaaaaaaa mbona wao huwa wanapondea kwa wenzao kazi misifa kwao hawapajengi ukweli ndo huo kama mumechukia kunyweni sumu.
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,

hahhahahah!! huko ukanakoita kwenu Mwanza kumefikia hatua hiyo shauri ya mchango wa wahaya au tuseme watu wa Kagera. Kaama alivyosema Tulimumu wahaya wamekuwa wawekezaji wakuu nje ya Bukoba si kwa majengo na biashara tu kama mtoa mada anavyolenga - kwa kiasi kikubwa hasa awamu ya kwanza imewatumikisha kitaluma bila kuwawezesha kuijenga Bukoba. Aidha wametumikishwa kwa uaminifu tofauti na makabila ambayo yalijikita katika kupora raslimali za nchi hii na kujenga kwao huku awamu ya kwanza ikiwakenulia meno.

hali ya vijijini ni nzuri - mfano uvunaji wa maji - huwezi kuta wahaya wanakunywa maji ya madimbwi wakishirikiana na mifugo kama wafanyavyo kwa mtoa hoja. kuna mifano mingi lakini hapa si mahala pake
 
Ni vigumu kuuona uzuri wa bukoba kama ulienda na Bus. Nahisi wewe mleta mada utakuwa ulienda bukoba na bus za Bunda, ukafika stand la vumbi kisha ukaenda kuishi Lodge za Uswahilini. Laiti ungekuja na ndege ukaenda kuishi hoteli nzuri kibao zilizojazana Uganda road, Kashura, Uzunguni na Nyamkazi naamini usingekuja hapa kuongea huu upuuzi.

Hivi kama una unakuja Dar ukashuka pale ubungo terminal alafu ukaenda kuwatembelea ndugu zako wanaoishi Kwa mtogole, mbagala, au temeke kisha ukarudi makwenu unafikiri mtu akikwambia dar ni pazuri kuna viwanja vikali na watoto wazuri utamuelewa???

Jifunze kutembeatembea kila upatapo fursa ya kusafiri.
Ni kweli mkuu, mleta uzi inaonyesha alishukia ile stendi ya vumbi pale akaibukia mitaa ya uswazini, basi akafikiri Bukoba yote iko hivyo.
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,
Habari ya bukoba mkuu
 
Nimefika hapa takribani wiki moja iliyoisha yani mjii huu ni tofauti na nilivyouzania kutokana na majigambo ya ndg zetu wahaya, miundo mbinu na mji ulivyokaa basi taabu kweli kweli, natamani kilichonileta huku nimalize fasta nirudi zetu kwetu mwanza,,
Nenda hata ss hatukutak mkuu
 
Back
Top Bottom