Ni kweli wahaya ni watu wanaoongoza miongoni mwa makabila yanayoongoza kwa watu wake kuwa na elimu ya juu na pia uwezo wa kiuchumi. Tatizo lao mimi naona wanawekeza zaidi nje yaani kwenye mikoa ya nje ya kwao kuliko kwao. Angali majumba ya kifahari yaliyopo Dsm na sehemu nyingine za nchi, angalia mashule yanayofanya vizuri, angalia mashirika mbali mbali ya binafsi nk. Wahaya ni matajiri lakini wamewekeza utajiri wao nje ya mkoa wao na wengi ni kama wamehama kabisa kwao ambapo huenda mara moja moja hasa wakati wa misiba tofauti na wachagga ambao wamewekeza kwao vizuri na hurudi kwao kila mwaka kufanya maendeleo ndio maana ukienda vijijini utakuta majumba ya nguvu kuliko hata yaliyopo mjini Dsm na kwingineko