Brother Mrisho.. please tap out! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brother Mrisho.. please tap out!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jan 5, 2011.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa wale wapenzi wa Mixed Martial Arts, mtaelewa nikisema mtu kawekwa kwenye submission possition.

  Ina maana mikono, miguu, shingo, tumbo na mwili mzima umekabwa kabali na huwezi kujinasua na pumzi yakuishia.

  Kinachofuata kwa kukosa afueni ni kuchapa kiganja chako mara kadhaa kwenye sakafu au mwili wa aliyekuweka kwenye submission na hivyo una tap out, kujisalimisha na kupoteza pambano.

  Sasa kaka yangu Khalfani Mrisho, tayari yupo kwenye submission position, lakini anataka eti kufa kiume hataki kuonekana kashindwa, namuambia please tap out!

  • Kachakachua na kuchakachulishwa akaapishwa haraka haraka
  • Alidai hakuna haja ya katiba, sasa kaunda tume
  • Kadai Demkrasia imekuwa nzuri, lakini polisi wake na Serikali yake inawanyanyasa wapinzani.
  • Kadai kaunda kikosi bora, lakini ni mizoga ileile imemwagiwa chumvi na maji inukie vyema
  • Umeme kacheza nalenale ili apate kura ya kula, sasa nchi kiza hata ushuzi hauonekani kwa kurunzi
  • Kashindwa kwa makusudi kesi ya Dowans, sasa ushahidi kila kona unaonyesha wazi uzembe wa Serikali yake na yeye mwenyewe
  • Alidai tutakuwa na neema ya Chakula kwa mvua nyingi na mabwawa ya umeme kufurika, Hali ya hewa wanadai tuendako ni kiama, tujiandae kwa njaa kali
  • Kachapisha noti mpya, huku nyingine zimeibiwa hata kabla hajaapishwa uupya
  • Kadai ni tatizo la uchumi wa dunia, tunajua ni matumizi mabaya ya Serikali yake na wapanga uchumi wasio na tija wala nia ya kuhakikisha uchumi wetu unakua
  Niendelee?

  Nawaachia muongezee wenyewe, ila mimi namwambia, please tap out!
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndiyo unastuka leo au unazuga tu. Mwenzio naufanyia kazi msimamo wako kuwa TZ hakuna upinzani na kwamba CDM ndiyo ovyo kabisa na nimeachana na siasa nimejiunga na ufisadi ....................... kwa msaada wako
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Kaka hasira za nini tena?
   
Loading...