Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ndogo ya Mbowe, Superitendent Jumanne Malangahe atoa Ushahidi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Mahakam_Leo_imeanza_rasmi_saa_5%3A00_asubuhi_hii_Kama_ambavyo_Jaji_alisema_Jana.%0A%0APicha_Mh...jpg


Baada ya Mawakili wa Utetezi kuweka pingamizi kuhusu ushahidi wa Afande Jumanne, ikakubaliwa kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ili kupata majibu halali ya kisheria kutokana utata uliopo.

Kesi hiyo inaendelea leo Mahakamani hapo

=====

UPDATES

=====

Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe ameingia mahakamani amewasalimu watu "Bwana Yesu asiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Asalam aleykum l"

Watu karibu wote ukiondoa makarao, Wameitikia "Amen, Milele Amina, Aleykum Muislam Mwenyekiti"

Jaji ameingia sasa

Kesi inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Pius Hilla, Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Esther Martin, Nasorro Katuga, na Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala anamtambulisha Wakili PAUL KAUNDA kuwa wakili mpya wa mshtakiwa wa Pili.. Pia anawatambulisha

Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kiwhelo
Dickson Matata
Alex Massaba
Maria Mushi
Khadija Aaron

Wakili wa Serikali: Tutakuwa na Mashahidi 6 Na vielelezo 4, Na Leo tuna shahidi Mmoja Tunaomba Kuendelea, Lakini Kabla ya Kuendelea Leo tunaona Kuna Utambulisho wa Wakili Mpya PAUL KAUNDA, Je Instructions za Yule wa Mwanzo zimeisha tupate Utaratibu wa Mahakama..

Kibatala: Wakili Msomi Mwenzangu amenielewa Mwanzo Nimesema Kwamba Wakili John Malya ameanza Kwenye Mahakama Nyingine na Punde atakapofika nitamtambulisha, Huyu PAUL KAUNDA hakuwahi Kuwa kwenye kesi hii hapo Mwanzoni ila Kuanzia sasa tutakuwa naye

Wakili wa Serikali: Kama ni hivyo imeeleweka

Jaji: Kwa hiyo anajiunga na ninyi kuanzia Leo

Kibatala Ndiyo

Jaji: Mashtaka Mmesema Mna vielelezo Vingapi

Wakili wa Serikali: Vinne

Jaji: Upande wa Utetezi Mpo tayari Ndiyo

Jaji: Jina

Shahidi: Superitendent Jumanne Malangahe

Jaji: umri

Shahidi: 46

Jaji: Dini

Shahidi: Muislamu

Shahidi: Wallah wabillah watallah Nathibitisha Ushahidi nitaotoa utakuwa ni Kweli na Ukweli Mtupu, Eeeh Mwezi Mungu nisaidie

WS: Umesema Wewe ni Askari Polisi, Je Shughuli zako Unazifanyia wapi kwa Sasa

Shahidi: Wilayani Arumeru Mkoani Arusha

WS: Una nafasi gani hapo Wilayani Arumeru

Shahidi: Mkuu wa Upelelezi, Wilaya ya Arumeru

WS: Majukumu yako ni Yapi

Shahidi Kuzuia Uhalifu
Kukamata watuhumiwa
Kuwapekua watuhumiwa
Kuwaongoza Askari Waliochini yangu ktk Shughuli ya Upelelezi

WS: Kuna Mtu Mmoja anaitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya, Elezea Mahakamani kama Unamfahamutu huyu

Shahidi: Namfahamu

Wakili wa Serikali: Tangu lini

Shahidi 05 August 2020

Wakili wa Serikali: ilikuwa je Mpaka Unamfahamutu

Shahidi: Baada ya Kumkamata pale Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Ilikuwa je Ukamakamata

Shahidi: Baada ya Kuwepo Kwa Taarifa Kwamba ajihusisha Kula Njama za Kutenda Vitendo Vya Kigaidi

WS: Vitendo gani Vya Kigaidi alivyokuwa ajihusisha navyo

Shahidi: Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Maeneo yenye Mkusanyiko Kama Vil Masoko, Kukata Miti na Kuweka Barabarani, Ikiwemo na Kuwadhuru Viongozi wa Serikali, Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya

Wakili wa Serikali: Wakati Unamkamata ni Mazingira gani ambayo Ulimkamata hapo Madukani

Shahidi: Siku hiyo Hapo Rau Madukani tulikuwa na Askari Wenzangu ambao Jumla tulikuwa Watano, Ambapo Tuliongozwa na ACP kingai ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha


Martin Maranja Masese
@IAMartin_
·
4h
WS: Na wewe ulikuwa wapi

Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru

Shahidi: alikwepo Pia Inspector Mahita, alikwepo Detective Coplo Francis na Detective Constable Goodluck

WS: Hao ni Askari wa Wapi

Shahidi: hao ni Askari alikuja nao Afande Kingai, alikuja nao Arumeru

Shahidi: Ukamataji Ulifanyika Majira ya Saa Saba Mchana Katika Maeneo ya RAU Madukani, Ambapo tulifika wote sisi watano na Tuligawanyika katika Maeneo Mawili ambapo Eneo Moja alikuwa akiongoza Afande Kingai, Mimi Mwenyewe na Detective Constable Goodluck

LEneo lingine alikwenda Inspector Mahita na Detective Coplo Francis Ambapo tulijigawa Kwa Upande wa Kulia na Kushoto

WS: Kulia na Kushoto Mwa Nini

Shahidi: Mwa Kibanda ambacho tulipata Taarifa Kwamba Wapo pale Ambapo Mohammed Ling'wenya alikuwa na wenzake wawili

WS: Wenzake Wawili ni akina nani

Shahidi: Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo na Moses Lijenje alimaarufu kama Kakobe

WS: Sasa Baada ya Kuwa Askari mmejigawa mara Mbili kama Mlivyo Sema Nyinyi Askari mlifanya nini

Shahidi Maeneo waliyo kuwa watuhumiwa hao palikuwa na Njia Mbili

Jaji: Naona Kama anatoa Ushahidi Kwenye Kesi Kubwa na Siyo Kesi Ndogo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Ulimkamata Ulimpeleka Wapi

Shahidi: Baada ya Kumkamata na Kumfanyia Upekuzi nilimpeleka Katika Kituo cha Polisi Kati Moshi

WS: Sasa Kwenye Gari alibaki na nani

Shahidi: alibaki na ACP Kingai, Detective Constable Goodluck, na Coplo Francis wakati Mimi na Inspector Mahita tulienda Kituoni kukabidhi Unga unazaniwa Kuwa Madawa ya Kukevya

Shahidi: Tuliondoka na Mohammed Ling'wenya kwenda Maeneo Mbalimbali ambapo tuliambiwa tumgeweza Kumpata Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Maeneo gani hayo

Shahidi: Rau Madukani, Pasua, Aishi Mpaka Boma, Maeneo ambayo yeye Mohamed Ling'wenya alikuwa akiyataja

Shahidi: Ni yeye Kutuongoza na Kutushauri Kwa hiari yake tupite Maeneo mbalimbali

ilipofika Saa 3 Kuelekea Saa 4 tulikuwa Chakula Maeneo ya Boma tukiwa na Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya Akiwa kwenye hali Nzuri

ulirudi Moshi Kwani tulikuwa hatujafanikiwa Kumpata Moses Lijenje,

WS: Meneo hayo yote mliyopita Mlikuwa nani nani

Shahidi: Ramadhan Kingai, Mimi Mwenyewe, Inspector Mahita, Detective Constable Goodluck, Coplo Francis na Dereva wa Gari hilo ambaye ni Detective Constable AZIZI

Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Mohammed Ling'wenya alikuwa wapi

Shahidi: Alikuwa mekaa katikati

Wakili wa Serikali: na Mtuhumiwa Adam Hassan Kasekwa alikuwa amekaa wapi

Shahidi: amekaa Nyuma, baada ya Siti za Katikati

Wakili wa Serikali: Baada ya kutokufanikiwa Mlimpeleka wapi Mtuhumiwa

Shahidi: Tulirudi Kituo cha Polisi Kati Moshi, Tukawakabidhi kwa Askari wa Chumba Cha mashitaka

Wakili wa Serikali: Muda gani

Shahidi: Saa Nne Kuelekea Saa Tano za Usiku

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa kabibidhi kwa Askari wa Chumba Cha Mashtaka nini kilitokea

Shahidi: Baada ya Kuhakikisha Mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya Kupokelewa aliulizwa Hali yake akasema Nzuri

Wakili wa Serikali: aliweka Wapi

Shahidi: Mahabusu

Wakili wa Serikali: Wewe na Askari Mliokuja Kituoni Mlifanya nini

Shahidi: Tuliondoka kwenda Kuelekea na Shughuli zingine za Kiupelelezi

Wakili wa Serikali: baada ya Kumkabidhi Kituo cha Polisi Moshi alikaa Kwa Muda gani

Shahidi: alikaa Mpaka Asubuhi ya tarehe 06 August 2020

Wakili wa Serikali: nini kilitokea

Shahidi: Mimi na Afande Kingai tulifika pale, Nikamchukua Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mwenzake Kwenda Kumtafuta Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kumchukua Mohamed Abdilah Ling'wenya kwa Shughuli za Kiupelelezi

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Sijasikia Mahali ambapo Shahidi amesema alikwenda Kwa Shughuli za Kiupelelezi

Wakili wa Serikali: Naomba Nikumbushwe

JAJI: Kumtafuta Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Asante, ni Maeneo gani sasa Mlienda Kumtafuta Moses Lijenje

Shahidi: Moshi Mjini, KCMC, Rau Madukani, Pasua, Himo, Aishi Hotel, Boma na Arusha Sakina

WS: Mlipata..?

Shahidi: Hapana, Tulimkosa na Kuamua Kurudi Kituoni, na Tulipofika Kituoni pale Moshi Afande Kingai alisema amepokea Maelekezo tuwapeleke Watuhumiwa Dar es Salaam

WS: Sababu za Kuwa leta Watuhumiwa Dar es Salaam ni nini

Shahidi: Kwa sababu Shauri Lilifunguliwa Kituo cha Polisi Kati DSM, Aina ya Uzito wa tuhuma zilizokuwa zinawakabili watuhumiwa, Tulitakiwa kwa namna yoyote ile Kuzuia Uhalifu Ulipokuwa unata Kufanyika

WS: Baada ya Kingai Kukwambia inatakiwa Watuhumiwa Kuwapeleka DSM nini Kilifanyika

Shahidi: Saa Moja Jioni Tulianza Safari ya Kuelekea DSM, Tulipofika Njia Panda Ya Himo, Gari yetu ilipata Matatizo ya Kiufundi, Afande Kingai akapiga simu kwa kaamanda wa polisi Kilimanjaro

Baada ya Kukaa pale tuliagiza Chakula tukiwa na Mohammed Ling'wenya Akiwa na Afya Nzuri bila tatizo Lolote

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukaa pale Muda gani Safari iliendelea

Shahidi: Ilifika Gari ya aina ya FOTON station Wagon ikiendeshwa na PC Wendo, Tukaanza Safari

WS: Mpangilio wenu Kwenye Gari Ulikuwaje

Shahidi: Mbele alikaa Kingai na Dereva wa Gari hilo, Kati Katikati nili Kaa Mimi, Mohamed Ling'wenya na Mahita Upande wa Kulia Na Nyuma alikaa Adam Kasekwa Detective Constable Goodluck

WS: Safari yenu iliwafikisha wapi

Shahidi: Safari ya Takribani Masaa Manane ilitufikisha Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Lini Siku ya Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Saa ngapi

Shahidi: Saa Kumi na Moja Kuelekea Saa Kumi na Mbili

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika nini kiliendelea

Shahidi: Alipokelewa na Chumba cha Mashtaka

WS: Nani aliwakabidhi

Shahidi: Mimi Mwenyewe na Afande ACP Ramadhan Kingai

WS: baada ya kuwafikisha Central Dar es Salaam akitokea Moshi hali yake ilikuwaje

Shahidi: alikuwa na hali Nzuri kabisa, kwa Mujibu wa Mafunzo yetu,

Unapopokea mtu Kuna Mambo ya Kuzingatia, Ikiwemo swala la Afya

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Walipokelewa na Kuwekwa Mahabusu na Sisi tuliondoka

WS: Tarehe 06 August 2020 Wakati Mnamchukua Alfajiri Mohammed Abdilah Ling'wenya alikuwa na hali gani

Shahidi: Siku hiyo wakati namchukua Mohammed Abdilah Ling'wenya alikuwa Mzima na hakuwa na Tatizo lolote

Wakili wa Serikali: Kuna Madai kwamba Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya aliteswa akiwa Mikono Mwa Polisi baada ya wewe Kumkamata

Shahidi: Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya hakuwahi Kuteswa hata kidogo Muda wote tulipokuwa naye

Alikuwa Vizuri kuanzia Kituo cha Polisi Moshi na Kwamba angekuwa na Tatizo asingepokelewa

Wakili wa Serikali: VIPI kuhusiana na Ukaaji wake hapo Moshi Kati ya Muda wa tarehe 05 na Tarehe 06 August 2020, Ulipomchukua Kituo cha Polisi Kati Moshi

Shahidi: alikuwa Vizuri Kabisa

Kibatala/ OBJECTION yeye alisema aliondoka, Sasa Kusema Mambo ambayo amesema Kwamba amemkabidhi na Kuondoka ni "HERE SAY"

Jaji: bila Shaka Kwa Kumbukumbu za Mahakama alisema aliondoka Baada ya Kumkabidhi

WS: Siku ile ya tarehe 05 August baada ya Kumkabidhi Kituo cha Polisi Kati Moshi, Kitu gani kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kufika Siku hiyo ya tarehe 05 August 2020 hatukuendelea na Chochote pale

WS: Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya mlimuacha akiwa eneo gani pale Polisi

Shahidi: Aliwekwa Lock up pamoja na wenzake

WS: turudi sasa tarehe 07 August 2020, Baada ya Kumkabidhi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam nini kiliendelea

Shahidi: Tuliondoka Kwa Muda sisi na Kiongozi wetu ACP Ramadhan Kingai

Shahidi: Tukarudi baadae na Baada ya Kufika Afande Kingai alinipa Maelekezo nimuhojo Mohammed Ling'wenya

WS: Ilikuwa Saa ngapi wakati anakupa Maelekezo

Shahidi: Majira ya Saa Moja, Nilianza Kutafuta Chumba, Cha Kuweza kumuhoji

WS: Ilikuwa ni eneo gani

Shahidi: Ni Chumba katika Eneo la Polisi Mjini Kati Dar es Salaam

WS: Baada ya Kutafuta Chumba Nini kiliendelea

Shahidi: Kwenye Saa Mbili nilifanikia Kupata Chumba saa Mbili na Saa Mbili na Nusu nilimfuata Mtuhumiwa Kutoka Chumba cha Mashtaka

WS: Ulitoa Kutoka sehemu gani na Ulienda Kumuhoji sehemu gani

Shahidi: Nilimtoa Chumba cha Mashtaka katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kwenda Kwenye Chumba Jirani palepale

WS: Taratibu gani Ukitumia Kumchukua

Shahidi: Nilisaini Kwa Kitabu cha Detention Register

Shahidi: Tukarudi baadae na Baada ya Kufika Afande Kingai alinipa Maelekezo nimuhojo Mohammed Ling'wenya

WS: Ilikuwa Saa ngapi wakati anakupa Maelekezo

Shahidi: Majira ya Saa Moja, Nilianza Kutafuta Chumba, Cha Kuweza kumuhoji

WS: Ilikuwa ni eneo gani

Shahidi: Ni Chumba katika Eneo la Polisi Mjini Kati Dar es Salaam

WS: Baada ya Kutafuta Chumba Nini kiliendelea

Shahidi: Kwenye Saa Mbili nilifanikia Kupata Chumba saa Mbili na Saa Mbili na Nusu nilimfuata Mtuhumiwa Kutoka Chumba cha Mashtaka

WS: Ulitoa Kutoka sehemu gani na Ulienda Kumuhoji sehemu gani

Shahidi: Nilimtoa Chumba cha Mashtaka katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kwenda Kwenye Chumba Jirani palepale

WS: Taratibu gani Ukitumia Kumchukua

Shahidi: Nilisaini Kwa Kitabu cha Detention Register

WS: Ulisaini Kitu gani

Shahidi: Kuonyesha Mtuhumiwa huyo sasa yupo Mikononi Mwangu

WS: Detention Register ulipata wapi

Shahidi: Kwenye Chumba Cha Mashtaka, Nikasaini Ndipo wakanipatia Mtuhumiwa huyo

WS: Leo hii Ukiiona hiyo Detention Register Unaweza Kuitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Kwa Kuona Sahihi yangu, Ambapo Nilimtoa a Mtuhumiwa Kwa ajili ya Mahojiano.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tunaomba Kupatiwa Exhibit P1 ambayo tuliitumia Siku ya tarehe 20 Mwezi September ambayo tuliitumia Kwenye kesi Ndogo

MTOBESYA: awe Specific kwa anachoomba Kwa Sababu hiyo Nyaraka siyo kwa ajili ya Kesi hii, Kama anataka Kuomba aombe kwa Maombi rasmi

WS: Statement yangu haiko hivyo, Lakini naomba nikumbushwe nilichokiongea

Jaji: sasa tumpatie kwanza halafu tutaona anataka kusema nini mbeleni


Martin Maranja Masese
@IAMartin_
·
4h
WS: Leo hii Ukionyeshwa Detention Register hiyo, Kitu gani Kitakufanya Ukumbuke Kwamba Ulimtoa Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Uwepo Wa Sahihi Yangu

WS: Vitu hivyo Vinapatika wapi Kwenye hiyo Register

Shahidi: Kwenye Sehemu Imeandikwa "OUT" hapo ndipo Utakapoona Saini yangu

WS: Mheshimiwa Jaji naomba tumpatie Kielelezo Shahidi Kwa Utambuzi wa alichokisema

Shahidi anasoma, anakagua kielelezo, anarekebisha na miwani yake vizuri..Anafunua karatasi haraka haraka..

Anatungalia wananchi kidogo kama tunamtizama, anavua miwani yake,

Shahidi: Nimeiona

WS: Elezea Kitu gani Umeona

Shahidi: Uwepo Wa Majina ya Mohamed Abdilah Ling'wenya

WS: Ulixhokiona ni nini na nini

Shahidi: Sahihi Yangu na Sahihi Yake

WS: lipo eneo gani haswa la Detention Register

Shahidi: Majina ya Mtuhumiwa yapo Kushoto na...

MTOBESYA: Objection. Mheshimiwa Jaji hakusema mambo ya kushoto na kulia

Jaji: Sawa sawa

WS: Ungependa Mahakama ifanye nini hiyo Detention Register

Shahidi: Naomba mahakama ipokee kwa utambuzi

Jaji: kwa Utambuzi?

WS: yes

MTOBESYA: Tuna Objection kwenye kupokelewa kwa hii nyaraka, kwanza shahidi hajasema tangu aiache hii nyaraka alionana nayo lini tena..

Kwa sababu Nyaraka inataka Kupokelewa, basi ni ADMISION, na Kwamba Nyaraka inatakakiwa kutolewaa Shahidi awe COMPETENCE Na inaenda Pale ambapo Shahidi ana authontfica

Mtobesya: Kesi ya DPP dhidi Ya SHARIF MOHAMMED

Mahakama ilisema Shahidi anapoomba Kupokelewa Nyaraka Mahakamani, Shahidi aonyeshe kwamba anatambua Nyaraka anayotaka Kupokelewa Mahakamani, Moja ni UNIQUE na ya Pili ni CHAIN Of CUSTODY

Jeremiah Mtobesya: hapa kwenye Chain Of Custody inaenda kwa shahidi kufanya foundation ambapo shahidi anatakiwa kufanya kwenye witness box..Na Kwamba Unique Feature ambayo Shahidi kafanya Siyo ENTRY.. Kwa Mfano Kitabu hiki ni Kweli Kinatumika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Mtobesya: Shahidi hajafanya wala hajaonyesha Kwamba Kitabu hiki kinatoka Central na Features zake ni hizi hizi, Kwa hiyo ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi haja' lay foundation kwa hiyo hajafanya authentication.....

Mtobesya: Na Pili Kwamba Shahidi hajasema Tangu aachane na Hiki Kitabu Tarehe 07 August 2020 Kimemfikiaje Leo hapa Mahakamani, Kwa hiyo Shahidi hajafanya CHAIN OF CUSTODY..

PAUL KAUNDA: kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili nakubalina na yote yaliyowasilishwa na Wakili Msomi Mtobesya..

Fredrick Kihwelo: kwa niaba ya Mshtakiwa Watatu napinga pia kupokelewa kwa nyaraka hiyo na naunga mkono hoja iliyotolewa na Wakili MTOBESYA

Kibatala: pia tunapinga Kwa shahidi Kutoa D. R hata Kama Kwa ajili ya Utambuzi, kwa Sababu kutoa Nyaraka ya Utambuzi ni suala la Kisheria kunapaswa Kuwa na LEGAL NA FACTUAL, Ni Wazi Kwenye Kumbukumbu zako kwamba Nyaraka hii ilitolewa Katika Shauri Dogo la Adam Hassan Kasekwa,

Shauri lile lina hadhi ya Pekee yake. katika hili tuna tatizo na NEXUS Kwa Shahidi Kutoa Nyaraka Kutoka Kwenye Store ya Mahakama, Wenzetu walitakiwa Kuandika Barua au Hatua zingine, Nyaraka hii warudie Mikononi Mwao, Kwa sababu Mahakama Na wao ni Taasisi Mbili tofauti

Kibatala:

Wamezua Wasiwasi Kwa walivyo iomba na Kumpatia Shahidi hapa Mahakamani, Shahidi Hakuongozwa kwa namna yoyote ile kuhusianisha Kuwepo Kwa Nyaraka hii Mahakamani na Yeye Kuja kufanyia Utambuzi, Nyaraka ilikabidhiwa na Mtu Mwingine Kabisa,

Kibatala: hajazungumza chochote Kati yake na Shahidi Msemwa, angekuwa yeye tungefumba macho kisheria, Kwa hili hajaonyesha uhusiano wowote kati yao, Nyaraka inapotolewa kama ID ni prerequisite baadae kwenda kutolewa Kuwa Kielelezo, Kwa hiyo tunapinga kupokelewa kwa nyaraka hii

Kama alivyosema Mtobesya na wenzangu wote

Jaji anaendelea kuandika. M

WS: Tunaomba muda muda mfupi wa hairisho ilikuweza kutoa Hoja zetu, zipo kwenye Soft Copy lakini tutahitaji muda wa kuziprint na kuziwasilisha

WS kwa sauti ya chini sana, kisha akaketi zake

Jaji: upande wa Utetezi mnasemaje

Kibatala: Hatuna pingamizi na hairisho lakini tunaomba lisizidi nusu saa kwa sababu leo tumechelewa kuanza na ni Kwa sababu Ya Ombi lao hao hao upande wa mashtaka

Kibatala anakaa kisha anateta na wenzake kwa umaridadiii

WS Robert Kidando: Zinatosha

Jaji: Basi tunahairisha kwa dakika 30, mpaka saa ngapi

Kibatala: Saa nane kamili iwe kama dakika 35

Jaji: Saa nane kamili

Jaji: Basi nane kamili tutarudi tena kuendelea na Kesi

Jaji anatoka..

Ufafanuzi Kwa kilichotokea mahakamani hadi serikali kuomba hairisho:

Daftari la kuingiza na kutoa mahabusu baada ya kesi ndogo Ya Adam Kasekwa kutolewa uamuzi , utaratibu wa sheria na mahakama nyaraka ile inatunzwa store ya mahakama, swali ambalo mawakili wetu wamejiuliza leo;Down pointing backhand index

1. Imekuwaje kitu kipo store ya mahakama, kimefikaje mahakamani kwa shahidi wa leo?

2. Kama walikihitaji kutumia walipaswa waandike maombi ya kisheria kuomba nyaraka ile ambayo sasa ni mali ya mahakama Itolewe store ya Mahakama iletwe Mahakani leo, hilo halikufanywa...

3. Kitendo cha nyaraka leo (iliyokuwa store ya mahakama) kuibukia Mahakamani ghafla ni kiashiria kwamba kuna mawasiliano ya siri na kinyume na utaratibu wa Mahakama kati ya ofisi ya mashtaka na mahakama kwamba wanakutana na kupanga mambo ya kufanya Mahakamani..

4. Moja ya sababu ya kutupilia mbali kesi ndogo ya Adam Kasekwa juu ya pingamizi lake, Jaji Siyani alisema ameshangaa kwanini mawakili wa utetezi hawakupinga hiki kielelezo, LEO SIYO TU KINAPINGWA BALI KINAKATALIWA KUINGIA MAHAKAMANI KINYEMELA kutoka kwenye store za Mahakama

===

Jaji Kaingia

Kesi inatajwa

Column za mawakili upande wa Jamhuri ipo vile vile

Kibatala:Nilitoa Taarifa awali, Kwamba Wakili John Malya atakapofila nitamuombea Ruhusa, Naomba Sasa Ikukupendeza tumuingize Wakili John Malya ambaye atakuwa na Paul Kaunda kwenye Jopo letu

Jaji: nani ataanza!?

WS: Ataanza WS Abdallah Chavula na Baadae Pius Hilla

WS Abdallah Chavula: Baada ya Kusikiliza Hoja za Mapingamizi kutoka kwa Wenzetu Upande wa Utetezi, Sisi Upande Wa Jamhuri hatukubaliani nao

Na akaeleza Mahakama Kwamba Ushahidi Unaendelea Mpaka Pale Shahidi atakapo authonticate ile Nyaraka, Na Akailekeza Mahakama Kwenye Shauri la DPP Vs Sharif Mohammed au Jina lingine la Athuman na wenzake 6, Shauri la Rufaa ya Jinai la 64 Mwaka 2016

Naomba na sisi tujibu Kuanzia Hapo, Shauri hilo kuanzia Ukurasa wa Saba Mpaka Ukurasa wa Nane, Naomba kunukuu kilichozungumzwa..

Jaji: Haraka Haraka

WS ANASOMA...

WS: huwezi Kuzi' apply test hizi Kwenye kielelezo ambacho ni nyaraka. Sifa hizi zilikuwa Kwenye Kielelezo ambacho ni gari,

Mheshimiwa Jaji Kwa ufupi tu niseme Hoja ya Mwenzetu ambazo amekuwa akisheresha na Kesi hii haziendani

Tulichonacho Mahakamani ni Nyaraka, Mheshimiwa Jaji haya aliyokuwa anayasem hayakuonyesha Uniqueness kwenye Shauri Letu hayahusiani, Ingekuwa ni Bunduki au Simu Hoja yake Ingekuwa na mashiko lakini Kwa kuwa anatoa Nyaraka basi havihusiani

WS: Hoja Nyingine Wenzetu wamejikita sana ni Competence, Naomba nielekeze Mahakama Yako Katika Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE WATATU, lilikuwa ni Shauri la Jinai la Rufaa Namba 354 la Mwaka 2019

Mahakama Ilikutana na Mazingira kama haya

Isipokuwa Wenzetu walikuwa wanatoa Kielelezo Sisi kama Utambuzi Lakini Inafahamika kwamba Kanuni ni zile zile, iwe Unatoa Kwa Utambuzi au Kielelezo,

Wenzetu wanasema Shahidi Siyo Competent, Lakini Kwenye Ukurasa wa 12 Wa Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE WATATU

Ukurasa wa 12 Paragraph ya Kwanza

WS ANASOMA..

WS: Kwenye Hilo hilo naomba nirejeshe Mahakama Kwenye Shauri la DPP Vs Mohammed SHARIF Ukurasa wa 9 Paragraph ya Tatu

WS ANASOMA...

WS: Hapa pia Mahakama ya Rufaa imesisitiza KNOWLEDGE kwamba Knowledge ni suala la Msingi sana,

WS: Na Subject Matter Yetu Leo Mahakamani ni ENTRY ya Utambuzi 07 August 2020 Saa Mbili na Dakika 10 Asubuhi,

Shahidi ameeleza Mahakama Kwamba Majira hayo alifika Kwenye CHARGE ROOM (CRO) ya Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Kwa Malengo ya Kupatiwa Mtuhumiwa

WS: Na Shahidi huyu anasema alipopatiwa Mtuhumiwa aliweka Sahihi Katika Kielelezo ambacho tunataka kipokelewe, na Baada ya Sahihi akaondoka na Mtuhumiwa, Shahidi akahojiwa "Utatabua Vipi hicho Kitabu Ulicho weka Sahihi zako"

Kipi Kitakufanya Utambue, Shahidi Kasema Nitaitambua Kwa Sahihi Yangu, MWISHO akamaliza kwa Kusema hayo yote utayakuta Kwenye Entry ya 07 August 2020..

Mheshimiwa Jaji Kipi Kingine atafanya, Hayo ndiyo ya Kipekee Hakuna Zaidi ya Hayo Kwenye hii Nyaraka tulizotaka Kuitoa

WS: Nikionanisha yalisomwa na Shahidi Katika haya Mashauri Mawili tuliyoya yarejea Hakuna Shaka Shahidi Wetu ana Information ya Subject Matter ambayo ni ENTRY ya 07 August 2020

Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wakaenda Mbali zaidi Kwa Kueleza Habari ya Chain Of Custody

Kwenye Hilo walahu Mwenzetu alikubali Kwamba hana Ubishi Kwamba Kwenye Kanuni ya Chain of Custody InaKuja Kufanyia Maamuzi Baada ya Kuisha kwa Shauri na siyo Katikati Mwa Shauri

Lakini Kasema kwa Lililopo hapa Tulipaswa Ku Establish Chain of Custody

Hakuielekeza Mahakama Kwa Kanuni gani, Kwa Kifungu gani cha Sheria Wala Kwa Maamuzi ya Mahakama, Hakufanya. Bali alichofanya ni Kutoa Hoja isiyo kuwa na Msaada na Sheria.

Mheshimiwa Jaji naomba Nikurejeshe Kwenye Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO Katika Ukurasa wa 17, Kwa Ruhusa Yako naomba Ninukuu Kuanzia Haya Ya tatu

Anasoma...

WS: Katika Shauri hili kilichokuwa Kinabishaniwa ni Nyaraka na Mahakama ikasema Kwamba Hoja ya Chain of Custody inapaswa Kuwa Established Mwisho wa Shauri na siyo Katikati ya Shauri..

Mheshimiwa Jaji naomba niishie hapa nimkaribishe Mwenzangu Pius Hilla Naye aendelee...

WS: Mheshimiwa Jaji Nianze Kwa Kusema Kwamba nayaunga Mkono yite ambayo Mr. Chavula ameya Establish, Na mimi naomba niseme Machache Kuhusiana na Foundation..

WS: Wakili Mtobesya alielekeza Mahakama Kwamba Shahidi hakuieleza Mahakama Kwamba Hiko Kitabu ni Cha Jinsi gani

Wakili Mwenzangu amelisemea hilo namimi Nitaongezea Kidogo, Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyopo Kizimbani Alisha eleza Kwamba akimfikisha Mohammed Ling'wenya Kituo cha Kati Dar es Salaam, Na Kwamba Watu wale waliingizwa Mahabusu, Mheshimiwa hatuna Dar es Salaam Nyingine

Hatuna Kituo kikuu cha Mjini kati Dar es Salaam Kingine, Hakuna Kituo Kingine Cha Kati Dar es Salaam ambacho Mahakama inaweza Kukifikiria zaidi ya Kilichopo, Na Kingine Shahidi alisema kwamba Siku ya tarehe 07 August 2020 alikwenda Kituo cha Kati ambapo aliweka Sahihi Yake Katika

yaraka Iliyopo Mbele yetu

KWA Ushahidi huo ni Foundation Tosha Kwamba Shahidi Ana zungumzia Nyaraka ya Kitu gani, Mheshimiwa Jaji nihame kwenye Foundation nizungumzie alichokisema Kibatala Kwamba Hakuna Nexus na Kwamba Kielelezo kilipaswa Kitoke Kwenye Exhibit Store ya

Mahakama na siyo Kuomba Kama tulivyofanya. Mheshimiwa Jaji Hoja yetu Kwenye hili ni Kwamba Wenzetu Hawapo Sawasawa,. Hawapo Sawa Kwasababu Mheshimiwa Mahakama Yako tukufu haijaelezwa ni Procedure ipi Imekiukwa. Mahakama Yako tukufu haijaelezwa Sheria ipi imekuwa violated.

WS: Mheshimiwa Mahakama Yako Haijaelezwa Kwa namna yoyote Ile Washitakiwa wamekuwa Treated vipi, Mheshimiwa Kibatala anasema Kwamba Trial Within Trial Ya Adamoo Ilishaisha Kule na Exhibit Ilipaswa iwe Store.. Tunakubaliana na hilo ni Separate Case Mheshimiwa Jaji lakini Kiuhalisia uwezi Kulitenganisha Shaurl Lile na Shauri la Msingi Lililopo Mahakamani na Uzuri hapajawahi kuwa na Disposal Order Ya Vielelezo, Tupo sahihi Kuomba Vitu vya Mahakama na Kuendelea Kuvitumia na Wala hatuja violate sheria Yoyote ile

Mheshimiwa Jaji ukizipima hizi Hoja zilizotolewa na Wenzetu ni Hoja yangu kwamba haziwezi Kuzuia Nyaraka Isipolelewe, Haina Uzito wa kuzia Nyaraka Tunayoomba Ipokelewe, Mheshimiwa Pasipo kuichosha Mahakama Yako tukufu tunaomba Mapingamizi yao yatupiliwe Mbali

Jaji anaandika..

Mahakama ipo kimya..

Jaji Utetezi

MTOBESYA anasimama..

Mtobesya: Mheshimiwa nimesikia Mawasilisho ya Wasomi Wenzetu Mawakili wa Serikali,

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji nimesikia Kaka Yangu anasema Kwamba Shauri la DPP na Sharif Mohammed Ukurasa wa Saba

Amesoma Mwenyewe, Naomba na mimi niisome..

Mtobesya anasoma..

Mtobesya: Nashukuru Kusoma kwake kumeleta Msisitizo Hapa Mahakamani, Kwa Wasilisho lake Kwamba Kesi hii haihusiki na Shauri hili amejielekeza Vibaya..

Mtobesya: Kuna sehemu pia amesema pia kwamba Hoja yetu ya Competence kwa Shahidi Kuliko Ushahidi Wenyewe, Ni Kwamba Ushahidi Hauwezi Kujithibitisha Wenyewe, Katika kesi hiyo hiyo YA DPP Vs SHARIF MOHAMMED, Ukurasa wa Nane, Paragraph ya tatu

Ni Kwamba anayepaswa Kukielezea Kielelezo ni Shahidi Mwenyewe, Na Ni Hoja yetu wakati anasoma Nyaraka hajafanya Kufanya ionekane anakijua, Nimesikia Wakili wa Serikali Kwamba Kinachotakiwa kuwa authenticated ni ENTRY Siyo Document..

Sisi tunasema Shahidi anafanya kwa lolote lile Authenticate Lile analosema, Ipo pia Kwenye Kesi Ya SHARIF MOHAMMED, Ukurasa wa Nane aya ya Pili

Mtobesya anasoma...

NA pia alikuwa anasema Kesi ya SHARIF kuwa Haijazungumzia Chain of Custody, Sasa hapo nimekusomea..

Mtobesya: Na Hayo ni Maagizo ambayo Mahakama ya Chini inapaswa kuyafuata, Na Bado tunasisitiza kwamba Shahidi hajafanya hayo,

Nimesikia Kaka Yangu anasema Kwamba nimesema Chain of Custody ni Jambo la Mwisho SIJASEMA HIVYO..

Nimesema Kwamba Kuna baadhi ya Mahakama Zinasemaje Chain of Custody ni Jambo la Mwisho, Lakini tofauti na Kilichopo Mhakamani ni Suala la Prerequisite, Chain of Custody ni Kungalia Ushahidi Wote kama palikuwa na Proper Paper Trade..

Mtobesya: Lakini tofauti na Kilicho zungumzia hapa ni kwamba hajasema Mara ya Mwisho aliona wapi Nyaraka Mpaka Leo anaitoa hapa Mahakama, Wenzangu pia walitupitisha Kwenye Kesi Ya CHARLES GAZILABO..

Kwenye hiyo kesi walirejea Kwenye hiyo Hapo sasa ni Submission yetu kwamba Knowledge ni suala la Msingi lakini Kwenye Kesi hii ni Tofauti..

Hii ya GAZILABO Unakubalina na Mimi Kwamba Kwenye Kesi hii Shahidi alikuwa na Knowledge, Mpaka Kwenye hukumu Majaji wanasema Shahidi Yule hakuitambua Mpaka Unique Features

Mtobesya: Sasa Shahidi hajafanya Chochote Kwenye suala la ENTRY na Kwamba kama Tunakubaliana na Kanuni za GAZILABO, lakini tunatofautisha Mazingira ya GAZILABO na Mazingira haya..

Nimalizie kwenye Wasilisho la kaka yangu Wakili wa Serikali Pius Hilla, Kwamba Shahidi alifanya Kazi Nyaraka ambayo ilikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam..Hakuna Kinachoifanya hiyo Nyaraka Ifanye iwe ya pekee

Na sisi hatukatai kwamba Kuna Kituo kikuu cha Polisi Kati Dar es Salaam, Lakini Hakuna Lolote Kwenye Nyaraka Kinachoifanya ionekane ni Nyaraka ya pale Central

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji sisi tunahitimisha Kwamba Kanuni ni zile zile zinatumika iwe Kwa Utambuzi au Kielelezo, Kanuni zipo wazi Kabisa, Na sisi tunasisitiza kabisa kwamba Nyaraka hii ISIPOKELEWE..

Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji..

Mtobesya anaketi, lakini anasimama Wakili Paul Kaunda na anasema anayo mengine ya kuongeza katika hilo.. Lakini anachapa Kiingereza kitupu.. Shughuli ni pevu...

Kaunda: Mheshimiwa Jaji Nianze Kwa Kurejea Provision na Jurisprudence ya Kumbukumbu za Mahakama, Kwamba Muda Sahihi wa Kupinga Nyaraka inayowasilishwa Kwa Maombi iwe Kwa Utambuzi au Kielelezo ni pale Inapotolewa tu..

Na siyo wakati wa Cross examination na Siyo wakati Wa Re examination, nasema hivyo kwa sababu zifuatazo..

Kaunda: Shahidi aliyepo Kizimbani hajaiambia Mahakama Kwamba Nini Kilitokea Kuanzia tarehe 07 August 2020 Mpaka sasa Kuhusiana na D.R...Na hiyo ndiyo Kanuni Kuu ya Chain of Custody Juu ya Nyaraka, Alipaswa Asiache Ombwe..

Kwenye Kesi Ya SHARIF ilisema Kwamba Kushindwa Kufanya hivyo Chain Of Custody inakataaa.. Mheshimiwa Kwenye Kesi hiyo hiyo Ukurasa wa Nane Paragraph ya pili, Mheshimiwa Jaji Masati wakati huo na mnukuu ifuatavyo..

Kaunda Anasoma.....

KAUNDA: Na hii Ndiyo Hoja yetu, na Hayo ndiyo ajayasema Bw. JUMANNE, Na Hoja ya kusema tusubiri Mpaka Mwisho wa trial Ndiyo Mahakama ndiyo iangalie Siyo Sahihi, Inapaswa Ingaliwe tangu 07 August 2020 Mpaka Leo Nyaraka Ilikuwa wapi.. Kwakifupi Mahakama Isifanye kinyume na hayo...

KAUNDA: Mheshimiwa Jaji mwaka Jana mwezi september MAHAKAMA iliandaa mwongozo,

MAWAKILI WA SERIKALI WAMENYANYUKA WOTE GHAFLA... Kama tupo CAMBODIA au BANGLADESH....

KAUNDA: Jaji Tuaiache hiyo, siyo New Fact, Ni Sheria tu nasoma...

Jaji: hawatopata Nafasi Kuzungumzia hiyo

Paul Kaunda: Sawa

Paul Kaunda: Ni Mahitaji ya % Msingi Katika Mahakama inapotoa Sifa za Ushahidi,

Jaji: unatuletea mambo Mapya

Paul Kaunda: Sawa Mheshimiwa Jaji, Mimi naomba Kuishia Hapo....

Fredrick Kihwelo: Wakili wa Serikali Pius Hilla amesema Kwamba Trial Within Trial ni sehemu ya Kesi hii,

Jaji: Umesikia hivyo?

Kihwelo: Ndiyo

Jaji: Hakusema hivyo, Nilisikia Anasema Trial Within Trial Ya Adam Kasekwa ni Sehemu ya Kesi ya Msingi, Wewe ishia alipoishia Kusema

Kihwelo: nilitaka Kusema Trial Within Trial Ya Adam Kasekwa Ni Vitu Viwili tofauti na Trial Within Trial Ya Mohammed Abdilah Ling'wenya.. Ndiyo Maana Wameomba tena Kuingiza Nyaraka

Jaji: Kwa hiyo Hoja yako Kama Kingekuwa ni Kitu Kimoja Wasingeomba Upya Kupokelewa Kwa Nyaraka

Fredrick Kihwelo: Ndiyo hivyo,

Kibatala: nimemsiliza Kwa makini Hoja zake Bw. PIUS Hilla lakini haja Jibu Hoja hata Moja..

Kwamba Nyaraka anayo iomba Kupokelewa Leo ipo Kwemye Exhibit Room kwa sababu ilitolewa Kwenye Shauri Lingine, na sijasikia akipinga hilo

Kibatala: Kwa hiyo ni Ghafla sana Tumekuta Nyaraka ya Ushahidi Imetoka Exhibit Room imejikuta ipo hapa mahakamani kwa Afisa wa Mahakama, Tunakubali kwamba Shauri Dogo ni sehemu ya shauri Mama, Lakini Leo Hatupo Katika Shauri Mama..

Kibatala: Ndiyo Maana Leo Shahidi PW1 ameapishwa na Leo amepewa Jina la PW1 wakati Shauri Mama ni PW8, Hairithi chochote na Shauri lililopita, Hajapinga kwamba Kuna Permission Rule Kwamba Kuna Sheria Iliyomruhusu Kwamba anaruhusiwa Kutoa Exhibit Store..

Kibatala: Kwa hiyo Kuna Mazoezi fulani ya kisheria walitakiwa kuyafanya yaweze Kuwapa Exhibit hapa Mahakamani, Pia hawajasema Kuhusu Ku' lay Foundation Kesi hii inahusiana Vipi na Kesi ya Adam Kasekwa.. Siyo Jukumu La Mahakama Kutoa Kielelezo Kwenye Kaunta Kwenda Kwa Shahidi,

labda Iwe Kwamba Ilishapokelewa, Wenzangu wanasema Sijaonyesha Procedural Violation, Sasa Kama sijafanya hivyo nilicho fanya hapa ni nini???? Wakati Mahakama Inafanya Uamuzi wake, Je Kielelezo kilichotumika kwenye kesi ya Adamoo Kingeruhusiwa tu Kuingia Kwenye kesi mama?

Kibatala: Jibu ni Hapana, lazima Yangekuja Maombi Rasmi, Kwamba Siyo Jukumu la Mahakama, Hapo Hoja Shahidi haijamfikia Makusudi,

KIBATALA: Jambo la pili Ni kwamba Wenzetu hawa wanacheza na vichaka kuhusu kesi ya Jana, Ndiyo Maana wanasema "Hawajasema Hawajasema".... They are very Clever Nawasifu kwa hilo... Ila wajue Kwamba Mahakama Kuvuruga Taratibu za Kisheria tu Ndiyo Madhara yenyewe...

Kibatala: BUNGE limetunga Sheria halafu Mahakama ikakiuka kwa umma hayo tu ni Madhara Kwa kuwa Mkataba wa Wananchi Kupitia BUNGE Umekiukwa... Na hiyo ndiyo Adversarial System..

Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji....

Jaji: Jaji Nimesikia Hoja zenu Kama namna ambavyo mmeziwasilisha na Nitahitaji Muda wa Kuzipitia.. Itanibidi Kuhairisha ili niweze kupitia na Kesho nifanye Maamuzi.. Kwa Namna ambayo Mmewasalisha kwa muda Mrefu na Mimi Nitahitaji Muda Mrefu Kupitia na Kutoa Maamuzi yangu..

Jaji: Kwa hiyo tukutane Kesho Saa 5 Asubuhi, Basi nahairisha shauri hili mpaka Kesho saa 5, SHAHIDI UTAPASWA URUDI, ILI UAMUZI UKIISOMWA UWEZE KUENDELEA USHAHIDI WAKO, Muwe na Jioni Njema wote

Jaji anatoka

Adios Amigo brothers, tukutane kesho tuendelee, ingawa tunayajua maamuzi
FD1RKdzWYAMhMP-.jpg

Wakili Msomi Paul Kaunda.. Wakili wa CHADEMA kanda ya Serengeti yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara....
zz3.jpg
zz2.jpg
zz1.jpg
zz.jpg


Mapichapicha kutoka mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Ubungo-Mawasiliano, DSM....
 
Nilishituka kidogo na kujiuliza kukikoni leo kina Erythrocyte Nyendo Replica au Roving Journalist kutotuandalia LIVE UPDATES ya kinachoendelea mahakamani...?

Ndipo nikakumbuka kuwa, muda wa mahakama waliokubaliana ni jana ni saa 5asb na siyo saa 3asb km siku zote tulizizoea....

Asante, tunasubiria kwa hamu hizo updates ili kujua huyu Afande Jumanne Malangahe atauteteaje uongo wake kwa namna atakavyopangua kwa hoja maswali ya mtego ya upande wa utetezi...
 
View attachment 2005439

Baada ya Mawakili wa Utetezi kuweka pingamizi kuhusu ushahidi wa Afande Jumanne , ikakubaliwa kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ili kupata majibu halali ya kisheria kutokana utata uliopo .

Kesi hiyo inaendelea leo Mahakamani hapo
Sasa naamini Jaji anamapungufu mengi katika kuweza kuamua yaliyo wazi. Siamini kama ni Jaji wa mahakama kuu huyu.
 
Siasa za visasi nchi hii vilianza rasmi 2016 wakati wa kumtafuta mrithi wa JK, Vita ikawa kubwa ndani ya CCM, uadui ukawa mkubwa kati ya kambi na kambi. Baada ya CCM kumpa urais waliyempa hali ikawa ni mbaya zaidi, uhasama ukahama toka makundi ya CCM na kurudi kwa raia wote - aliyempiga rais hata kwa mambo ya msingi alikipata anashostahili, vyama vya siasa navyo nikazuiwa kufanya siasa nchini hadi leo wanafanya katika mazingira magumu mno.

Hadi leo kinachoendelea kwa Mh. Mbowe ni mwendelezo wa siasa za chuki na kukomoana. Sina uhakika kama nchi yetu itarudi kwenye upendo na kuheshimiana uliokuwapo tangu enzi zile za mwalimu mpaka hadi 2015 upendo ulipokoma rasmi.
 
View attachment 2005439

Baada ya Mawakili wa Utetezi kuweka pingamizi kuhusu ushahidi wa Afande Jumanne , ikakubaliwa kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ili kupata majibu halali ya kisheria kutokana utata uliopo .

Kesi hiyo inaendelea leo Mahakamani hapo
Pot...nakuamina sana....katika historia kuna kipengele wazungu wanasema "kule kwenu ilikua ngumu kutawala mkoloni....mana ukitafakari mipaka yenu ni milima mirefu mashark,kaskazn na magharibi....chini unaikuta nyanjaa kubwa...mkoloni ilikua mbinde kuweka himaya yake...nakuona ukiwakilisha vyema kupambana na ukoloni wa mtu mweusi ...Erythrocyte the Great!!
 
Akidi yetu nayo inaingia kijiditali kufuatilia mwenendo wa kesi ndogo (Trial within a trial).
KESI ndogo ndani ya kesi ya msingi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, imeanza kusikilizwa, Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu, Mawasiliano jijini Dar es Salaam. Kesi hiyo ndogo imeanza kusikilizwa mahakamani hapo mbele ya Jaji Joackim Tiganga, leo Jumatano, tarehe 10 Novemba 2021. Kesi hiyo inatokana na mapingamizi ya upande wa utetezi dhidi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling'wenya, wakiiomba mahakama hiyo isiyapokee kwa madai kuwa si halali
N.B
The concept of trial within a trial :

https://www.academia.edu › THE_C...
the concept of trial within trial - Academia.edu

4.2. In order to establish the allegation of involuntariness of a confession, the main trial is...

1636534395314.png
 
Back
Top Bottom