Misa ya marehemu imemalizika mchana huu, pale St. Alban ikafuatiwa na heshima za mwisho.
Watu ni wengi wamejitokeza wakiwemo waheshimiwa Membe, Tibaijuka, Ole Medeye, Nyalandu, Mzee Mengi, Rugumyamheto, Paul Rupia, Mzee Kassanga, etc, etc.
Kwa wale wazoefu wa waumini wa St.Alban, wanaushirikiano mkubwa sana miongoni mwao wakati wa shida na raha, na inapotokea shida kama msiba, huwa haijalishi msiba ni wa mtu wa status gani, siku zote hujitokeza kwa wingi.
Binafsi nimepata fursa ya kukutana na lots of good old friends tuliosoma nao Tambaza ya zile, akiwemo jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina maaruf la 'Chief'.
Msafara ukiongozwa na piki piki ya Traffic, umeleta usumbufu mkubwa kwa magari kusimamishwa kwa muda mrefu kuruhusu msafara kupiota. Sasa wameelekea kambi ya jeshi ya Lugalo kwa heshima za kijeshi, kabla ya safari ya kuelekea shambani kwake Mapinga kwa mazishi.