Breaking Newz: Kizaza habari maelezo watimuliwa!

Inabidi apite ofisi zote ili kuhakikisha wote wanaodaiwa wamelipa au wanafukuzwa.
 
majuzi kawashikisha adabu wizara ya Bwana Nchimbi.

Ingawa alivyopewa hiyo post watu walimsema kuwa 'kabebwa', utendaji wake ni wa kupigiwa mfano kuzidi hata 'wasiobebwa'
 
sasa nimeamini ile kauli waliyosema kuwa hawatamwonea mtu awaye yeyote aibu. Big up
 
Kama hawalipi kodi atimue tu hamna cha serikali wala nini mbona wanahela ya kulipa Dowans lakini deni la ofisi inashindikana
 
aibu kubwa sana lakini ngoja tuone nini kitaibuka j3
 
asiishie huko tu,apite pite na kwenye taasisi nyingine za serikali..
 
Nimependa sana kauli ya mkuu wa oparesheni hiyo! "Yeyote anaeona anadaiwa akalipe deni mapema"
 
Hizi Wizara/Idara zenye maofisi kwenye majengo ya NHC si huwa zina bajeti ya pango kila mwaka kutokana na kodi zetu, kwa nini hawalipii? Ni sawasawa tu kutolewa nje, walitaka wakae bila kulipa ili iweje?!

Ni haki yao kutimuliwa tukizingatia kuwa HAKI ni malipo/marejesho anayostahili mtu kulingana jambo alilolitenda (hawakulipa kodi ya pango, wanahaki ya kutimuliwa)
 
Ni mzuri sana, wanafata maagizo ya JMK kawaambia hakuna kuwachiwa mtu na msilielie hamna fedha wakati mna rasilmali majumba (yakudhulumu) nchi nzima na hao mawizara na idara za Serikali si wana bajeti na wanapewa fedha zinakwenda wapi? nawapa miezi sita nione mabadiliko na nione mna pesa za kutosha NHC la sivyo mtakuja kujieleza.

Ahsante JMK. Hivyo ndivyo inavyotakiwa sio kuanza kuandikisha watu sijui wewe kabila gani, unakula chakula gani, una asili gani, wanao wanasoma shule gani...

Hayo yanatokea baada ya JMK kuwaita Ikulu na kuwauliza kulikoni? Mbona Mzee Sabodo analalamika, walipojitafuna tafuna ndio akaanza kuwapa mipasho, amma wajipange kiukweli amma wanakwenda na maji. Wamemuudhi JMK kwa fomu lao la kibaguzi, tena kama ni mimi kwa ile fomu saa hizi hawana kazi. Wamemkuta mtu mwenyewe ana huruma kupita kiasi.
 
Wadaiwa sugu wa madeni ya kodi ya NHC. Wanastahili kutolewa. Kumbe jeuri yote hiyo ya kufungia magazeti huku hawalipi kodi? Aibu! Kweli, mficha maradhi kifo humuumbua!
 
bora wewe mpotevu umeweka wazi,,,,nadhan ni ubishi tu ila habari INAELEWEKA

Siyo kwamba ubishi, wengine wanaelewa ila tu wanamchukia Mchechu ambaye ameingia NHC mwaka jana kwa sifa ya utendaji bora, ndiyo ameanza sasa kuonesha kazi na bado!!! Ataingia hata kwa hao wanaopangisha nyumba za NHC wa wahindi na wao kukaa chanika
 
mimi naona ni sawa kabisa kufanya hivyo mbona sisi tunapokosa pesa ya pango tunafukuzwa iweze leo leo wao tuwaonee huruma?
acha wakome
 
Back
Top Bottom