Deodatus "sheria Mpya Kuruhusu Mwandishi Wa habari kumshitaki Mtoa Taarifa

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema, sehemu ya sheria ya sasa inaruhusu mwandishi wa habari kumshitaki mtoa taarifa endapo atakataa kutoa taarifa inayotakiwa na mwanahabari.

Balile ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, alipozumgumza na baadhi ya wanahabari katika ofisi za jukwaa hilo, jijini Dar es Salaam.

Pia Balile amemshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kuingilia kati katika maeneo ambayo maofisa wa serikali walipotaka kunyanyasa wanahabari.

“Kuna maofisa wa serikali walitaka kuendeleza utamaduni wa kunyanyasa wanahabari. Jambo hili limekuwa likiwatesa wengi, lakini nimshukuru Msigwa maana amekuwa makini katika hili,” alisema Balile.

Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema, baada ya bunge kupitisha marekebisho ya sheria ya habari, kinachofuata sasa ni kuomba fursa ya kukutana na serikali kwaajili ya kupendekeza mambo gani yaingie kwenye kanuni.

Miongoni mwa mambo ambayo wadau wa habari wangependa kuona yanaingia kwenye kanuni mpya na kuanza kutumika ni pamoja na suala la leseni ya magazeti kuwa zaidi ya miaka mitano tofauti na ilivyo sasa.

“Tutashauri serikali kwamba, kanuni zetu zielekeza kuwa lesini pamoja na kitambulisho cha mwanahabari (press card), zidumu kwa zaidi ya miaka mitano, pamoja na makosa ya kitaaluma yanapaswa kubaki kwa wanataaluma wenyewe, hili litasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani” amesema Balile

Kwenye mkutano huo pia Balile amesema, eneo lingine wanalotarajia liingie kwenye kanuni, ni umiliki wa hisa katika vyombo vya habari kutowekewa mipaka.

"Sheria inataka mwekezaji kutoka nje ya nchi amiliki hisa isiyozidi asilimia 49, jambo hili linapunguza uwekezaji kwenye vyombo vya habari.

“Tutamshauri Waziri Nape kwamba, mwekezaji kwenye vyombo vya habari asiwe na ukomo kama ilivyo kwenye mitandao ya simu na maeneo mengine.”

Source: Azam Tv
 
Kumshtaki kivipi yaani?
Sijaelewa hapo naombeni mnieleweshe.
Nahisi Kama Mtoa Taarifa Akimpatia Mwandishi Wa Habari Taarifa Ambazo Sio Za Kwel


na Taarifa Hizo Zikasababisha Matatizo Katika Taaluma Yake kama Sedition And Defamation Anaweza Fungua Shitaka Mahakamani ....
Ama Kutoa Fake News Kwa Mtu Habari Na Habari Hizo Zikawa Za Kuogofya Katika Jamiii Na Kuleta Chuki Ama Mvurugano.....
 
Nahisi Kama Mtoa Taarifa Akimpatia Mwandishi Wa Habari Taarifa Ambazo Sio Za Kwel


na Taarifa Hizo Zikasababisha Matatizo Katika Taaluma Yake kama Sedition And Defamation Anaweza Fungua Shitaka Mahakamani ....
Ama Kutoa Fake News Kwa Mtu Habari Na Habari Hizo Zikawa Za Kuogofya Katika Jamiii Na Kuleta Chuki Ama Mvurugano.....
Anhaaa.....
Na wao wakireport uongo ni vivo hivyo sio?
 
Back
Top Bottom