NACTVET: Malalamiko kuhusu vyeti yanatakiwa kuwasilishwa kwetu kwa maandishi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Baada ya malalamiko kutolewe na member kwenye Jukwaa la Habari na Hoja ndani ya JamiiForums.com kuhusu Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kuwazungusha baadhi ya watu ambao wanafanya mabadiliko ya taarifa za vyeti vyao vya elimu, mamlaka husika imetoa maelezo.

Malalamiko ya memba wa JamiiForums.com ~ Nimelipia marekebisho ya cheti cha Chuo, huu ni mwezi wa nne sasa, NACTVET wananizungusha tu

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano waa NACTVET, Jeff Shellembi amesema kwa kawaida vitu kama hivyo (malalamiko) vikaletwa kwetu kwa maandishi ili changamoto zijulikane na kuwe na mifano hai.

Kama kuna chochote lazima taasisi iandikiwe kisha kuwe na utaratibu wa majibu, Serikali tunafanya kazi kwa makaratasi ili anapokuja mtu wingine inakuwa rahisi kukabidhiwa na kujua nini hasa kimefanyika.

Sisi huwa tunashughulika na namba ya mtu na sio jina lake, hivyo kama kuna mtu anahitaji kufahamu kuhusu changamoto au kitu fulani.

Kuna kesi nyingi tunaoshughulika nazo ambazo zinatatuliwa kupitia info@nacte.go.tz kuna mtu ambaye na majukumu ya kujibu malalamiko mengi kwa njia hiyo.
 
Angeongezea tu zile kauli zao za shibe kuwa "hatushughuliki na kelele za mitandaoni"
 
Back
Top Bottom