Breaking news;MAGUFULI AKAMATA NETI ZA BUSH BWAWA LA MUNGU

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Kama waziri aliekunywa maji ya bendera ya chama nahisi huyu alikunywa zaidi
mhe waziri wa uvuvi BW magufuli amekamata watu;polisi;wakuu wa kata;serikali za mitaa pamoja na neti zile zilizotolewa na RAIS JOJI bush wakati alipokuja kwa ajili ya wanaoumwa malaria habari zaidi zinasema waziri amehuzunika sana baada ya kuona hata wakuu wa polisi wa mwanga wanashiriki kwenye uhalifu wa kuwalinda wale wanaovua samaki kinyume cha sheria...katika kuonyesha hili yuko makini jamaa aliomba zote ziliozkamatw ziwashwe moto mbele yake...na hapo ndipo wananchi walipojaa n akushindwa kuamini kinachotokea...
kazi kweli kweli;hongera MAGUFULI;hivi hawa mawaziri wengine HAWAKO KAZINI???
 
Hizo net za kuzuia malaria au za kuvua samaki?

Basi kama ni neti za kuzuia mbu zinatumika kuvulia samaki hao wavuvi watakuwa na akili!
 
neti zile zilizotolewa na RAIS JOJI bush wakati alipokuja kwa ajili ya wanaoumwa malaria habari zaidi

Basi kama ni neti za kuzuia mbu zinatumika kuvulia samaki hao wavuvi watakuwa na akili!

kabisa??
 
neti zile zilizotolewa na RAIS JOJI bush wakati alipokuja kwa ajili ya wanaoumwa malaria habari zaidi

Basi kama ni neti za kuzuia mbu zinatumika kuvulia samaki hao wavuvi watakuwa na akili!

kabisa??

Hawana kabisaaaa. Na wanapoteza maana ya kupewa misaada ya kuokoa maisha yao na gonjwa la malaria. Hawa wananchi wanapaswa kupewa darasa la umuhimu wa afya zao na madhara ya utumia wa aina hii ya mitege. Manake wanaangamiza hata mazalia ya samaki kwa kutumia aina hii ya zana.
 
... habari zaidi zinasema waziri amehuzunika sana baada ya kuona hata wakuu wa polisi wa mwanga wanashiriki kwenye uhalifu wa kuwalinda wale wanaovua samaki kinyume cha sheria...

Mnatuambia waziri kasema tatizo ni kuvua samaki kwa njia zisizotakiwa au ni wizi wa vyandarua vya Bush?

Habari za ki-bongo haziko coherent, hazieleweki. We are uninformed masses. Maelezo shagalabagala.
 
Hata mimi sijaelewa kinachoendelea! Net za mbu zinatumika kuvulia au? Na kwanini zichomwe? Sio wazipeleke zikatumike ipasavyo?
 
Net za mbu zimetumika kuvulia samaki waziri anachokataza ni kutumia zana duni kama hizo ambazo kwa kawaida achilia mbali kuwapatia mahitaji kwa mda mfupi..zinaondoa uwezekano wa kuwa na samaki mbele ya safari..hii ikiwa na maana net unavua mpaka mayai ya samaki...hata wale ambao hukuwakusudia nao unawachukua...ukisha wafikisha nchi kavu wamekufa....huna cha kuwafanya..anachosema watu watumie zana nzuri wavue samaki wakubwa wakubwa sio mpaka vitoto vya samaki...ambavyo ndio vinakuwa.Sasa ukiwavua na hao kesho utavua nini?Ila huyu jamaa anafanya kazi balaa...angekuwa waziri mkuu sijui ingekuwaje
 
Na kwanini zichomwe?

Ni kwamba Waziri kaamuru vidhibiti vya wizi wa vyandarua vichomwe? Haiwezekani ha hahahahaha...you can't make that up, its so incredible. Destruction of evidence. Sometimes huwa najidhani mimi ndio slow sielewi. Lakini hapana, something is gotta be fishy with this info here, I am telling you, we are a misinformed bunch.

Vyandarua vya Bush, sheria za uvuvi haramu, Waziri kaamua wachome....I'm like whoa whoa whoa...slow your role, will ya'? Say who what?
 
Sio vyandarua kuibiwa, ni kwa sababu vyandarua vimetumika katika uvuvi. Uvuvi haramu. Kutumia vyandarua kuvua ni uvuvi haramu kwa sababu vinaharibu recruitment sites za viumbe wa majini.
 
Jamani wanannchi hawa ni maskini hawana njia nyingine ya kuongeza kipato ili waweze kupata walau milo mitatu kwa siku. Sasa net hizo ndizo wameamua kuzitumia kuvulia samaki heri wafe kwa malaria kuliko njaa. Nadhani ni fundisho kwa serikali wananchi hawawezi lala ndani ya net wakiwa na njaa...cha muhimu ingebidi wawezeshwe kwanza na net zifuate...
 
Watu wengine wanajifanya hawaelewi kiswahili sababu tu eti wako majuu. Kiswahili kitabaki kiswahili. Soma taarifa na uielewe usitafsiri ili uielewe.
 
Jamani wanannchi hawa ni maskini hawana njia nyingine ya kuongeza kipato ili waweze kupata walau milo mitatu kwa siku. Sasa net hizo ndizo wameamua kuzitumia kuvulia samaki heri wafe kwa malaria kuliko njaa. Nadhani ni fundisho kwa serikali wananchi hawawezi lala ndani ya net wakiwa na njaa...cha muhimu ingebidi wawezeshwe kwanza na net zifuate...

Wavue kwa hizo net, waue mayai na kuvua juvenile fish, kusiwe na recruitment. Mwisho wa siku hakuna samaki kabisa, watakula hizo net badala ya kutumia kuzuia mbu kudadadadadeki!

Watanzania hawapendi kusikiliza wataalam, wahusudisha short cuts na hawana longtime planning walai tena. No wonder mafisadi baadhi wanatetewa na watanzania hao hao wanaojiita wapiga vita ufisadi.
 
Net za mbu zimetumika kuvulia samaki waziri anachokataza ni kutumia zana duni kama hizo ambazo kwa kawaida achilia mbali kuwapatia mahitaji kwa mda mfupi..zinaondoa uwezekano wa kuwa na samaki mbele ya safari..hii ikiwa na maana net unavua mpaka mayai ya samaki...hata wale ambao hukuwakusudia nao unawachukua...ukisha wafikisha nchi kavu wamekufa....huna cha kuwafanya..anachosema watu watumie zana nzuri wavue samaki wakubwa wakubwa sio mpaka vitoto vya samaki...ambavyo ndio vinakuwa.Sasa ukiwavua na hao kesho utavua nini?Ila huyu jamaa anafanya kazi balaa...angekuwa waziri mkuu sijui ingekuwaje

Sio vyandarua kuibiwa, ni kwa sababu vyandarua vimetumika katika uvuvi. Uvuvi haramu. Kutumia vyandarua kuvua ni uvuvi haramu kwa sababu vinaharibu recruitment sites za viumbe wa majini.

Okay then, kama hivyo ndivyo, sasa elezeni habari ya wizi wa vyandarua vya Bush inahusiana vipi hapa?

Maana nyinyi mme ignore baadhi ya aliyoyasema mleta habari, mimi nimetilia maanani kila kitu. Kwamba kuna ufisadi wa vyandarua vya Bush, wizi, na Waziri akachoma moto vidhibiti. Nyinyi wenzangu mna jinsi ya kuelewana ambayo mtu ka mimi ukijifanya kuzingatia, kusikiliza kwa makini, kila kilichosemwa unakuwa huelewi?

Ni kwa nini Waziri amechoma moto vidhibiti vya vyandarua vya misaada vilivyoibiwa? Mjibieni MwanaHALISI.
 
Okay then, kama hivyo ndivyo, sasa elezeni habari ya wizi wa vyandarua vya Bush inahusiana vipi hapa?

Maana nyinyi mme ignore baadhi ya aliyoyasema mleta habari, mimi nimetilia maanani kila kitu. Kwamba kuna ufisadi wa vyandarua vya Bush, wizi, na Waziri akachoma moto vidhibiTI. Nyinyi wenzangu mna jinsi ya kuelewana ambayo mtu ka mimi ukijifanya kuzingatia, kusikiliza kwa makini, kila kilichosemwa unakuwa huelewi?

Ni kwa nini Waziri amechoma moto vidhibiti vya vyandarua vya misaada vilivyoibiwa? Mjibieni MwanaHALISI.

Ni hivi, wavuvi wote wanaotumiwa zana haramu kuvua, zana hizo zikikamatwa dawa yake ni kuchomwa moto. Kwa sababu gani basi, iligundulika kuwa hivyo vidhibiti baadae vilikuwa vinarudi kuendeleza libeneke la uvuvi haramu.

Hebu fikiria, ndugu Dilunga, hebu fikiria polisi wenyewe wanahusika na uvuvi wa kutumia vyandarua, akikamatwa polisi, kesi itaishia juu kwa juu, na vithibiti vile vitarudi ziwani kama kawa kuendeleza libeneke la uvuvi haramu. Inasikitisha sana. Wananchi wanaona, ukikutwa na kokoro, inachomwa moto, ukikutwa na baruti...sijui inakuwaje.

Kuhusu la wizi wa vyandarua, hiyo ni kesi nyingine, kwa sababu hakuna anayejua kwamba vimeibiwa. Pengine hao wavuvi waligawiaa vyandarua vya bure, huko kliniki wake zao walipewa bure walipokuwa wajawazito, au watoto wao walio chini ya miaka mitano walipewa vyandarua hivyo bure. Hivyo kuvipata na kuvitumia katika uvuvi sio lazima wawe wameviiba, wanaweza kuwa wamevichukua toka majumbani mwao. Hapo hakuna kesi ya wizi. Kuna kesi ya uvuvi haramu. Ambayo sijui kama ipo kwa sababu, sidhani kama wanapelekwa mahakamani. Nahisi ndio maana waziri akaamuru vichomwe.
 
Ni hivi, wavuvi wote wanaotumiwa zana haramu kuvua, zana hizo zikikamatwa dawa yake ni kuchomwa moto. Kwa sababu gani basi, iligundulika kuwa hivyo vidhibiti baadae vilikuwa vinarudi kuendeleza libeneke la uvuvi haramu.

Hebu fikiria, ndugu Dilunga, hebu fikiria polisi wenyewe wanahusika na uvuvi wa kutumia vyandarua, akikamatwa polisi, kesi itaishia juu kwa juu, na vithibiti vile vitarudi ziwani kama kawa kuendeleza libeneke la uvuvi haramu. Inasikitisha sana. Wananchi wanaona, ukikutwa na kokoro, inachomwa moto, ukikutwa na baruti...sijui inakuwaje.

Hujajibu.

Ufisadi wa vyandarua vya Bush unahusianaje hapa?
 
Kuhusu la wizi wa vyandarua, hiyo ni kesi nyingine, kwa sababu hakuna anayejua kwamba vimeibiwa. Pengine hao wavuvi waligaia vyandarua vya bure, wake zao walipewa bure walipokuwa wajawazito, watoto wao walio chini ya miaka mitano walipewa vyandarua hivyo bure. Hivyo kuvipata na kuvitumia katika uvuvi sio lazima wawe wameviiba, wanaweza kuwa wamevichukua toka majumbani mwao. Hapo hakuna kesi ya wizi. Kuna kesi ya uvuvi haramu. Ambayo sijui kama ipo kwa sababu, sidhani kama wanapelekwa mahakamani. Nahisi ndio maana waziri akaamuru vichomwe.

Okay.

MwanaHALISI kajuaje vyandarua ni vile vya Bush?
 
Mimi na wewe tumesoma hii habari hapa. Ukiniuliza amejuaje unanionea. Sikuwa na mwanahalisi. Labda tumuulize Kubenea.

Kwa hiyo hata wewe hukuelewa, au? Sasa mbona ulikuwa mstari wa mbele kueleza kilichosemwa?

Lazima unajua, maana hata unafahamu kwamba mleta mada ni Kubenea. Umelikorogwa, sasa utalinywa: Dimension ya vyandarua vya Bush imekujaje hapa?
 
Jamani wanannchi hawa ni maskini hawana njia nyingine ya kuongeza kipato ili waweze kupata walau milo mitatu kwa siku. Sasa net hizo ndizo wameamua kuzitumia kuvulia samaki heri wafe kwa malaria kuliko njaa. Nadhani ni fundisho kwa serikali wananchi hawawezi lala ndani ya net wakiwa na njaa...cha muhimu ingebidi wawezeshwe kwanza na net zifuate...

...dah, :D ha ha haaaa....haki ya mungu! safari ni ndefu, acha tu! kheeeee :eek: !!!
 
Kwa hiyo hata wewe hukuelewa, au? Sasa mbona ulikuwa mstari wa mbele kueleza kilichosemwa?

Lazima unajua, maana hata unafahamu kwamba mleta mada ni Kubenea. Umelikorogwa, sasa utalinywa: Dimension ya vyandarua vya Bush imekujaje hapa?

Mukulu, issue ya BUSH muulize Kubenea, sio lazima nijue kila kitu dunia hii. Issue ya uvuvi naijua, napiga vita wanaovua kwa kutumia vyandarua, viwe vya BUSH au vya A to Z.

Juu ya hilo, mtake radhi mheshimiwa Magufuli kwa kumfanya mbu mbu mbu wa sheria, kumwona zoba wa sheria, anayeidhinishakuchoma vithibiti vya kesi. Ulijuaje kama hapo kuna kesi kama sio kuzua?
 
Back
Top Bottom