Breaking neeeeewz

Mi nilitaraji kuwa mitihani ya kidacho cha sita ingefanyika november ili matokeo yao yatoke february na wajiunge na vyuo august. cha kushangaza wanaturudisha may! au ndo mpango wa kuwapeleka JKT vijana kwa lazima unaivishwa?
 
Aiseee baba yangu hapo hakuna kitu wanapoka rangi nyumba ya matope

mi nakula mbege 2
 
Katiba ijayo inabidi tuichangie kwa makini sana ,miaka 50 ya utawala binafsi bado hatujaweza kuwa na mfumo mzuri kwa jambo lolote lile,inasikitisha sana,yani kila anayeingia anafanya lake.Natumaini kungekuwa na katiba nzuri na iliokamilika kusingewezekana kufanya jambo kama hilina tungekuwa na uwezo wa kuhoji .Katika kuingia katika uchaguzi mkuu 2015 inabidi kuchagua wabunge imara na makini bila kuangalia itikadi za vyama na wanatakiwa wafanyiwe mdahalo mapema ili kujua kilaza ni yupi na niyupi anatufaa na si tukubaki tuu wakimbie mdahalo. Na waliopo bungeni tumewaona na tumesikia michango yao yenye nafaka na iliyokuwa na pumbu,kama tukiendeleza uswahiba kujuana na uchama hatutofika hata kidogo,hasa sisi vijana inatubidi kuangalia mbele wale wazee walisha vuna hawana tena michango kwa taifa na wapo kwa maslai yao binafsi tuu sisi ndiyo wenye miaka takribani 60 mbele yetu na zaidi.Tujitafaka tuchukue hatua.Kuna msemo usemao mzee kufa ni lazima ila kijana inawezekana kufa
 
ipo siku watakuja na muunganiko wa physics na history kitu kitaitwa PHYS-HISTORY mark my words hii nchi kila siku wanakuja na yao...
 
nchi inalewalewa kama machela.elimu ilshakuwa kitu cha kujaribiwa kila mara mitahala na mihura inabadilishwa
 
MARK TIME game!

Ndugu mwananchi kinachofanyika hapa ni kuchelewesha jeshi kubwa la vijana (MZIGO) kuhitimu shule ili kujaribu kubana mahitaji makubwa (pressure) ya MIKOPO na nafasi huko vyuoni.

Ukiwa kipofu unaweza fikiri wataalam wa Wizara/Serikali hawako makini kwa kubadilibadili mambo kila mara, lakini NYUMA YA PAZIA watu wanajua wanachofanya. Huu ni mkakati 'wa kijanja zaidi' wa kufidia mapengo ya bajeti mwaka hadi mwaka - kwa gharama ya walewale waliolala. Keep on sleeping.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Tatizo ni kuwa, sera ya Elimu Tz inaendeshwa kisiasa zaidi so maamuzi yake yanafanyika kwa kutumia mioyo badala ya kutumia vichwa!!!!
 
Mbona hujaweka chanzo unasema breaking newz afu huandiki yametamkwa na nani na wapi au unadhani wote wana hiyo breaking newz yako! Andika habari nzima ili ieleweke.
 
watanzania kulalama mtaacha lini! what matters ni siku za kukaa darasani, haijalishi mtihani unafanya Januari au Agosti,
 
Hi ndio Tz.Mwaka 2005 wakafuta masomo ya biashara (book-keeping na comerce) yakarudishwa tena 2006.
hii ndo tz(kichwa cha mwandawazimu>benjamin w mkapa) xo m2 akija on power anafanya anavyotaka akimaliza mda wake ndo tunaona madudu,kama hapo awal hakukuwa na wasomi
 
Elimu ya Tanzania iliporomishwa mwaka 1967 tulipoamuwa kuwachana na mfumo uliowekwa na Waingereza. Kwa miaka 38 baada ya hapo tukajitahidi kufanya kila njia kuigaragaza elimu kwa wengi na kuwasomesha wachache ambao tulidhani wangeifanya kuwa hii nchi ni pepo ya dunia. Kwa bahati mbaya kabisa hao wachache waliosomeshwaa kwa makusudi kabisa, wakawa ndio kuni za kuiteketeza hii nchi katika kila nyanja, kuanzia elimu, afya, uchumi, utalii mpaka utu na jamii.

Leo miaka 7 ya Kikwete tunaona mabadiliko makubwa sana, tunaona vyuo vikuu vikijengwa kwa idadi ya zaidi ya kimoja kila mwaka toka aingie madarakani, tumeona shule za sekondari zaidi ya 4000 zikijengwa wakati wake, tumeona kuwa kuna baadhi ya shule wameruhusiwa wafate mfumo wa Kiingereza na kwa sasa unatambulika tena rasmi.

Tunaona jitihada na bajeti ya wizara ya elimu ikipanda kila mwaka. Ni mwanzo mzuri baadaa kusambaratishwa na kutuacha kuwa nchi ya mwisho kielimu kulingana na jirani zetu kama Kenya na Uganda.

Tunamtakia kila la kheri Kikwete airudishe mitaala na iwe bora kuliko ilivyokuwa wakati tunapata Uhuru.

Wengi tulioiwahi elimu na mitaala ya mkoloni tunasikitishwa sana tukiona elimu ilipopelekwa pabaya, sijui nani alitudanganya kuwa tunaweza kuleta maendeleao bila kuwekeza kwenye elimu kwa nguvu zaidi? Nakumbuka shule yangu ya awali Kisarawe, tulikuwa na kila cha kujivunia kama shule na nakumbuka shule yangu ya pili H. H. The Agakhan Secondary School ambayo baadae ikaja kuitwa Tambaza Secondary School.

Tulikuwa tuna maabara ambayo hata hospitali nyingi tu nyingine kwa sasa haina. Tulikuwa tuna Art room, ambayo ukiingia unajuwa nipo chumba cha ma artist. Tulikuwa tuna vifaa vya michezo ambavyo hata timu za Taifa kwa sasa hazina, tulikuwa, tulikuwa, tulikuwa, tulikuwa.

Roho inauma sana.
 
Elimu ya Tanzania iliporomishwa mwaka 1967 tulipoamuwa kuwachana na mfumo uliowekwa na Waingereza. Kwa miaka 38 baada ya hapo tukajitahidi kufanya kila njia kuigaragaza elimu kwa wengi na kuwasomesha wachache ambao tulidhani wangeifanya kuwa hii nchi ni pepo ya dunia. Kwa bahati mbaya kabisa hao wachache waliosomeshwaa kwa makusudi kabisa, wakawa ndio kuni za kuiteketeza hii nchi katika kila nyanja, kuanzia elimu, afya, uchumi, utalii mpaka utu na jamii.

Leo miaka 7 ya Kikwete tunaona mabadiliko makubwa sana, tunaona vyuo vikuu vikijengwa kwa idadi ya zaidi ya kimoja kila mwaka toka aingie madarakani, tumeona shule za sekondari zaidi ya 4000 zikijengwa wakati wake, tumeona kuwa kuna baadhi ya shule wameruhusiwa wafate mfumo wa Kiingereza na kwa sasa unatambulika tena rasmi.

Tunaona jitihada na bajeti ya wizara ya elimu ikipanda kila mwaka. Ni mwanzo mzuri baadaa kusambaratishwa na kutuacha kuwa nchi ya mwisho kielimu kulingana na jirani zetu kama Kenya na Uganda.
Tunamtakia kila la kheri Kikwete airudishe mitaala na iwe bora kuliko ilivyokuwa wakati tunapata Uhuru.
Wengi tulioiwahi elimu na mitaala ya mkoloni tunasikitishwa sana tukiona elimu ilipopelekwa pabaya, sijui nani alitudanganya kuwa tunaweza kuleta maendeleao bila kuwekeza kwenye elimu kwa nguvu zaidi? Nakumbuka shule yangu ya awali Kisarawe, tulikuwa na kila cha kujivunia kama shule na nakumbuka shule yangu ya pili H. H. The Agakhan Secondary School ambayo baadae ikaja kuitwa Tambaza Secondary School.
Tulikuwa tuna maabara ambayo hata hospitali nyingi tu nyingine kwa sasa haina. Tulikuwa tuna Art room, ambayo ukiingia unajuwa nipo chumba cha ma artist. Tulikuwa tuna vifaa vya michezo ambavyo hata timu za Taifa kwa sasa hazina,tulikuwa,tulikuwa,tulikuwa,tulikuwa.Rohoinaumasana.
una kazi maalum jf wewe, jk??
 
Back
Top Bottom