Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,503
- 113,616
Wanabodi,
Juzi usiku nikiwa bar fulani maarufu karibu na Mlimani City, jamaa aliniafuata mezani na kuniambia kuna mzigo wa I Phone 5 pieces 2, na I Phone 4s pieces 3 umeibwa Mlimani City!, na bado uko ndani ya box zake na hazijafunguliwa!. Unauzwa kwa bei poa!.
Uko wapi?, nikatolewa nje na kupelekwa kwenye gari fulani hapo nje, nikakuta hizo I phone 5 simu mbili na I Phone 4S simu tatu!, ndipo nikaonyeshwa hiyo I Phone 5!. Kwa masikini mimi siijui hata hiyo I Phone 5 ya ukweli, nikamuomba aifungue niione!. Jamaa kwanza akagoma kuwa kwa vile ni brand new, iko sealed kwenye box yake, akasema ili aifungue, lazima nionyeshe I'm serious buyer, asije kuifungua halafu nisinunue, mara akaifungua nikaishangalia!.
Bei ya kuanzia ni 1.5!, akanielekeza dukani pale kwa Mama Dubai ni 1.8, na maduka mengine ni mpaka 2.2!. Kiukweli kwa mwandishi wa habari wa bongo, 1.5 ni mshahara wa robo mwaka!. Nikamwambia asifungue maana huko sifiki hata nusu!. Akanishauri basi ninunue zile 4S na moja ilikuwa imefunguliwa!.
Akaniwashia nikaitest kwa bluetooth nikathibitisha its genuine!. Hiyo 4s akasema dukani inauzwa laki 8, yeye anataka laki 6 tuu!. Huko nako ni mbali sifiki, nikamshukuru nikarudi ndani kwenye kinywaji changu!. Jamaa akanirudia, na kuniuliza nina ngapi, maana jamaa ndio kwanza ametoka kukwapua, hivyo hana kitu na atakubali kwa bei yoyote!.
Tukakubaliana I phone 5 kwa laki 5!, sijui jamaa anatumia dawa!, mara nikaanza kujisachi nilichonacho, tena nina bahati, siku hiyo nimetoka kupiga deal heavy na TPDC mtambo wa gesi Kinyerezi, "libahasha lake linene" nimesha tumia tumia hapa na pale, na kuwarushia rushia kwa m-pesa akina ninii wote, sasa nilikuwa nimejikalia bar kujipongeza hivyo nilikuwa "loaded"!.
Nikajikung'uta kung'uta nilicho nacho haikufika laki 5!, nikamwambia twende kwenye ATM ya karibu nijazie!, jamaa akaonyesha ana haraka,akaniuliza kwani zimepatikana ngangapi, nikamwambia 380,000 jamaa akasema lete tuu hata hizo hizo, kwasabu yeye hakuingia gharama yoyote!, nikamlipa nikakabidhiwa I phone 5 yangu Brand New, "Original!" ndani ya box yake kwa 380,000 tuu!. Akaniambia kama nina pesa mahali, ile I phone 5 ya pili anaweza kuniuzia kwa laki 3 tuu na zile I phone 4s atanifanyia kwa laki mbili mbili!.
Duu!, nikaona hii ni big deal!.Kimoyo moyo nikaanza kufurahi na kujifariji kuwa inaweza mimi nikawa ndie mwandishi wa habari wa wa kwanza hapa bongo kumiliki I phone 5! (niliwahi kuwa mwandishi wa habari wa kwanza bongo kumiliki pikipiki!),
Kufika home, nikamweleza wife na kumwambia kesho namnunulia na yeye!, na watoto wetu watatu wakubwa (tunao 6), kesho tunawanunua zile 4s!. Kama tumeweza kuwanunulia I pod na games za PSP!, kwa nini tushindwe kuwanunulia simu nzuri za I phone?!.
Niicharge I phone yangu, nika iwasha ili kui sinc na MacBook yangu, duu!, nikashangaa hazionani!, kujaribu camera, nikakuta ni utumbo mtupu, kwenda kwenye I tunes, haiendi!, nikawasha tena bluetooth ku browse computer yangu, ikagoma ku pair!, ndipo sasa nikafunguka macho!...yaani hata mimi?!. Kumbe nimeingizwa mjini hivi hivi huku najiona!. Hivi sikustuka jamaa kaanzia 1.5 na kushuka mpaka laki 3, na mimi nimeendewlea kupelekwa tuu kama ling'ombe!. Inawezekana hawa jamaa wanatumia dawa?!. Ila kiukweli huyu Mchina sasa ni mwisho!, kama huijui the "original" thing!, you can't tell a difference!.
Swali kwa mnaoijua I phone ya ukweli, ina nini cha ziada mbona hii ya mchina ina karibu kila kitu?!.
Nimechaki bei ya I phone 5 ya ukweli kwenye net ni $ 199 (16gb), $299 (32gb) na $399 (64gb), nini kinachoifanya hii I phone 5 iuzwe kwa milioni 1.8 hadi 2.4 maduka ya hapa kwetu!?.
Pasco.