Waziri Mchengerwa: Nilipewa bajeti ya dola laki 5 ili kununua basi moja la mwendokasi

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,755
15,238
Waziri wa Tamisemi Mh Mchengerwa amesema alishangazwa baada ya kuletewa bajeti ya manunuzi ya dola laki 5 kwa basi moja la mwendokasi.

Mchengerwa aliifutilia mbali hiyo bajeti baada ya kubaini ni sawa na kununua behewa la treni.

My take:
Hawa wapigaji mbona hawachukuliwi hatua? Rais Samia pia alishawahi kulalamika na kutukana stupid baada ya kugundua bei ya ndege imeongezwa mara 3 zaidi!

Pia uwanja wa mpira utakaojengwa Arusha ambao utakuwa mdogo kabisa wenye uwezo wa kuingiza watu elfu 30 tu kama ule wa New Amaan Zanzibar, bajeti yake imetengwa billion 286, hela ambayo ni nyingi mara nne kuliko uwanja wa Mkapa ambao unauwezo wa kuingiza watu zaidi ya elfu 60!

Je, tabia hii ya kuongeza bei ya miradi tungeweza kweli kuhamishia serikali na kujenga ikulu Dodoma, kujenga bwawa?

Pia soma:

Serikali kutumia Tsh. Bilioni 190.57 kununua V8 mpya za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ujenzi wa Makazi na Utawala
 
Waziri wa Tamisemi Mh Mchengerwa amesema alishangazwa baada ya kuletewa bajeti ya manunuzi ya dola laki 5 kwa basi moja la mwendokasi !
Mchengerwa aliifutilia mbali hiyo bajeti baada ya kubaini ni sawa na kununua behewa la treni.

My take
Hawa wapigaji mbona hawachukuliwi hatua?
Rais Samia pia alishawahi kulalamika na kutukana stupid baada ya kugundua bei ya ndege imeongezwa mara 3 zaidi!

Pia uwanja wa mpira utakaojengwa Arusha ambao utakuwa mdogo kabisa wenye uwezo wa kuingiza watu elfu 30 tu kama ule wa New Amaan Zanzibar, bajeti yake imetengwa billion 286 !, hela ambayo ni nyingi mara nne kuliko uwanja wa Mkapa ambao unauwezo wa kuingiza watu zaidi ya elfu 60!

Je tabia hii ya kuongeza bei ya miradi tungeweza kweli kuhamishia serikali na kujenga ikulu Dodoma, kujenga bwawa ?
Ukute hata kuongea hivyo anadanganya ili kuhamisha tatizo!
Kifupi "mbwa koko" huwezi kumbadili tabia ili umfuge, unamuua.

Viongozi wetu karibia wate wameharibika.
 
Natafakari hizi pesa zote zinazochezewa nchi hii kuanzia kwenye ripoti ya CAG ukizijumlisha napata jibu kweli hii nchi sio masikini. Magufuli alikuwa sahihi.

Wameigeuza nchi shamba la bibi wanachuma wapendavyo, wanajaribu kuiba hapa wakishindwa wanaenda kuiba pale, naamini hata hapa navyoandika hivi wapo wanaowaza kuiba huko kwenye ofisi za serikali.

Mchengerwa angetakiwa atuambie aliwaagiza TAKUKURU wafanye uchunguzi, lakini badala yake anatuambia tu aliifutilia mbali hiyo bajeti, hii ni sawa na kuwaruhusu wakajipange kwa wizi ujao tena.

Mtu akishakuwa na nia ya kuiba, nia yake haiwezi kwisha mpaka atakapofanikisha lengo lake, kinachotakiwa kabla hajafikisha lengo, awahishwe mahakamani akatulie huko.
 
Waziri wa Tamisemi Mh Mchengerwa amesema alishangazwa baada ya kuletewa bajeti ya manunuzi ya dola laki 5 kwa basi moja la mwendokasi !
Mchengerwa aliifutilia mbali hiyo bajeti baada ya kubaini ni sawa na kununua behewa la treni.

My take
Hawa wapigaji mbona hawachukuliwi hatua?
Rais Samia pia alishawahi kulalamika na kutukana stupid baada ya kugundua bei ya ndege imeongezwa mara 3 zaidi!

Pia uwanja wa mpira utakaojengwa Arusha ambao utakuwa mdogo kabisa wenye uwezo wa kuingiza watu elfu 30 tu kama ule wa New Amaan Zanzibar, bajeti yake imetengwa billion 286 !, hela ambayo ni nyingi mara nne kuliko uwanja wa Mkapa ambao unauwezo wa kuingiza watu zaidi ya elfu 60!

Je tabia hii ya kuongeza bei ya miradi tungeweza kweli kuhamishia serikali na kujenga ikulu Dodoma, kujenga bwawa ?

Hapo kwenye uwanja wa mpira wa Arusha kujengwa kwa bil 286 nilishangaa sana, hiyo gharama kubwa sana jamani kwa kiwanja cha watu 30,000

Mh. Rais Samia hapa inafaa aangalie upya hii ya uwanja wa mpira wa Arusha kuna mashaka sana sana, hela nyingi mno
 
Maigizo hayo, wote ndio wale wale tuu hapo alikua kwenye harakati za kutafuta sifa kwenye macho ya watu, hata hiyo bilioni 230 ya uwanja Arusha ni wizi tuu hiyo ni pesa ya kujenga viwanja vitatu vya kisasa kabisa lakini hii ndio maana ya kula kwa urefu wa kamba kama alivyo agiza mama yao
 
Nikichogundua ww ndio sio muelewa imagine bossi wako anakupa burungutu la hela halaf nakwambia iba tu ila kwa urefu wa kamba we ungefanyaje?
 
Aliyempa hiyo Bei Ni Edwin Mhede au huyu Kihamia.
PhD za Tanzania zimesomea kufuja Mali.
Lakini hata hivyo hao wahuni wapigaji si wamewateua wao wenyewe? Kwani waliteuliwa na upinzani.
CCM watagie nyumba Yao kwanza kabla hawajatuambia watu waliowateua wanapigaje pesa.
 
Mpaka unajiuliza hawa watu ni kina nani ambao hata rais mwenyewe anawagawaya? Au ni wale ambao anakula nao urefu wa kamba zao sasa labda unakuta wamezidisha kamba sasa kinachotokea unajikuta unalalamika na kutukana kimoyo moyo ambapo kuwachukulia hatua huwezi sababu wote ni wachafu mnajuana
 
Back
Top Bottom