Boxing day tumepigwa box

Boxing day tumepigwa box

Siku ya ndoa unapata taarifa kuwa bibi harusi mtarajiwa ni lara1 kwa nini usikimbie hiyo harusi?
 
Last edited by a moderator:
Chaa hiji ni uchiku nchana? Endeleza stori mkuu, usiku tayari huu
 
hapo ndipo nnapowakubali wanawake khaa.... ku play innocent kumbee ndio maana nshasema hawa xyz stak hata kuwaskia..........
 
Sasa mambo ndiyo yakawa hivyo, harusi imegeuka msiba.
Watu wakaanza kujaribu kuficha mambo yasiende nje but we all know BAD NEWS TRAVEL FAST.
Kina shangazi wakaanza kutuma SMS kwao huko; harusi hakuna.
Kina maza wakubwa nao wanatoka nje kupokea simu, daah ikawa shida.
Yule mtoto wa mshenga anatukanwa matusi makubwa na familia yake na ya yule demu.
Mzee wake anakosa hadi raha mtoto wake ndiye kaharibu ndoa ya watu.


Tena baba wa yule mtoto wa kigogo anogopa naye pozi limeisha,
kumbe yule fiancee wa mtoto wa kigogo naye ni mtoto wa kigogo mwingine mwenye heshima zake tu. Si ujajua Birds of the same feathers flock together!!!!
Incase harusi haifungiki then basi mambo yakiharibika kwa huyu demu wa brother ni dhahiri kabisa kwamba lile jamaa toto la kigogo halitaoa nalo.
Mama wa binti analaumiwa sana na mumewe kwa kulea ujinga,
Naskia familia nzima kimenuka binti kawatia aibu nzito.


Sasa huku kwa brother,
Ile naendelea mazungumzo kusema ntoe simu ncheki muda nakuta simu simu inaita namba ngeni. Sikupokea, huwa sina mazoea ya kupokea namba ngeni.
Jamani sijawahi kupata Missed calls nyingi vile, SMS nyingi balaa.
Kila mtu anataka kujua what was going on.

Ile simu ilivyoendelea kupiga, nkamwabia brother naenda chooni one time kumbe naenda kupokelea toilet.
Ile nasema halloo kumbe ni lile toto la mshenga likaulizia mko wapi?
Mimi nkamwambia siwezi kukwambia jamaa linataka hadi kulia kwasababu kila mtu analitukana so linataka lije pale limbembeleze brother akubali


Huwezi amini hadi yule mzee kigogo alinipigia simu,
Sema sikupokea brother alinikataza nsipokee.Jina lake nalionaga kwenye magazeti tu.
Nkauchuna tu, mzee akatuma sms anataka kuongea na brother ila ndiyo ikawa haiwezekani.
Na kwa bahati mbaya chaji ilikata nimekesha na simu toka jana sijachaji na watu wamepiga kweli.


Brother aliniambia kauli moja tu,
You are too young for this. Ukikua zaidi utaelewa.
Mimi ikabidi niwe mpole tu kwasababu kweli binti kazingua saana.
Tangu nakua sijawahi kuona mwanamke kapendwa vile.
Trip za Zanzibar kwa saaana, jamaa akiwa anaenda hata sehemu yoyote nzuri nje ya nchi akiwa na mkwanja ni lazima waende wote.


Yani full bata hadi masista wakawa wanaponda,
Si unajua wivu wa kina dada?
Wanasema wewe usimdekeze sana huyo itakula kwako.
Tukawa tunachukulia pouwa tu; si utani kumbe watoto wa kike wanajuana kwa vilemba.


Bro akasema bibi harusi kajichagulia fungu lake,
Na mimi sirudi nyuma; japo mimi najua inamuuma lakini ndiyo basi tena.
Kaniambia nilimpenda sana ila ndiyo basi tena kischo ridhiki hakiliki.
Kama yuko nje ya ndoa anafanya hivi, akiingia je?

Akaniombama nimsindikize ATM tukaenda, kulikuwa na foleni kiaina.
Mimi nkaenda duka moja la M-Pesa ni jirani na Bank kuna dada moja namfahamu nikaomba niboost simu wakati bro yuko foleni.
Ile simu inawaka nkampigia baba simu nkamwambia mzee nimeshindwa.
Mzee kaniambia try hard mchana unaingia huku watu washaanza kufika kanisani; na watu wamefurika balaaa.
Tobaaa ile namaliza kuongea na simu kumbe na wale masista wa M-PESA habari zishawafikia mudaaa,
nkashangaa. Wakaniambia mujini ishakuwa gumzo balaa, akanionyesha Message kwenye magroup yake ya Whatsapp watu wanaongea balaaa.
Masista duuh wa mujini wamefurahia kweli hiyo ndoa kutokuwepo kwasababu bro anafahamika balaa tangu yuko anafanya kazi VODACOM.

Huku home sasa,
Wale wazee wa yule binti wakamwomba mama hata akubali kuliambia kanisa kwamba bibi harusi anaumwa, harusi isogezwe mbele hata mambo yaishe kiustaarabu.
Lakini mchungaji akasema ni bora ukweli usemwe yaishe kuliko kuficha, itakuja kuleta madhara baadae.


Sasa town nako,
Ile narudi kumcheki bro pale ATM naye ndiyo naye akawa anatoka,
Akaniita kwenye kona akaniachia hela ndefu kweliiii,
machozi yanamlenga mishipa imemtoka kweli daah.
kumbe ile jamaa alitunza pesa kiba kwa ajili ya honey moon ila ndiyo kanipa na mimi fungu wala sikukataa.


Jamaa huwa halii hata chembe,
Misiba inapita yeye chuma cha pua tu. Lakini jana alishikwa pabaya.
Akaniambia rudi home dogo na let no one burden you with something you can't handle.
Akaniaga kasema anarudi mikoani, plus he needs a time alone to rethink about his life.
Tukaenda mpaka sheli ya mafuta akajaza zake mimi akaniacha nkarudi pale M-PESA nkachukua simu yangu then kwenye bajaji hadi church kwa pastor kumpa mrejesho.


Kufika kwa mchungaji,
Basi pale church nakuta watu wamefurika,
Basi mchungaji ikabidi atangaze msiba.
Wenye kulia walilia, wenye kusikitika walisikitika.
Lakini HAKUNA NAMNA TENA.
Binti kazingua!!!!!!!
Mimi niliogopa hata kuingia church ikabidi nibaki ofisini kwa mchungaji tu. Full aibu.

Nilivyofika home,nkaanza simuliwa na masista sasa.
naskia binti yule fiancee wa mtoto wa kigogo wazazi wake wamekinukisha,
demu kamtukana matusi ya nguoni na pete aliirusha chini, full kulia.
Kamtukana mitusi ya nguoni bibi harusi kwenye simu hadi basiiii.
Maskini bibi harusi kakosa vyote,
Aliwataka mtoto wa kigogo na brother mwishowe kawakosa woteeeee.
Nkaskia alitaka hadi kufa, hali yake si nzuri hata kidogo.
Hakuna hata anayehangaika naye.

Baba wa yule msichana na ndugu zake walikuja jana Usiku home,
Mzee watu aliomba sana msamaha; daah hadi dingi alijisikia vibaya.
Baba mtu ni mstaarabu balaa, nkaja kujua ni mamaza ndiyo wanaoharibu watoto wa kike.
Wakasema walipenda sana wawe ndugu zetu lakini Mungu hakupanga.
Walikuja kurudisha hela ya mali na wakasema watasaidia kufidia gharama za harusi,
lakini mzee wangu akakataa katakata kupokea akasema ile siyo biashara na bahati mbaya huwa zinatokea na watoto ndivyo walivyo.

Leo asubuhi sana mzee kaitisha kamati,
Japo nao wamekataa kurudishiwa michango yao kwasababu wengi ni ndugu wa karibu.
Ila michango ya watu wengine wa nje ndiyo tunarudisha.
Daah bonge la hasara, kisa tamaa ya mtu moja tu.
Kweli inatisha hasira saana.

Mchana huu Mzee kasafiri kaenda kumfuata brother huko kwake,
Kasema ni lazima arudi wayamalize siyo kukimbia-kimbia matatizo,
Kauli hii sijaielewa hata kidogo na sijaipenda kwa kweli.
Sasa sijui huyu mzee anataka jamaa aoe tena au?
Kaenda na timu ya wazee kama kumi hivi, pamoja na washenga wote wawili.
Naskia yule mzee anataka kumwomba radhi brother.

Bibi yangu mzaa baba,
alikuwa anampenda sana binti yule, yaani ni balaa!!!!
Na ndiye aliyemwambia baba kwamba mbona kuna wanandoa wanazaa hadi kuzaa ila maisha yanaenda, Huyu mjukuu mbona ana hasira hivyo?
Hajui kusamehe?
Misimamo gani hiyo jamani?
Mrudisheni hapa aje tuyamalize kama familia siyo kukimbia tu.



Yaaani hapa ndiyo nkaona huyu bibi naye ananingizia mbu kwenye neti,
Eti asamehewe?
Kwa misingi ipi?
Mimi sisamehi mtu.
Sema nkauchuna tu.
Wazee wanajaribu kutumia busara lakini it is too late.
Navyomjua brother huwa habadiliki.

Jamani ndiyo yameshatokea,
Harusi hakuna sasa hivi natafuta tu mteja wa tuxedo yangu mpya.

Ame kweli binti naye kapata zawadi yake ya BOXING DAY.
 
It's a sad story, ila umefanya kosa kumuacha Broh a-drive kurudi mkoani anapoishi... Angeweza kupata bonge la ajali na ungejilaumu sana..kwa Hall yake alipaswa kutafuta tu hotel hapa town atulie all alone ila sio kusafiri alone tena yeye mwenyewe ndio dereva.
 
Back
Top Bottom