Boxing day tumepigwa box

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
21,035
64,851
Wasalaaam,
Wakubwa shikamoo, wadogo marahaba.
Wahenga wanasema ukistaajabu ya mussa utajashangaa ya firahuni.

Jana was boxing day na kweli familia imepigwa box za kichwa kibao.
Kuna mambo mimi nakua nilidhani yanatokea tu kwenye movie au kwa vitabu vya Shigongo.

Jana ilibidi kuwe na harusi ya nguvu ya brother wangu bwana.
Lakini to my surprise he called off the wedding.
Duuuh sad aisee.

Asubuhi ya Boxing day naenda home sasa kusalimia baada ya kuruka usiku wote wa Christmas.
Nakuta zile nderemo za jana hazipo, sebule kimya kama kuna msiba.
Nakuta maza analia hadi kwikwi; mimi sijui kuna nini kinaendelea.
My mother is too fragile yani daah.

Sasa nauliza kuna nini, mara naitwa kwenye room hivi.
kulikuwa na mshenga wa familia yetu na familia ya yule binti na wazee wengine.
Mara nkambiwa bwana harusi haipo ndiyo maana unaona pako hivi.
Nlishangaaa kinoma.

Kuuliza wakasema ndugu yako kagoma kuoa,
Nkataka kujua kisa; wakasema kumbe binti alikuwa na mahusiano toto fulani la kigogo na hadi jana lilikuja kwenye harusi kwa upande wa mwanamke.

Navojua mimi lile jamaa na yule manzi ni family friends wazuri tu,
na binti wa watu ni mstaarabu kweli.
Huwa nalionaga tu kitaa na kaka wa yule manzi sana.

Nlibaki nacheka tu,
Nkawaonea huruma wazee.
Ukumbi washalipia, Chakula tayari, wamelipia hadi hoteli ya kufikia ndugu za mwanamke, wapiga picha, sijui zawadi ya familia na hadi hela ya fungate.

Juzi juzi tu dada zangu wametoka kutafuta nguo za harusi,
Wengine jana wameshinda saluni.
Ndugu wa pande zote wamesafiri toka mbali.
Hivi unawaambiaje?
Si Aibu ya kufungia mwaka hii.

Maskini naangalia simu ilikuwa silent na hata sipendi vibration inakula chaji nakuta missed call zaidi ya mia.
Binti wa watu kapiga simu, brother zake, mzee na brother mwenyewe.
Nkajua tu hapa kishanuka.

Mzee wangu mbabe sana na mkoloni vibaya,
Ila siku ile alinywea kawa mdogo kama piritoni.
mtoto anataka kumvua nguo.

Akaniomba niongee na brother,
kwasababu mimi ndiye tupo close sana na isitoshe brother ndiye kanisomesha mimi so tunaelewana sana.

Mimi nligoma nkasema nashauri nini sasa?
Kama hajawasikiliza ninyi atanisikia mimi?
Nkawaambia mimi kwanza ni Junior i just turned 23 few months ago.

Ila wazee wakakomaa wakaanza kunipamba ujinga,
Mara Unajua wewe una busara sana,
Mara wewe you are gifted in persuasion.
Wakati huyu huyu mzee alishwahi sema mimi ni Luggage hapa nyumbani.
Na hata siku nije na chchote chema yeye lazima asema umebahatisha.
Simply Mkoloni.

Nkakubali sema kwa shingo upande,
Naona wenge tu. Najipa matumaini yule binti hajafanya kitu kasingiziwa.
Nalinda heshima za watu jamani.

Nimepiga simu brother hapatikani,
Sema nkajua brother anapopendelea kushinda.
Mimi mdogo mdogo hadi town, nkategemea ntamkuta mtu kachanganyikiwa.

To my surprise nakuta bro kakaa peke yake,
Alivyoniona kanichangamkia kweli na mtu mwenye furaha ova hakijatokea kitu.
This made me very nervous.
Sasa kukaa akanimbia dogo usije ukafanya ujinga kama mimi kaka yako. Never in a lifetime.
Aliyonisimulia hapo hadi ladha ya harusi iliisha,...
Nkashau hata nlichotumwa kufanya.....

Daah wadada mnazingua sana,
Hivi kumbe kwenye ujinga wa mtoto wa kike hata mama huwa anachangia.
That's a fact.

Itaendelea.........






 
Hii story ungeileta jana leo ingekuwa imeisha tayari,, tusingehangaika kusubiri leo.
 
Mara Unajua wewe una busara sana,
Mara wewe you are gifted in persuasion.
Wakati huyu huyu mzee alishwahi sema mimi ni
Luggage hapa nyumbani.




Nimefurahia hapo tu.
 
Ile kukaa na brother akaniuliza is mother okay?
Nkamwambia she's overwhelmed.
Akaniambia hakupenda kumwona maza kwenye such situation.

Brother akaanza kunieleza kinaga ubaga yaliyomsibu.
Binti ana madhaifu kibao tu, sema kuna ile hope ya kibinadamu kutegemea mtu anabadilika.
Sasa ijumaa ya Kuelekea Christmas walienda kupokea wageni wa huyo ndugu wa mwanamke ili kuwaelekeza hotelini na kadi za kuingilia ukumbini. Kazi hiyo nilipewa mimi Young MALCOM sema nkamwambia bro sitaweza kwenda kwasababu namalizia mipango fulani ya kazini.
Aisee najuta kutokwenda hiyo siku hiyo.

Sasa bro mshenga na marafiki zake hao mdogo mdogo mpaka huko kwa wageni.
Wakawapeleka wazazi kwa hoteli, sasa kuna timu ya marafiki na ndugu wao walikaa hoteli nyingine.Mshenga ni mzee akageuza kwasababu keshaonana na ndugu wa muhimu.

Kazi ya kadi zilizobaki bro aksema atapeleka tu kwa hao ndugu.
Brother na wenzake wakaenda hiyo mitaa sasa siyo mbali na hapo,
Wakawapigia simu hao majamaa; kumbe wako kwenye Pub fulani wanapiga mvinyo.
Wengi wao pale ni marafiki wa ile familia na kama 30's and 40's hawamjui brother kama ndiyo bwana harusi.
Hata kwenye Send Off hawakuwepo.

Basi kama kawaida be my guest ndiyo ikaharibu everything,
Majamaa wangine wanaangalia sijui mechi maskini bro naye akakaa acheki.
Sasa pombe kukolea jamaa moja akaanza,
Hivi unajua nimestushwa sana na harusi hii hata sikujiandaa.
Akaendelea kusema daah yeye yuko Malaysia akaambiwa eti fulani anaolewa.

Akasema X(bibi harusi) ni ndugu yangu ila kama anaolewa basi kila demu anaolewa.
Brother wangu ni mtu PASSIVE-AGGRESSIVE hata ufanyaje huwa hapaniki na mpole kinoma.
Wale jamaa wa mezani wakamuuliza kwanini unasema hivyo?
Akasema mimi yule namfahamu tangu anasoma Malysia ni tatizo.

Brother kimya tu yuko perplexed,
ananiambia jasho linamtoka wenzake wako pale vichwa chini wanashindwa hata kumwangalia na kumwambia jamaa asiendelee.
Hili libraza lake likaanza kusimulia kwamba dogo alikuwa na Uhusiano na mtoto wa kigogo tangu wako Chuo huko Malaysia. Waliachana na hilo toto la kigogo lilivyoenda Kusoma sijui PhD Uingereza; demu yake akafanyia Canada.

Kumbe muda huu mambo yananendelea Malaysia bro ndiyo mahusiano yamekolea.
Kumbe kuna kipindi katikati binti walishwahi zinguana na brother kuhusu huyo jamaa.
Binti akasema ni mtu tu wa ofisi na family friend hata home wanamjua.
Kumbe Uongo mtupu.

Sasa ile dada karudi Tanzania,
Kwanza kapata kazi bonge ofisi.
Brother kuna Wajerumani alisoma nao akamwombea kazi pale na ile kukuta binti yuko vizuri kichwani ikawa rahisi sana tu.
Kumbe brother anamsaidia mwanume mwenzake kulea.

Brother akasema kimoyo kama ni hayo mbona walishayamaliza,
Zinaweza zikawa fitna tu au maneno ya watu.
Sasa ile pombe imekolea yuke ndugu mtua akasema "Naskia jamaa anayetaka kumuoa ni mtu poa kishenzi, duuh kweli wanaume tunachezewa"
Akaaendelea j5 hiyo demu alila kwa huyo mtoto wa kigogo na ameondokea alhamisi kwake.

Kuna rafiki ya brother ikabidi aingile kati aanze kumchana yule jamaa kama mzushi,
Jamaa limelewa sasa lishakuwa bishi likatoa simu likaanza kuonesha SMS za yule mtoto wa kigogo wanataniana na yeye kwamba dogo langu siku hizi humwezi.

Jamaa kamtumia message eti "i was just reminiscing nothing special man, it happened so quickly and i couldn't help it. Nature has no medicine"

Tena SMS nyingine jamaa kaandika "Unajua atakuwa mke wa mtu keshokutwa, so i regret what i did. Hata yeye mwenyewe kakosa furaha"

Sasa kumbe hayo mahusiano ya hao wawili mama yake binti ndiyo aliyeyabariki na alitaka mara ya kwanza hilo jamaa lioe binti yake.
Kuna kipindi lilishawahi kufanya kazi na huyo maza ofisi moja kumbe maza anausoma mshahara wa lijamaa ni mkubwa balaa.
In short kumbe ndugu walitaka mtoto wao aolewe kwa kigogo.

Lakini toto la kigogo lina binti mwingine kichwani,
na hivyo binti akawekwa kapuni tu.
Jamaa lishamtambulisha huyo fiancee wake hadi kwa huyu mchumba wa braza.
Na wifi ni kibao tu na brother ashawahi kutana nao pale Mlimani City wakiwa pamoja kama mara 3 hivi.

Haya turudi sasa kwa bro,
Kaondoka na majaa ghafla bila hata kuaga.
Huyoo kwenye gari kampigia simu binti yuko na wenzake town kamfuata hadi alipo.
Cha kushangaza lile lijamaa lipo naye na yule fiancee wake na watu kama 6 hivi wanapiga story.
Demu akamwambia braza anapiga story za kimwisho mwisho kabla ya kuolewa.

Brother akatabasamu tu,
akapiga nao story mbili tatu akawaambia akasepa bila kusema chochote.
Sasa jamaa alivyo na roho ngumu akasubiri Christmas iishe na siku ya harusi ifike ndiyo atumbue JIPU duuh.

Asubuhi imefika jamaa kamwita mshenga wa binti pale sasa sebuleni,
Ndugu wote wakaitwa jamaa akasema hakuna harusi leo.
Na uso mkavu kabisa.
Ndiyo kueleza hayo yote mambo yakawa hivyo.


CC: mwekundu, Raimundo, Moisemusajiografii, Jackichanii, kijani11, Born2xhine, Hansss, Molembe, luckyline, Zamiluni Zamiluni, kkenzki

 
Last edited by a moderator:
Sasa yule mshenga na kina maza wakamvaa jamaa kwamba anataka kuwapotezea muda,
Anataka kuwafanya watoto wadogo; anasikiliza maneno ya watu tu.
Hajiamini na mke wake. Elimu haijamkomboa.
Mama yetu mkali na dingi wote wakali.

Wakataka ushahidi uje,
Brother hakuongea akatoka nje kwa hasira rafiki yake did all of the talking.
Sasa mshenga wa binti akataka ushahidi kawa mkali kama mbogo.
Jamaa akataja jina la aliyesema hayo yote.

Haahaaa kumbe lile jamaa ni litoto la yule mzee mshenga,
mzee wa Kihaya posi liliisha ghafla.
Jasho tupu.
Mzee akalipigia simu litoto lake hata halipokei, kupiga jamaa ndiyo likaanza safari kuja home likaelekezwa hadi kufika.
Naskia linanuka pombe full hang-over baba mtu akaanza sasa kuuliza wewe umemwambia nini bwana harusi?

Jamaa linashangaa,
Bwana harusi gani?
Mchumba wa dada yako X?
Jamaa kuangalia vizuri sebuleni likamuona rafiki ya brother aliyekuwa naye jana.
Jamaa naskia nusu lizimie pale sebuleni. Likajua rafiki ya bro ndiyo bwana harusi.

Bro akaingia ndani akaenda moja kwa moja kwa lijamaa akalinyang'anya simu jamaa likajaribu kufurukuta lakini wapi.
Likaanza kuleta uzungu wake wa kihaya pale oooh mara right to privacy.
Right to privacy MY NECK!!!
Wazee wakasema kama simu haina kitu kwanini muogope?

Si ndiyo kuanza kusoma SMS pale kucheki namba ya Tigo Pesa ni jina la yule mtoto wa kigogo.
Na zaidi yule binti naye kumbe huwa wanautani na hilo libraza hadi hiyo j5 anaenda kulala kwa hilo jamaa ilikuwa kama utani na binti alimwambia kabisa jamaa.

Jamaa kukuta ni kweli sebule nzima kimya kirefu,
Naskia lijamaa limeshiwa kujitetea mara nlikuwa nimelewa tukawa tunataniana tu.
Pumbavu wewe umelewa wiki nzima???IDIOT

Mshenga akapiga simu kwa binti; kapokea kwa bashasha leo anaolewa.
Mzee akamuuliza tu J5 ulilala wapi?
Binti kigugumizi ghafla. Akaanza ooh kwani vipi?
Mzee akamchana ukweli wote pale.
Binti kaangua ngolo kwenye simu.

Sasa wazee wakajidai wanatumia busara pale,
Eti ni heri uoe halafu mtaachana.
Mara ooh jamani tunza heshima ya familia kijana.
Usiwafanyie hivi ndugu zako.

Viongozi wa dini wakaja ikagonga mwamba,
Ndugu ikagonga mwamba.
Iisee ilishindikana. Zikaanza kupigwa simu pale home.
Wazazi wa binti wakaelezwa na mshenga wao pale huko hotelini hapakaliki.
Naskia mzee wa yule binti akamvaa maza mtu na mashangazi.
Walipiga simu kwa mama na baba lakini jamaa keshagoma.

Sasa yule mtoto wa kigogo si ndiyo kachanganyikiwa ikabidi familia yake itake responsibility.
Wazazi wake wakapiga simu kwa brother, simu haipokelewi.
Wale wazazi wa lile jamaa walikuja kuharibu hali ya hewa baada kusema aoe tu watampa kiasi cha pesa siri isitoke nje.
Naskia mzee alimind balaaa

Sasa ya bibi harusi mtarajiwa huku ndiyo yalikuwa makubwa.

Itaendelea leo usiku.


 
Back
Top Bottom