Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,681
- 106,794
Wapenzi wa movie😅😅😅
Tulishachotwa akili kweli na hawa watengenezaji wa muvi. Hivi lini bongo movie tutafika huku..walishawahi kupata hata Tsh 10Mil???.
Issue Ipo hivi....
Muvi ya Avatar ilitoka 2009 ikashika rekodi ya kua muvi iliyoingiza pesa nyingi zaidi duniani baada ya kuvunja rekodi za Titanic na Lion King (1992)
Mwaka 2019 ndio ikatoka Avanger Endgame ikavunja rekodi ya Avatar kwa kupata Dollar 2.797Bilions, sasa bwana wiki iliyopita Director wa Avatar David Cameron akasema anahitaji $Mil 7 tu aweze kuivunja rekodi ya Endgame. Avatar ikaonyeshwa tena huko kwa Xi Jiping akapata $12.3Milions kwa siku mbili. Kafikisha kiasi cha Dollar 2.802Bilions.
Hivyo avatar imerudi kwenye rekodi yake ya muvi iliyoingiza pesa nyingi zaidi duniani..
Mashabiki wa Marvel Studio/Marvel Cinematic Universe nami nikiwemo😅😅 wanawashinikiza Director wa Avanger Endgame Joe na Anthony Russo na producer wa Marvel Studio Kevin Feige waionyeshe upya muvi warudi kwenye rekodi yao.
Kweli vita ya panzi ni furaha ya kunguru, Marvel Studio inayomiliki Avanger Endgame ni kampuni tanzu iliyonunuliwa na Disney Company...Lakini pia kampuni inayosambaza muvi ya Avatar ambayo ni 20th Century Fox nayo inamilikiwa na kampuni ya Disney Company. So technically faida yote inaenda kwa Disney wakati sisi huku tunaparuana macho😆😆