Bouncer ameolewa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,773
Habari za leo wapendwa
Huyu shosti ni tangia ile shule ya boda, lakini tangu shule alikuwa anatukondesha mbaya, shost huyu alikuwa mbabe, dining alikuwa anachota top layer ile yenye mafuta yote alafu huyo anaondoka kabla hamjaaza kusave kwenye sahani zenu.

Zile siku za shida ya maji, umechota maji umeyaweka mvunguni, shost huyu anachukua maji na anakuamsha mkaoge kama mliyachota pamoja, na lakumwambia huna. Si unajua baada ya shule kila mtu ki vyake.

Mjini si unajua unanyimwa chakula na njaa hii lakini maneno ni buree, basi nyepesi nilizozipata ni kuwa shost alitumiwa ujumbe afike baa flani mume wake anajivinjari na totos za bank, amefika pale akakuta jamaa anatangaza ufalme meza imechafuka vyakula na mazagazaga kibao,

shost alipige teke kila kilichokuwepo mezani, na mdada aliyekuwa pembeni mwa bwana shemeji alichukua kibao cha heshima kilichopelekea meno kadhaa kudondoka, baada ya hapo akamwambia mumewe aamke waondoke mume kama kondooo huyooo.

Bwana shemeji amefika ofisini kesho yake anaanza kuomba msamaha kwa mchepuko, akamwambia ameshafanya appointment na dentist saa tisa wakutane kwenye clinic flani, khe ile saa tisa bwana shemeji amefika clinic anakutana na shost amejaa pale, kumbe habari alishazipata kuwa wanakuja.

Kumbe nyumbani jamaa anapata vibao vya heshima na wala hawezi kusimula kwa mtu yeyote kuwa my wife wake huwa anampigaga.
Basi nitunzieni hii siri jamani mwenyewe asijesikia kuwa niliwaeleza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom