BoT yawang'ang'ania mafisadi wa EPA baadhi wapewa likizo za mwezi

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Na Ramadhan Semtawa

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema hakuna mtumishi wake miongoni mwa wanaotuhumiwa katika upotevu wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), atakayesalimika katika mchakato wa kuwashughulikia utakaokamilika hivi karibuni.

Onyo hilo lilitolewa jana na Gavana wa BoT, Prof Benno Ndulu, kufuatia tuhuma dhidi ya Kamati Maalumu ya Nidhamu kuwa, limewatoa kafara baadhi ya maafisa wa kati wa benki hiyo huku wa ngazi za juu waliohusika na ufisadi wa fedha za EPA wakiachwa na kuonya itawalipua vigogo wa juu wanaoachwa.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma hizo, Prof Ndulu alisema, BoT katika maamuzi yake imekuwa ikizingatia ripoti ya kitaalamu ya Kampuni ya Ernst & Young kuhusiana na suala hilo.

Kampuni hiyo ndiyo iliyobaini ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni za EPA katika hesabu za mwaka 2005/06, ufisadi ambao awali uliibuliwa na Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini, kabla ya kusitishiwa mkataba ghafla.

Prof Ndulu alifafanua kwamba, ripoti hiyo iliweka bayana kila idara na udhaifu wake pamoja na wahusika, hivyo wanafuata ushauri huo.

Kwa ufafanuzi zaidi, Prof Ndulu alisema baada ya BoT kupitia kwa kina ripoti hiyo, ilifanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa adhabu kwa watuhumiwa.

"Sielewi wanachokisema, tunaongozwa na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ernst & Young waliobaini wahusika, huko ndiko tulikoanzia sisi," alisema Prof Ndulu na kuongeza:

"Hata sisi tulifanya uchunguzi wetu wa kina, hatumuonei mtu wala hatutamuogopa mtu yeyote katika kuchukua maamuzi na hatua za kinidhamu. Subirini mchakato ukamilike mtaona, kama kuna atakayeonewa au atakayeachwa, mchakato bado unaendelea."

Wakati Prof Ndulu akisema hayo, taarifa zinasema kuwa, mchakato huo wa kung'oa baadhi ya watumishi bado unaendelea huku wengine wakienda likizo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya watu ambao majina yao yanatajwa na yameonekana zaidi katika nyaraka za malipo ya EPA na ambao wamo katika ripoti ya Ersnt & Young, wako likizo za mwezi mmoja ikiwa ni sehemu ya kupisha uchunguzi.

Hata hivyo, baadhi yao ambao tayari walipewa barua za kuachishwa kazi wamekata rufaa na kwamba bado zinapitiwa na jopo Maalumu la Kamati ya Nidhamu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kuna uwezekano mkubwa wa baadhi yao kupewa barua za kuachishwa kazi muda tu baada ya kurejea au hata kabla ya kurejea, kisha wataruhusiwa kukata rufaa kama walivyofanya baadhi yao.

Mchakato huo wa BoT kung'oa watumishi waliohusika kutia taifa hasara katika EPA, unafanyika kwa makini ili kuondoa uwezekano wa benki kushtakiwa na kuweza kuwalipa watuhumiwa mamilioni ya fedha.

Hata hivyo, kumekuwa na tuhuma ya kuwepo taarifa kwamba, BoT katika mchakato huo wa kuwaadhibu watuhumiwa wa EPA imekuwa ikitoa kafara maafisa wa kati huku wale wa juu zaidi wakiachwa, hali ambayo imefanya baadhi yao kuapa kuwalipua vigogo zaidi.

Wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma wiki mbili zilizopita, Rais Jakaya Kikwete, alisema BoT kwa kutumia mamlaka yake itachukua hatua kwa wahusika na kisha itatoa taarifa kwa umma.
 
Benno Ndulu hana credibility ya kuleta objective reforms BOT.

Wakati uozo wote unaendelea yeye ndiye alikuwa second in command, unategemea nini sasa?
 
Mnyama Fisi hata akiwa na njaa kiasi gani kamwe hali mzoga wa Fisi mwenzie.
Ndulu hana uwezo wa kuwarudi wenzi wake ni fisi kamwe hali nyama ya fisi mwenzie.
 
Waache hizi blah blah sasa tunataka hatua inayofuata ichukuliwe mara moja; tena hatua kali ili iwaume mpaka wawataje hao wakubwa wao waliowashinikiza (kama kweli walishinikizwa)kufanya huu wizi.
Tuache kuzunguka na hili jambo forever, its been long enough for next steps to be taken.
This issue is too sensitive kwa mwananchi wa kawaida anayeishi maisha ya kubangaiza, while the country is eaten and destroyed by few monsters!
 
Benno Ndulu hana credibility ya kuleta objective reforms BOT.

Wakati uozo wote unaendelea yeye ndiye alikuwa second in command, unategemea nini sasa?

Pundit, nadhani hawa walidhani hii kitu ingekuwa imeshatulia, wanaona bado inawaandama tu kila kukicha. Alikuwa wapi miezi yote hii kuwachukulia hatua wahusika? Sasa wameona eti wawape likizo ya mwezi!!!! kwanini mwezi mmoja na siyo miezi 12, kwanini wapewe likizo badala ya kufukuzwa kazi kama kuna ushahidi tosha walihusika na ufisadi wa mabilioni ya EPA? Huyu Ndullu ni msanii, kama boss wale alivyoshindwa kuiongoza nchi, yeye pia kashindwa kuiongoza BoT.
 
kuna ukweli fulani kuwa maofisa walifukuzwa ni wale walioshinikizwa kusaini madude ya balali na mkapa
 
kuna ukweli fulani kuwa maofisa walifukuzwa ni wale walioshinikizwa kusaini madude ya balali na mkapa

Waseme hivyo basi ili ukweli uanikwe juani na ufanyiwe kazi,sio wao watolewe kama mbuzi wa kafara wakati Mkapa anapeta.
 
Msingi wa kuwaweka kwenye hatia hawa watu ungewekwa kwa kumjumuisha Balali moja kwa moja kwenye hili suala. Kushindwa kwa Serikali kumhoji Balali na kupata undani/ukweli wa hili jambo ni udhaifu ama upungufu uliofanywa kwa makusudi kukwamisha sheria kuchukua mkondo wake.
 
Benno Ndulu hana credibility ya kuleta objective reforms BOT.

Wakati uozo wote unaendelea yeye ndiye alikuwa second in command, unategemea nini sasa?

Si kweli Benno alikuwa second in command wakati madudu yanaendelea! Angalia kumbukumbu zako vizuri Pundit! Benno alikuwa WB wakati huo.
 
"Sielewi wanachokisema, tunaongozwa na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ernst & Young waliobaini wahusika, huko ndiko tulikoanzia sisi," alisema Prof Ndulu na kuongeza:

"Hata sisi tulifanya uchunguzi wetu wa kina, hatumuonei mtu wala hatutamuogopa mtu yeyote katika kuchukua maamuzi na hatua za kinidhamu. Subirini mchakato ukamilike mtaona, kama kuna atakayeonewa au atakayeachwa, mchakato bado unaendelea."
.[/FONT][/SIZE][/COLOR][/QUOTE]

Sasa sijui walifanya uchunguzi wao wa nini tena wakati ripoti ya Ernst & Young ilikuwa inawaongoza. Na katika mapendekezo ya Ernst & Young wako wakubwa waliopendekezwa kupigwa chini kama Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki wa wakati huo ambao JK alimteua kuwa Naibu Gavana. Wawapige chini watu waliopendekezwa kwenye ripoti ya Ernst & Young kwanza halafu wafanye uchunguzi kama kuna wengine waliohusika. Haiwezekani watu waliopendekezwa na ripoti kupigwa chini hao hao wanaongoza vikao vya kuwachunguza wenzao
 
Si kweli Benno alikuwa second in command wakati madudu yanaendelea! Angalia kumbukumbu zako vizuri Pundit! Benno alikuwa WB wakati huo.

Ingekuwa vizuri umtaje aliyekuwa second in command ili ku-set records vizuri..hoja hujibiwa kwa hoja daima.
 
"Sielewi wanachokisema, tunaongozwa na ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ernst & Young waliobaini wahusika, huko ndiko tulikoanzia sisi," alisema Prof Ndulu na kuongeza:

"Hata sisi tulifanya uchunguzi wetu wa kina, hatumuonei mtu wala hatutamuogopa mtu yeyote katika kuchukua maamuzi na hatua za kinidhamu. Subirini mchakato ukamilike mtaona, kama kuna atakayeonewa au atakayeachwa, mchakato bado unaendelea."
.[/FONT][/SIZE][/COLOR]

Sasa sijui walifanya uchunguzi wao wa nini tena wakati ripoti ya Ernst & Young ilikuwa inawaongoza. Na katika mapendekezo ya Ernst & Young wako wakubwa waliopendekezwa kupigwa chini kama Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki wa wakati huo ambao JK alimteua kuwa Naibu Gavana. Wawapige chini watu waliopendekezwa kwenye ripoti ya Ernst & Young kwanza halafu wafanye uchunguzi kama kuna wengine waliohusika. Haiwezekani watu waliopendekezwa na ripoti kupigwa chini hao hao wanaongoza vikao vya kuwachunguza wenzao[/QUOTE]

Buying time and missuse of taxpayers money. Its clear as glass!Dont u know this? watu wale wapi?nandio maana kina Mwema wameomba waongezewe muda upo hapo mzee?
 
Benno Ndulu hana credibility ya kuleta objective reforms BOT.

Wakati uozo wote unaendelea yeye ndiye alikuwa second in command, unategemea nini sasa?

Pundit,

Una uhakika na ulichoandika hapo juu? Tafadhali chunguza tena, unaweza kuwa unamwonea bure huyu professor.

Nijuavyo mimi Prof. Ndulu hakuwa BOT wakati hayo madudu yanatokea. Prof. alitolewa WB na kupewa kuwa naibu gavana wakati Ballali anakimbilia USA. nafikiri walikuwa wanamwandaa kuchukua ugava.

BOT wanatekeleza report ya E&Y. Sasa kweli hao wataogopa naibu gavana na huku walimtaja gavana mwenyewe?

Ballali ametajwa kwamba achukuliwe hatua, sasa kama waliweza kusema yeye achukuliwe hatua, kweli wangewaogopa akina Reli kama walihusika?

Ninachoweza kusema mimi ni kwamba akina Reli na wenzake inatakiwa waondoke BOT kwasababu walishindwa kuona hayo madudu yakitendeka. Hata kama hawajahusishwa moja kwa moja na hiyo report lakini pia hawakutimiza kazi zao vizuri, hivyo wangeondolewa ili waje watu wapya.

Mimi nina imani na prof. Ndullu, sina sababu za kumfikiria vibaya maana naona anatimiza majukumu yake vizuri toka aingie BOT.
 
Back
Top Bottom