BOT yapunguza riba ya mikopo kwa Bank za ndani,toka 16% mpaka 12%

Hiyo ni majaliwa, hatuna sheria inayolazimisha mabenki ya biashara kushusha au kupandisha riba. Wanaweza waka bana ili kujipa faida.
Mabadiliko inawezekana yasiwepo kabisa kwa kuwa hakuna sheria inayozibana benk zetu linapokuja swala la kuongeza au kupungunza riba...Hili punguzo sana sana litazisaidia benk kuchota mapesa mengi benki kuu
 
BOT haina hela ya kukopesha mabenk, ukisoma post namba 12 utaona kwamba mara nyingi hizi ni zile overnight transactions, au short term loans ambazo hata wiki hazizidi.

Na ikitokea benki ikashindwa kurejesha in time gharama inakuwa kubwa zaidi. Benki zitaendelea kukopa kwa wananchi kwa mfumo wa fixed deposits.

Nimekupata mkuu Raimundo.
 
Alichoongea mkuu jbmukulu ndo jibu sahihi.

Concept ya discounting rate iko hivi:

BOT anapotaka kukopa kutoka kwa makampuni (benki zikiwemo) anatangaza Treasury Bills au Treasury Bonds; sasa mfano akitaka kukopa Tshs 100,000,000/-, anaidiscount kwa 16%, maana yake wewe unayemkopesha utampa Tshs 84,000,000 (maana yake ameiondoa ile 16%) lakini yeye atakurudishia sh mil 100,000,000/- kwa hiyo kampuni itakayomkopesha inapata faida ya 16,000,000 + interests zinazochajiwa kila mwezi.

Sasa kwa kuipunguza kutoka 16% mpaka 12% maana yake ni kwamba BOT anawabana wanaomkopesha, badala ya kumpa 84,000,000/- sasa itabidi kampuni husika impe 88,000,000/-, discount ni 12,000,000/- badala ya ile 16,000,000/- ya awali.

Kwa maana hiyo basi, wanaomkopesha wanaumia zaidi sasa hivi kuliko awali.

NOTE: Hapo nimetumia hesabu rahisi, ila wao wana jinsi wanavyocalculate hayo makitu yao mpaka kufikia jibu sahihi, ila uhalisia ni huo kwamba kumkopesha BOT gharama zimeongezeka zaidi ya awali.

Nimeona paragraph ya pili kutoka mwisho wamezungumzia kuhusu Bank zitakazoenda kukopa BOT as last resort nazo kuna marekebisho.

cc barafu

Mkuu barafu nitaomba hii response yangu na ya jbmukulu uzipandishe juu ili kurekebisha uelewa wa nini tulichodhani ndicho kumbe sicho, naona watu wanaimwagia serikali sifa kwa kutoelewa nini ni nini hapo.
Nashukuru kama Niko sahihi!
 
WAo Benk wanakopa BOT wanamkopesha mtu wa kawaida, ni wazi kwamba nao pia watapunguza riba kwa wateja wao/
Ni bora umemsaidia mkuu make watanzania wengi ni wajuaji kumbe hata a, b, c hawana
 
Alichoongea mkuu jbmukulu ndo jibu sahihi.

Concept ya discounting rate iko hivi:

BOT anapotaka kukopa kutoka kwa makampuni (benki zikiwemo) anatangaza Treasury Bills au Treasury Bonds; sasa mfano akitaka kukopa Tshs 100,000,000/-, anaidiscount kwa 16%, maana yake wewe unayemkopesha utampa Tshs 84,000,000 (maana yake ameiondoa ile 16%) lakini yeye atakurudishia sh mil 100,000,000/- kwa hiyo kampuni itakayomkopesha inapata faida ya 16,000,000 + interests zinazochajiwa kila mwezi.

Sasa kwa kuipunguza kutoka 16% mpaka 12% maana yake ni kwamba BOT anawabana wanaomkopesha, badala ya kumpa 84,000,000/- sasa itabidi kampuni husika impe 88,000,000/-, discount ni 12,000,000/- badala ya ile 16,000,000/- ya awali.

Kwa maana hiyo basi, wanaomkopesha wanaumia zaidi sasa hivi kuliko awali.

NOTE: Hapo nimetumia hesabu rahisi, ila wao wana jinsi wanavyocalculate hayo makitu yao mpaka kufikia jibu sahihi, ila uhalisia ni huo kwamba kumkopesha BOT gharama zimeongezeka zaidi ya awali.

Nimeona paragraph ya pili kutoka mwisho wamezungumzia kuhusu Bank zitakazoenda kukopa BOT as last resort nazo kuna marekebisho.

cc barafu

Mkuu barafu nitaomba hii response yangu na ya jbmukulu uzipandishe juu ili kurekebisha uelewa wa nini tulichodhani ndicho kumbe sicho, naona watu wanaimwagia serikali sifa kwa kutoelewa nini ni nini hapo.
Cc Cookie
 
Mikopo ya benki hawacalculate kama unavyofanya. Wale wana calculation zao wanazijua wenyewe
Siyo wanazijua wenyewe. Ni hesabu za cummulative interest rate. Kwa mfano kama umekopa 10 m na riba ya benki ni 20%:
1. Mwisho wa mwaka wa kwanza rba ni 2 million yaani 20% of 10m. Hivyo utalipa 12 million.
2. Mwisho wa mwaka wa pili rba ni 20% ya 12 million siyo 10 million tena, jawabu lake liite x.
3. Hivyo hivyo mwaka unaofuata riba itakuwa 20% ya (12 +x). Jawabu lake liite y.
4. Mwaka utakaofuata riba itakuwa 20% ya (12+x) +y.

Endelea hivyo hivyo mwaka wa mwisho wa kulipa deni. Assumption hapa ni kuwa ulikuwa hupunguzi deni kipindi chote cha mkopo. Kama ulikuwa unarejesha kidogo kidogo capital itakayotozwa riba ni ile bakaa ya deni ya mwisho wa kila mwaka hivyo itakuwa ndogo kutegemea na kasi ya urejeshaji.

Ni hesabu rahisi tu hizi na zinafundishwa O level secondary school. Ninarudia tena wengi hukimbia hisabati na kwenda kusomea maubishi. Maubishi haya wao huyaita siasa.
 
Kuna kitu mtoa mada anachanganya kama sio Mimi, kuna tofauti kati ya discount rate na interest rate. Barua inaonesha kilichoshuka ni discount rate. Mfano nikiwa nakuuzia Gari 10m kwa discount ya 16% halafu baadae nikashusha discount kuwa 12% ni wapi utalipa hela nyingi?
Kwa uelewa wangu discount rate ikipungua Wewe mlipaji unalipa zaidi na discount rate ikipanda unalipa kidogo. Kwahiyo BOT walichofanya kitasababisha commercial banks wapandishe interest rates charged by them kwetu sisi wakopaji.
cc Cookie
 
Back
Top Bottom