barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Nimeona tangazo la BOT kushusha "interest Rate" kutoka 16% mpaka 12% kwa Bank za kibiashara zinapokuwa zinakopa kutoka Benki Kuu Ya Tanzania (BOT)
Punguzo hili litaanza mwezi March.Nachotaka kujua toka kwa wataalamu wa uchumi,punguzo hili lina athari gani chanya katika kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja,kaya na mpaka Taifa?
Na je,kushuka kwa "interest Rate" hiyo,inaweza kusababisha kushuka kwa "riba" ya mikopo ambayo wafanyabiashara ndogondogo ma wafanyakazi hukopa kupitia bank za kibiashara kama CRDB na NMB??
Maana kama wao wamepunguziwa huko wanakokopa,kwanini wasipunguze huku wanakokopwa?
[HASHTAG]#UchumiWaViwanda[/HASHTAG] [HASHTAG]#TzYaViwanda[/HASHTAG] [HASHTAG]#UchumiWaKati[/HASHTAG]
================================
Ufafanuzi kutoka kwa baadhi ya wadau

Kuna kitu mtoa mada anachanganya kama sio Mimi, kuna tofauti kati ya discount rate na interest rate.
Barua inaonesha kilichoshuka ni discount rate. Mfano nikiwa nakuuzia Gari 10m kwa discount ya 16% halafu baadae nikashusha discount kuwa 12% ni wapi utalipa hela nyingi?
Kwa uelewa wangu discount rate ikipungua Wewe mlipaji unalipa zaidi na discount rate ikipanda unalipa kidogo. Kwahiyo BOT walichofanya kitasababisha commercial banks wapandishe interest rates charged by them kwetu sisi wakopaji.
Alichoongea mkuu jbmukulu ndo jibu sahihi.
Concept ya discounting rate iko hivi:
BOT anapotaka kukopa kutoka kwa makampuni (benki zikiwemo) anatangaza Treasury Bills au Treasury Bonds; sasa mfano akitaka kukopa Tshs 100,000,000/-, anaidiscount kwa 16%, maana yake wewe unayemkopesha utampa Tshs 84,000,000 (maana yake ameiondoa ile 16%) lakini yeye atakurudishia sh mil 100,000,000/- kwa hiyo kampuni itakayomkopesha inapata faida ya 16,000,000 + interests zinazochajiwa kila mwezi.
Sasa kwa kuipunguza kutoka 16% mpaka 12% maana yake ni kwamba BOT anawabana wanaomkopesha, badala ya kumpa 84,000,000/- sasa itabidi kampuni husika impe 88,000,000/-, discount ni 12,000,000/- badala ya ile 16,000,000/- ya awali.
Kwa maana hiyo basi, wanaomkopesha wanaumia zaidi sasa hivi kuliko awali.
NOTE: Hapo nimetumia hesabu rahisi, ila wao wana jinsi wanavyocalculate hayo makitu yao mpaka kufikia jibu sahihi, ila uhalisia ni huo kwamba kumkopesha BOT gharama zimeongezeka zaidi ya awali.
Nimeona paragraph ya pili kutoka mwisho wamezungumzia kuhusu Bank zitakazoenda kukopa BOT as last resort nazo kuna marekebisho.
cc barafu
Mkuu barafu nitaomba hii response yangu na ya jbmukulu uzipandishe juu ili kurekebisha uelewa wa nini tulichodhani ndicho kumbe sicho, naona watu wanaimwagia serikali sifa kwa kutoelewa nini ni nini hapo.
Obvious,kama cost of fund kwa hizi benk zitapungua maana yake interest za mikopo watapunguza.
Lakin pia interest kwa savers nazo zitaenda down. Hapo inategemea na ishu ya liquidity kuwa bank inazipata vipi.
All in all it is a good indication to the economy on financial aspect.