BOT yapunguza riba ya mikopo kwa Bank za ndani,toka 16% mpaka 12%

Huwezi kujifunza kama unadhani unaelewa kila kitu.

Kila siku ya Mungu nnayoishi duniani nnaejifunza mapya mengi sana. Kumbuka hilo.

Hapa hakuna ubishoo, barua ya BOT iko wazi, Kingereza sijajifunza leo au kupitia kwako, lugha za ki cooperate nnazielewa kuliko unavyofikiria. Kumbuka na hilo.

UNA MENGI SANA YA KUJIFUNZA KUPITIA KWA FaizaFoxy wa JF.
 
Hii itachochea ukuwaji wa uchumi ukizingatia ribs za taasis nyingne za fedha zitapungua hvyo tunatarajia investment nying kuongezeka. Pia mfumuko wa bei utashuka sana hvyo kuleta unafuu kwa watu wa kipato kidogo.
Mkuu hakuna kulichopungua hapo ni ongezeko
 
mie ni banker ila sijaona bank zikikopa BOT mkopo wa BOT ni intraday unakopa na unarudisha siku hiyo hiyo ukishindwa unageuzwa lombard unapigwa penalty ya hatari kwa msingi huo bank hazikopi BOT kushuka kwa hii rate ndio standards industry rate ila kwa tanzania haina impact sana kwasababu bank zipo huru kujipangia interest zitakavyo

sema hii inaweza kuzisaidia bank kupata pesa zaidi kwasababu kuwekeza kwenye Treasury bill kutakuwa kuna return ndo 12 kuliko fixed deposit ambapo banks zinatoa mpaka 16 percent return for the same period

Sorry broda, what is a coupon rate for recently auctioned t-bills?

CC: raimundo for your clarification.
 
Sio Lazima nao wapunguze hakuna Sheria inaowataka kufanya hivyo eti Kwa kuwa nao wamepunguziwa
 
Ruttashobolwa SAMAHANI MKUU, HIYO NOTICE YA BoT UMEISOMA AU UMEHARAKIA TU KUCOMMENT?


NI KWAMBA BoT IMEPUNGUZA DISCOUNT RATE (KWENYE BIDHAA KAMA SIMU TUNGESEMA NI OFFER AU PUNGUZO); SASA HAPA KTK FEDHA BoT ILICHOKIFANYA NI KUPUNGUZA DISCOUNT KWA MABENKI YANAPOKOPWA FEDHA NA BoT.

HIVYO KAMA DISCOUNT RATE IMEPUNGUZWA MAANA YAKE HAYO MABENKI YATAPATA GAWIO AU FAIDA NDOGO KUTOKANA NA FEDHA WANAZOKOPWA.

KWA MSINGI HUO BASI, KAMA DISCOUNT RATE IMEPUNGUZWA MAANA YAKE NI KWAMBA RIBA INAWEZA KUONGEZEKA KWA WAFANYABIASHARA WATAKAOKOPA KTK HIZI BENKI ZA BIASHARA ILI MABENKI YAENDELEE KUPATA FAIDA KUBWA KAMA MWANZO. KIUFUPI MIKOPO INAWEZA KUGEUKA KUWA GHARI NA HATA KWA WALE WANAOWEKA FEDHA KTK FIXED ACCOUNT WATARAJIE UWEZEKANO WA KUPUNGUZWA GAWIO.
 
Back
Top Bottom