Bot Yajitoa Ktk Swala La Epa

Injinia

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
849
26
Jamani, gavana anajua nini tusichojua? Anatishiwa toka juu?
Wenye data...
 
mkuu labda tunashindwa kuchangia maana hatuoni data ktk post yako zaidi ya swali.
Nadhani ingelikuwa umeiedit heading ya thread ungeeleweka au la, leta data tujimwage. I mean leta wimbo na sisi tutakupatia chorus
 
BoT yajivua EPA

Shadrack Sagati


GAVANA wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema benki hiyo kwa sasa inataka kuachana na majukumu ambayo haikupewa kisheria, kuepusha shinikizo na vitanzi kwa watendaji wa benki hiyo.

Profesa Ndulu alitoa mfano wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kuwa siyo shughuli za benki hiyo kisheria, bali walikabidhiwa njiani. Alisema kwa sasa BoT imesimamisha shughuli za akaunti hiyo kusubiri tathmini kuona kama kuna umuhimu wa kuendelea nayo.

Alisema kazi mojawapo ya benki hiyo ni kulipa fedha za serikali hivyo ni vyema shughuli nyingine zinazohusiana na uhakiki wa madeni hayo zikafanywa na taasisi nyingine na siyo BoT. “Sisi tunataka tuletewe tu hundi hapa, kwamba lipa huyu na uhakiki ufanywe na taasisi nyingine.

Hiyo ya kulipa ndiyo kazi yetu kuliko kuanza kazi ya kutathmini deni lipi ni halali halafu baadaye tulipe, kwa kweli hiyo siyo shughuli yetu,” alisema Ndulu. Alisema benki hiyo ni kwa ajili ya serikali, hivyo inawajibika kufanya malipo inapoamriwa na serikali. “Iweje yale ambayo siyo lazima tuyafanye sisi tuendelee kuyafanya?” alihoji.

Profesa Ndulu aliainisha kazi za benki hiyo kisheria kuwa ni kudhibiti mfumuko wa bei, kuhakikisha malipo yako sawa sawa, benki ziko salama na kusaidia ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi. Alisema iwapo itashindwa kutekeleza shughuli hizo, basi ni vyema ikawajibika lakini siyo kutwishwa mizigo mingi ya utendaji.

“Kwa kweli tunataka tupunguze shughuli za BoT ili tuwajibike zaidi kwa shughuli zetu za kisheria,” alisema na kuongeza, “hizo shughuli nyingine tunanaswa vitanzi, siyo shughuli zetu…tunataka kufanya biashara zaidi siyo kwenye shughuli nyingine ambazo zina shinikizo kutoka nje,” alisema.

Akizungumzia hatua zinazofanywa na benki hiyo baada ya kashfa ya EPA, Profesa Ndulu alisema pamoja na kusimamisha akaunti ya EPA, pia maofisa waliohusika wamesimamishwa kazi wakati uchunguzi unafanyika. Hata hivyo, alikataa kutaja idadi ya maofisa waliosimamishwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu ya Ernst & Young ilifanya ukaguzi katika BoT kuhusu EPA na kugundua wizi wa Sh bilioni 133, hatua ambayo ilisababisha Rais Jakaya Kikwete kumfuta kazi Gavana wa BoT, Daudi Ballali, na kuagiza kurejeshwa kwa fedha hizo pamoja na kufikishwa mahakamani kwa wahusika wa kashfa hiyo.

Tayari timu ya uchunguzi inayowahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeweza kurejesha Sh bilioni 60 na inaendelea na kazi yake. Profesa Ndulu alisema BoT pia inafanya tathmini ya usimamizi wa fedha itakayoendeshwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuanzia Mei mwaka huu.

Alisema tathmini hiyo itasaidia kuifahamisha dunia iridhike kuhusu benki hiyo inavyosimamia fedha zake. Akizungumzia hali ya uchumi kwa ujumla, gavana alisema uchumi unakua kwa asilimia saba kwa mujibu wa takwimu mpya, huku pato la taifa likifia Sh trilioni 17.7 kwa mwaka. Aliitaja sekta ya kilimo kuwa inachangia asilimia 26 wakati sekta ya ujenzi inachangia asilimia 19, madini asilimia 17.

Kwa upande wa mfumuko wa bei, Profesa Ndulu alisema hadi kufikia Juni mwaka huu utakuwa umefikia asilimia 6.5. Alisema mfumuko huo unatokana na kupanda kwa bei ya mafuta, kupanda kwa bei ya chakula duniani, kutokuwapo kwa mvua za vuli, ongezeko la ujazi wa fedha na ongezeko la bei ya umeme.

Alipoulizwa kama Sh bilioni 133 zilizochotwa na mafisadi kutoka akaunti ya EPA ziliongeza mfumuko wa bei, gavana alisema ni kweli kuwa fedha hizo baada ya kutolewa Benki Kuu ziliongeza ujazi wa fedha ambao unachangia pia mfumuko wa bei.

Hata hivyo, alisema hadi tathmini ifanyike ndipo itakapoweza kuonekana kama fedha hizo zilichangia mfumuko wa bei. Alitoa mfano kuwa huenda baada ya fedha hizo kutoka zilipunguzwa baada ya serikali kuuza dhamana zake.

“Kwa hilo hadi tathmini ifanyike kwanza ndipo nitakuwa na jibu zuri,” alisema. Kuhusu mikopo inayotolewa na mabenki, Profesa Ndulu alisema benki hiyo imepunguza kiasi cha dhamana zinazoenda kwenye mnada ili kuweka ushindani zaidi kwa mabenki hayo, hali ambayo imesaidia kupunguza riba kutoka asilimia 17.7 hadi kufikia asilimia 7.5.

Alisema kutokana na hali hiyo, benki nazo zinatakiwa zipunguze riba ya mikopo ishuke kutoka asilimia 16 hadi 15. Pia alisema kwa walipaji wazuri wao wanatakiwa wapewe riba ya asilimia 10.5 ya mkopo. Thamani ya shilingi ilielezwa na gavana huyo kuwa imeendelea kuimarika.

“Tutaomba vyombo vya sheria vitusaidie katika hili, maana kuna taasisi nyingi zinaendelea kushinikiza watu walipe kwa dola, hili halitakubalika na iwapo tutalitekeleza litasaidia kuendelea kuimarisha thamani ya shilingi,” alisema.

Source: HabariLeo
 
mkuu labda tunashindwa kuchangia maana hatuoni data ktk post yako zaidi ya swali.
Nadhani ingelikuwa umeiedit heading ya thread ungeeleweka au la, leta data tujimwage. I mean leta wimbo na sisi tutakupatia chorus

wrnyb9.gif
 
Back
Top Bottom