BOT wanapaswa kuliangalia kwa makini suala la udhibiti uhaba wa USD/Dollars

clento

Member
Nov 2, 2010
14
30
Habari wadau,
Suala la udhibiti wa upatikanaji wa fedha za Kigeni limezidi kuwa changamoto kubwa. Hali ambayo imepelekea kuwa na black market kwenye rate za ajabu ajabu hasa kwa USD.

Hali hii inawapa shida sana wafanyabiashara. Wakati hili likitokea serikali yetu pendwa inatuambia kuna reserve ya kutosha ya USD. Ugumu unakuja ukitaka kufanya muamala wa USD. Muamala mdogo wa $4,000 mfano unaweza kuhangaika wiki nzima kuikusanya hiyo pesa usifanikiwe.

Nini kinatokea? Mabank ukienda wanakuambia hawana $ hata ukitaka kufanya transfer kutoka kwenye acc yako bado ni tatizo na mabank mengi yame impose restrictions ya limit ya kununua 200, 500 hadi 1,000 tu kwa siku.

Bureau hata ukiwa upo mstari mmoja na mtu anayeenda kuuza USD ukifika zamu yako ya kununua wanakuambia hatuna/hatuuzi kwa sasa.

Nadhani hawa ndio wanaowakusanyia hao wanaoziuza kwa black market kwa rate ya juu hadi 2700 kwa $ 1 ya Kimarekani.

Ushauri wangu BOT iangalie namna ya kufanya ziara kwenye bureau (anonymously) kuona hizo misconduct maana vimegeuka vituo vya kukusanyia USD ziende black market kwa ubaguzi wa kuuza.

Mabank yadhibitiwe na limit ya kununua iongezwe.

Kuna watoa huduma wanaotoza ankara zao kwa USD wanajipangia rate zao, mfano ICD's au bandari kavu wanatoza rate hadi 2620 tshs kwa 1$ ya kimarekani, kushindwa kudhibiti hili kwa BOT ni bomu la kudumu linaloendelea kutengenezwa.

Ankara nyingi kutozwa kwa USD kwa miamala ya ndani kitu ambacho BOT ingeweza kuregulate kuzuia mapapa wa biashara wanaotoza kwa USD watumie tshs kwa rate elekezi ya BOT ama commercial Banks.

Kwa maono yangu sioni tukijinasua kwenye hili na zaidi kuendelea kuwapa mwanya wa watu kufanya black market.

BOT mnahitajika kuchukua hatua za Haraka sana.
 
Back
Top Bottom