Hivi Dotto Biteko umeshindwa kabisa suala la umeme?

kibori nangai

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
1,089
1,381
Ndugu Dotto Mashaka Biteko

Najua utakuwa kanda hii ya Ziwa maana jana ulikuwa Bukoba kwa wakatoliki.

Nakuulizaa tuu umeshindwa kabisa hili swala la umeme
samia SULUHU HASSANI Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Wewe ulikuwa Serikalini

Dr. Medrard Kalemani alikuwa waziri kwenye serikali yenu na Mzalendo wa kweli JPM aliwezaje kutatua tatizo la umeme.

Uliingia madarakani ukamuweka Makamba tukapewa ngonjera kibao Leo oo maji oo sijui nini ,yeye na maharage, mbwembwe kibao na uswahili tuu.

Leo Biteko na slogan yake Watanzania wanataka umeme
Sijui hata kaishia wapi.

Narudia toka asubuhi hatuna umeme huku kanda yako mkoani kwako uko seriously kwelii Dotto Mashaka Bitekoo
Nakuulizaa Watanzania tumechokaa.

Hizo kura mnazotafutaaa huko mnapishana kama mabasi ya Shabiby line barabarani

Swala la umeme sio kipaumbele chenuu
 
Kwani mlivyomuona azim dewji anatoa takwimu za umeme hamkushtuka yeye alitoa takwimu kama nani kama sio tatizo la kutengenezwa lile watu wapige hela.
 
Yaani mvua zinanyesha alafu kuna mgao wa umeme kweli inafikirisha.Sema sababu kuu watawala wanauhakika kwamba vyovyote wafanyavyo watapita kwenye chaguzi,wamesha tuchukulia poa.
 
Back
Top Bottom