BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

Mbona kama account imekosewa? TL yuko Nairobi Aghakhan Hospital au Nairobi Hospital Association?
 
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo
BOT wanataka kujiaibisha kama Judge mkuu. Waache wanasiasa wanyukane wenyewe kwa wenyewe lakini ninamuamini Mbowe zaidi ya Ndugai ama Beno Ndulu.
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa

shule ni muhimu zaidi
 
BOT wanataka kujiaibisha kama Judge mkuu. Waache wanasiasa wanyukane wenyewe kwa wenyewe lakini ninamuamini Mbowe zaidi ya Ndugai ama Beno Ndulu.
kumbe Lisu mmemfanya kuwa jukwaa la siasa?
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
Kwa nini zichangwe tarehe 8 sept na zitumwe tarehe 20 sept 2017..??

Nini kimefanya hela zikae almost 12 days mikononi mwa Bunge..??

Nini kimefanya watoe maelezo ya kwamba wametuma baada ya Mbowe kuongea..??

BTW, sijaona mantiki ya BoT kutoa maelezo waliyoyatoa..
 
Serikali na baadhi ya wabunge ndiyo wanataka iwe hivyo. Wangelishughulikia mapema watu wasingechukulia kisiasa lakini wamewapa watu watumie mwanya wa kisiasa.
 
Source ya Habari husika tunaomba iwe inaandikwa juu ya uzi ili kutopoteza muda wa kusoma habari husika.
 
Familia ya Lissu ilishasema haitaki serikali imgharamie hawana Imani nayo, unataka serikali ifanyaje?

Watu mnasahau hizi pesa ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjulisha yeyote yule kuhusu hizi pesa. Kama hawajapendezwa vile zimekuwa handled warudishe

Pesa zimefika zikiwa kamili kwanini bado mnalialia yani mnampangia mtoaji msaada masharti? Sijawahi sikia hii. Wangeweza kutuma hata next month Kama wangetaka
CCM mna jeuri sana na fedha zetu walipa kodi
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
Kwenye swala la dharura huwezi kufuata mlologo.ndio maana hata hospital Kuna watu wa emergency case.wao walitegemea angeweza kuishi wiki 2 bila kitibiwa?hata malaria huwezi kaa 2 week
 
Kwenye swala la dharura huwezi kufuata mlologo.ndio maana hata hospital Kuna watu wa emergency case.wao walitegemea angeweza kuishi wiki 2 bila kitibiwa?hata malaria huwezi kaa 2 week

Kwa nini zichangwe tarehe 8 sept na zitumwe tarehe 20 sept 2017..??

Nini kimefanya hela zikae almost 12 days mikononi mwa Bunge..??

Nini kimefanya watoe maelezo ya kwamba wametuma baada ya Mbowe kuongea..??

BTW, sijaona mantiki ya BoT kutoa maelezo waliyoyatoa..

Ni mada kama hizi zinaonyesha uelewa wa TZ ulivyomdogo, watu kama nyie ambao mpo mitandaoni hamuelewi sijui wale waliopo Ileje bongo zao zina hali gani

TL hahitaji msaada kutibiwa, hadi familia yake inampeleka KE tayari walikau wameamua kumtibu wenyewe na walijua gharama zote ni juu yao, msaada umekuja kama bahati tu, bila hata ya huo mchango TL angetibiwa. Aidha walisema hawama imani na gov hivyo hawahitaji msaada wao

TL anabima ambayo inamsaidia pia

Wabunge kutoa michango yao ni msaada sio jukumu wala lazima, wabunge kwa hiari yao walikubali ila yeyote yule angeweza kusema posho yangu isikatwe na isingekatwa. Zile sio pesa zako wala zangu au za wananchi ni poshso za wabunge. Again, ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjibu yeyote yule kuhusu mchakato wa hizo pesa, wangeweza kupeleka hata mwezi ujao kama wangeamua. Mtoaji msaada ndo huwa anaaamua atoe kiasi gani na kwa mtindo gani sio mpokeaji, ndo nasikia hapa mpokeaji anatoa masharti. Kama hawajapendezwa na jinsi hizo pesa zimekuwa handled wanaweza kurudisha
 
Chadema wapuuzi sana Kuna mambo ambayo siyo yakulalamika tu Pesa zenyewe ni makusanyo ya nusu ya posho za wabunge YY chadema kazi yao kupokea.

Naona watu wanaongea mambo ya emergency emergency ni upuuzi tu.... Unadhan asingetibiwa? Sasa anapata tiba safi kabisa na yuko poa Watz tunachanga kila Siku mil 300 zishafika mbali na hyo 46mil...vitu vingine Chadema mnyamaze tu maana havina maana sana Kufanya kila kitu headline!

Mbowe kuna kipindi anaudhi sana...
 
Ni mada kama hizi zinaonyesha uelewa wa TZ ulivyomdogo, watu kama nyie ambao mpo mitandaoni hamuelewi sijui wale waliopo Ileje bongo zao zina hali gani

TL hahitaji msaada kutibiwa, hadi familia yake inampeleka KE tayari walikau wameamua kumtibu wenyewe na walijua gharama zote ni juu yao, msaada umekuja kama bahati tu, bila hata ya huo mchango TL angetibiwa. Aidha walisema hawama imani na gov hivyo hawahitaji msaada wao

TL anabima ambayo inamsaidia pia

Wabunge kutoa michango yao ni msaada sio jukumu wala lazima, wabunge kwa hiari yao walikubali ila yeyote yule angeweza kusema posho yangu isikatwe na isingekatwa. Zile sio pesa zako wala zangu au za wananchi ni poshso za wabunge. Again, ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjibu yeyote yule kuhusu mchakato wa hizo pesa, wangeweza kupeleka hata mwezi ujao kama wangeamua. Mtoaji msaada ndo huwa anaaamua atoe kiasi gani na kwa mtindo gani sio mpokeaji, ndo nasikia hapa mpokeaji anatoa masharti. Kama hawajapendezwa na jinsi hizo pesa zimekuwa handled wanaweza kurudisha
Aiseee....
Hakuna aliyesema kuchanga ni jukumu la mtu, ILA UKISEMA UNACHANGA, NA UKACHANGA, MCHANGISHAJI AKILA, HILO NI TATIZO....

BTW, are you serious unaposema HATA WANGEPELEKA MWEZI UJAO? Kwa hali ile ya LISU... wapeleke mwezi ujao.... ROHO YAKO INAHITAJI REHEMA YA MUNGU ILI UONE MAANA YA ULICHOKIANDIKA
 
Ni mada kama hizi zinaonyesha uelewa wa TZ ulivyomdogo, watu kama nyie ambao mpo mitandaoni hamuelewi sijui wale waliopo Ileje bongo zao zina hali gani

TL hahitaji msaada kutibiwa, hadi familia yake inampeleka KE tayari walikau wameamua kumtibu wenyewe na walijua gharama zote ni juu yao, msaada umekuja kama bahati tu, bila hata ya huo mchango TL angetibiwa. Aidha walisema hawama imani na gov hivyo hawahitaji msaada wao

TL anabima ambayo inamsaidia pia

Wabunge kutoa michango yao ni msaada sio jukumu wala lazima, wabunge kwa hiari yao walikubali ila yeyote yule angeweza kusema posho yangu isikatwe na isingekatwa. Zile sio pesa zako wala zangu au za wananchi ni poshso za wabunge. Again, ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjibu yeyote yule kuhusu mchakato wa hizo pesa, wangeweza kupeleka hata mwezi ujao kama wangeamua. Mtoaji msaada ndo huwa anaaamua atoe kiasi gani na kwa mtindo gani sio mpokeaji, ndo nasikia hapa mpokeaji anatoa masharti. Kama hawajapendezwa na jinsi hizo pesa zimekuwa handled wanaweza kurudisha
Aiseee....
Hakuna aliyesema kuchanga ni jukumu la mtu, ILA UKISEMA UNACHANGA, NA UKACHANGA, MCHANGISHAJI AKILA, HILO NI TATIZO....

BTW, are you serious unaposema HATA WANGEPELEKA MWEZI UJAO? Kwa hali ile ya LISU... wapeleke mwezi ujao.... ROHO YAKO INAHITAJI REHEMA YA MUNGU ILI UONE MAANA YA ULICHOKIANDIKA
 
Familia ya Lissu ilishasema haitaki serikali imgharamie hawana Imani nayo, unataka serikali ifanyaje?

Watu mnasahau hizi pesa ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjulisha yeyote yule kuhusu hizi pesa. Kama hawajapendezwa vile zimekuwa handled warudishe

Pesa zimefika zikiwa kamili kwanini bado mnalialia yani mnampangia mtoaji msaada masharti? Sijawahi sikia hii. Wangeweza kutuma hata next month Kama wangetaka
Nakupa pole, uko nchi gani wewe ?? kama upo tz baas nakupa pole tena
 
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo

Hiyo BoT imeingiliaje kati hili jambo?

Mbona ni kama maelezo toka ndani ya bunge lemyewe ambayo in actual sense bunge lenyewe lilishatolewa maelezo??
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa

Jibu jepesi haswa wiring money 08/09/2017 to 22 September alaa acha hizo janja nyepesi hiyo. Na atajulia wapi wakati yeye hela kaanza kushika ukubwani kama wewe? kitu cha emergency mnaleta uwiring?
 
Back
Top Bottom