BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

Pesa za serekali sio za duka kwa duka. Jamani lazima kuweko Na nchanzo. Zamani sana nilipokuwa nafanya kazi serekalini. Ata kama kikosi au sec walikuweko kwenye ajali Fulani. Lazima mkuu wa kulikundi kuandika barua kujulisha Na kuomba chochote kile ata kama wakuu walikuwepo. So Mbowe kama kiongozi wa upinzani anatakiwa kuripoti kwa SPK Na kumpa taarifa huu ya ajali au ugonjwa wa Lissu. Huu ndio utaratibu wa kiserekali. Ata kama Rais angekuwepo. Mbowe andike barua kwa SPK. Na SPK atandika serekalini, kurejea barua ya Mbowe..m Hili CIG atakapokuja kuchunguza azijmkute nk........

Una hakika hizo ni hela za serikali?
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
Walimtaarifu kuhusu muamala huo? Kwa nini hata hospitali haikutaarifiwa? Na kwa nini toka 8/9 hadi 22/9 WHY
Msilaumu watu ombeni radhi.
 
So "as many as five days" is two weeks for you? Did you really grasp what you quoted?
It actually took 24hrs only, money was wired on 20th and received on 21st. All I know toka tar8 hadi 20 zilikua bado hazijatumwa
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
unalipa basing on the bill presented to you, sasa wewe una deposit tu hela
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
toka tarehe 8 mpaka 20 huoni hilo figisu, kwa nn wasimjulishe mbowe au mwanafamilia wa Lisu kabla ya kudodosha hiyo hela? ndio maana wazir anataka maombi ya kumtibu lisu yapelekwe kwake, hivi yule aliyechora nembo ya taifa NGOSHA alipeleka maombi kwa waziri ili apate matibabu muhimbili ? jiulize kama una akili timamu.
 
Mhmmm tangu tarehe 07 Sep hadi 23 Sept. kweli kwa ufanisi uliotukuka wa Bank kuu yetu nawapa 200% na kongole juu mkuu.
 
Walimtaarifu kuhusu muamala huo? Kwa nini hata hospitali haikutaarifiwa? Na kwa nini toka 8/9 hadi 22/9 WHY
Msilaumu watu ombeni radhi.
First, huu ni msaada. Msaada hauna masharti tena mtoaji ndo anaweza weka masharti sio mpokeaji

Second, familia ya Lissu ilijua gharama zote ni juu yao, msaada umekuja Kama bahati tu, bila hata ya huo msaada bado wao walishaamua atatibiwa Kenya na gharama zote ni zao

Bunge halina wajibu wakumtaarifu yeyote yule, Hili sio jukumu ni msaada Kama hawapendzwi nao warudishe, kwanza walisema hawataki serikali imgharamie

Pesa zimechangwa, zimetumwa timilifu I don't know what is all the fuss about au ndo Mtoto yatima haishi malalamiko

I wish TL a speedy recovery
 
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo
Uandishi wa makinikia!
 
It actually took 24hrs only, money was wired on 20th and received on 21st. All I know toka tar8 hadi 20 zilikua bado hazijatumwa

Isnt that the point of contention as to wahy it took 12 days to send the wire?
 
toka tarehe 8 mpaka 20 huoni hilo figisu, kwa nn wasimjulishe mbowe au mwanafamilia wa Lisu kabla ya kudodosha hiyo hela? ndio maana wazir anataka maombi ya kumtibu lisu yapelekwe kwake, hivi yule aliyechora nembo ya taifa NGOSHA alipeleka maombi kwa waziri ili apate matibabu muhimbili ? jiulize kama una akili timamu.
Familia ya Lissu ilishasema haitaki serikali imgharamie hawana Imani nayo, unataka serikali ifanyaje?

Watu mnasahau hizi pesa ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjulisha yeyote yule kuhusu hizi pesa. Kama hawajapendezwa vile zimekuwa handled warudishe

Pesa zimefika zikiwa kamili kwanini bado mnalialia yani mnampangia mtoaji msaada masharti? Sijawahi sikia hii. Wangeweza kutuma hata next month Kama wangetaka
 
Kwa vile lengo la Spika na Ofisi yake ni ovu na lililenga tu maslahi ya kisiasa na sio kutimiza wajibu wao, mpaka sasa hawajajua kuwa hawawezi kwa namna yoyote kujivua lawama na makosa, wangekuwa na chembe ya akili na uungwana wangeomba radhi tu. Walikuwa wapi wasitume fedha hizo toka tarehe 8 mpaka 20 September 2017??

Lakini kwa vile wanapenda hadaaa nilihisi watakimbilia kuitaka BOT itoe taarifa za muamala ule (Bank swift transcript) na wamefanya hivyo. Je sasa tukipewa taarifa za CBK (Central Bank of Kenya) zikionyesha siku na muda wa kuingia huo muamala upande wa pili watasemaje tena??

Kadiri wanavyojitutumua kwenye hilo shimo la uovu, unafiki na roho mbaya walilojichimbia ndivyo wanavyozidi kuzama!!

"The harder they come the harder they fall"
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
Since zimechangwa tayari mpk kutumwa how long zimechukua may be!?

Anza zilichangwa lini!?

Na zimetumwa lini!?

Sio walifanya baada ya kusikia kuna press conference ya mbowe
 
Acha ujuaji wa kipuuzi wakati hujui kitu, si ajabu bado unakula na kulala kwa shemeji yako afu unakuja hapa kubwabwaja kuhusu money wiring. Soma hapa

"Many domestic wire transfers can be completed within 24 hours (especially if transfers occur between accounts at the same financial institution). But international wire transfers may take longer. If you're sending money to another country, it may take as many as five days for the recipient to receive their funds"

Hii ni TZ to KE (BOT to Barclays)
Hata sielewi unachotetea ni nini. Kama ni 5 days int.trans, kuna siku 5 ngapi kati ya tarehe uchangishaji ulipokamilika hadi kutumwa, tarehe 8 - 20/09? Damu ya mtu haijawahi muacha mtu salama.
 
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo
Waandishi wa kitanzania ni pasua kichwa seduce me..yaan heading na kicho ndani hata haviendani tutakia washika mkia kwa kila kitu tz si soka si uchumi si taaluma..
 
PLATFORM imepatikana sasa...........
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom