BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

BoT yaingilia kati sakata pesa za Lissu

Yaani wewe umekaa hapo unadhani unaitetea serikali ua unazidisha tu chuki kwa watu
Nani alikuambia Lisu aliomba fedha toka bunge au serikali?
Fedha iliyochangwa kwa akili yako unadhani ni hela ya bunge au bunge alikuwa mchangishaji? Wapo wapumbavu wachache wanaodhani kuwa fedha ile ilikuwa ni ya bunge,lakini tunajua kuwa fedha ile ni michango binafsi ya wabunhe akiwemo lisu mqenyewe, kwa hiyo haihusiani chochote na mashariti ya kifedha ya bunge au serikali.
Fedha ya mashariti ama misaada ya serikali/Bunge tumewaambia hatuitaki kaeni nayo tutachangishana.
Tunajua wapi taifa mmelifikisha kwenye ukaburu,kodi zetu zinatumika kikaburu nk nk
Watanzania tumesusa nyinyi mnachekelea kana kwamba mmepiga bingo, la muhimu Sir God amewakatalia kusudio lenu,kazi tuliyoibakiza ni ndogo sana kuli tutokako hela ya masimango na vimbulu kama nyie kaeni nayo.
Kumbe unajua ni michango binafsi sasa kwanini mnalialia kwanini zimechelewa kutumwa. Sio pesa za umma zile, bunge lingeweza kuamua hata litume mwakani maana ni zao na hawawajibiki kwa yeyote kuhusu ule msaada. Ni posho zao.

Mkichanga pesa zenu mnakila sababu na haki ya kuuliza shingapi, lini na nani katumiwa ila mtu mwingine akichanga huna haki ya kuuliza kuhusu mchango wake.
 
Katika hili sakata namkumbuka ndugu Mrisho Gambo na kauli ya Makamu wa Raisi
 
Bot imeingilia kati nini sasa?
Itakuwa kuna foleni c wajua apo kenya boti zakuvuka na pesa ni chacheeeee.
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo
 
Kumbe unajua ni michango binafsi sasa kwanini mnalialia kwanini zimechelewa kutumwa. Sio pesa za umma zile, bunge lingeweza kuamua hata litume mwakani maana ni zao na hawawajibiki kwa yeyote kuhusu ule msaada. Ni posho zao.

Mkichanga pesa zenu mnakila sababu na haki ya kuuliza shingapi, lini na nani katumiwa ila mtu mwingine akichanga huna haki ya kuuliza kuhusu mchango wake.
Ukitoa za wapinzani za wana ccm zinabaki ngapi? Wangetoa za wapinzani wakazituma haraka kwani walijua umuhimu wa kuzituma haraka mkabaki nyie wenye mashaka yenu. Hata hivyo richa ya hizo za pamoja wabunge wa upinzani walichanga zingine zaidi ya milioni 60 na zikafika kwa wakati.sisi watanzania sio watoto kama mnavyodhani tunajua kwa nini!
Tambueni roho za sasa kwa wana ccm sio wote sio roho za kitanzania ni za kishetani tu, badilikeni tunawapenda rudini kwenye utanzania mmepotea.
 
Hela hazikutumwa hizo ni Sana'a tuu kwenda Kenya hapo viswahili Vinci mno ambapo haya kwa basis zingefika siku hivyo hiyo kama mngetumia njia ya kizamani maana kwa hela za Kenya ni milioni mbili na laki moja tuu..hao BOT wajibu kwa mini fedha inashuka thamani kila kukicha waachane na hela za matibabu hizo..
 
Kiufupi, bunge na serikali imeumbuka katika hili suala la TAL. Michango tunaendelea kuchanga kwa hiari na mgonjwa kakataa pesa zenu why kujikomba? Mlishakataa endeleeni kukataa. Juzi nimeuza mbuzi wangu wawili wenye mimba kwa shs 150,000 na kutuma shs 120,000. Najisikia niuze hata ng'ombe wangu mmoja.
 
Ajali tarehe 8 pesa imekusanywa trehe 9 hizo pesa zimetumwa tarehe 20!! Naona zinaanzishw nyuzi kibao za utetezi. Mbona zinatumika nguvu nyingi kwenye jambo hili?
Nani kakuambia pesa ilichangwa tarehe 8???? Acheni kuandika mawazo yenu hapa. Ahadi ya michango ilitolewa tarehe 8. Usiseme pesa ilichangwa tarehe 8. Kuahidi na kuchanga ni vitu viwili tofauti
 
Kwa hizo wiki 2 toka pesa zichangwe zilikuwa zinafanyiwa nini?
 
WAKATI Ofi si ya Bunge ikisisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge kiasi cha Sh milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), tayari zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeingilia kati.

Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mkoani Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetumwa kupitia BoT.

Taarifa hiyo ilisema kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo wakati fedha hizo zikitumwa ilikuwa ni sawa na Shilingi za Kenya 1,977,120.58. Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kilitumwa siku ya Septemba 20, mwaka huu kwenda Benki ya Barclays, tawi la Hurlringham, kwenye akaunti namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.

Taarifa hiyo iliambatanisha barua yenye kumbukumbu, Ref.NO FA.93/155/01B/260 kutoka kwa Meneja wa Akaunti za Nje wa BoT inayothibitisha benki hiyo kutuma fedha hizo kwa akaunti hiyo ya hospitali anakotibiwa Lissu. Ofisi hiyo ya Bunge imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, kulitupia lawama Bunge na hasa akielekeza tuhuma zake kwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kuwa wabunge wamekatwa posho kuchangia gharama za matibabu ya Lissu, lakini fedha zilizopatikana hazikuwa zimekabidhiwa.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimjibu Mbowe na kumtaka aache kupotosha taarifa za ushiriki wa Bunge katika tiba ya Lissu na kulichukuliwa suala hilo kisiasa. Alifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Bunge au ofisi inayotumia bima, iwapo inataka mgonjwa wake kuhamishiwa hospitali nyingine, lazima itoe taarifa ya daktari inayoelezea kuhamishwa kwa mgonjwa huyo.

Aidha, Ndugai alimtaka Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kukubali ofa ya serikali ya kutaka kugharamia tiba za Lissu akiwa nje ya nchi. Kwa sasa matibabu ya Lissu yanatokana na michango ya wadau mbalimbali ambapo kwa mujibu wa Mbowe hadi juzi jumla ya Sh milioni 204 zilikusanywa ambazo hata hivyo alibainisha kuwa hazitoshi na michango inaendelea. Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai, hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika na kwamba aliweza kuzungumza naye kwa kutumia simu ya kiganjani na kuwashukuru Watanzania kwa sala na michango yao.

CHANZO: Habari Leo
 
Mbowe hajui kwamba wiring money takes time up to days sometimes? Businessman gani hajui hilo? Sio kila kitu wafanye siasa
shughulikia yanayokuhu wachangiaji wako kimya kama unataka kuchangia a/c imeshawekwa wazi 01J1080100600 POROJO haziwezi kumtibu TL WACHENI MANENO wekeni hela kwenye hiyo A/C.we
unayejua kuhusu wiring money ni faida kwako kujua hilo
 
Nimejibu hili swali repeatedly ngoja nirudie kwa mara ya mwisho

TL hahitaji msaada kutibiwa, hadi familia yake inampeleka KE tayari walikau wameamua kumtibu wenyewe na walijua gharama zote ni juu yao, msaada umekuja kama bahati tu, bila hata ya huo mchango TL angetibiwa. Aidha walisema hawama imani na gov hivyo hawahitaji msaada wao

TL anabima ambayo inamsaidia pia

Wabunge kutoa michango yao ni msaada sio jukumu wala lazima, wabunge kwa hiari yao walikubali ila yeyote yule angeweza kusema posho yangu isikatwe na isingekatwa. Zile sio pesa zako wala zangu au za wananchi ni posho za wabunge. Again, ni msaada sio jukumu, bunge halina wajibu wa kumjibu yeyote yule kuhusu mchakato wa hizo pesa, wangeweza kupeleka hata mwezi ujao kama wangeamua. Mtoaji msaada ndo huwa anaaamua atoe kiasi gani na kwa mtindo gani sio mpokeaji, ndo nasikia hapa mpokeaji anatoa masharti. Kama hawajapendezwa na jinsi hizo pesa zimekuwa handled wanaweza kurudisha

Hatujauliza hela zilikuwa za lazima au laaa no swala ni hiyo kujifanya wiring............ na kuuliza Mbowe hajui maana ya wiring. usiwe mwepesi kujibu as if umeulizwa utarudi na mkate jioni no kumbuka unaongea na watu tofauti..... wiring my feet.
 
Tunajua wiring inafanya kazi kwa 24 hours only sasa nyie toka tarehe 8 mpaka 23 na bado mnaguts za kutetea upumbavu basi tusiwalaumu wasaliti wanaoturudisha nyuma kwa kujilimbikizia Mali,wizi mfano Kivuko Kibovu,madini na gas.

Pole Tanzania yangu
Kama unafatilia kwa makini . kuna taarifa ilitolewa na bunge baada ya kukusanywa pesa hizo akapigiwa Simu Mh.Mbowe aelekeze pesa hizo zitumwe wapi yeye akaeleza kwamba Zitumwe kwenye account ya CRDB inayotangazwa kuchangia Hapo nadhani Bunge likaingia ukakasi kidogo maana account hiyo ilionekana ni Mbunge so baada ya kutafakari Hayo wakampigia tena Mh.mbowe kumueleza kwamba hawawezi kutuma kwenye hiyo account wa naomba watume moja Kwa moja hospital ndio Mh. Mbowe akawarumia hiyo account wakatuma so kwa uelewa wangu nadhani hiyo dilayment ilitokea hapo ktk kujiridhisha zaidi.[emoji120]
 
Kwani hiyo account walitumiwa tarehe 20??Hivi account ni ya Chadema Bunge hawaiamini wataweza kumuamini tena Mbowe alipowapa account ya hospitali??

Alichofanya Ndugai na Management ya Bunge kinaakisi kutokuwepo kwa huruma na ubinadamu.Wakati Mbunge mwenzao anaumwa unaanza kuulizia wapi kutumia account ya hospitali??Michango ya TLS imefika kabla ya Wabunge wakati ya TLS ilichangwa baadaye sana.Hii haileti picha nzuri,wala usiutetee upuuzi wa Ndugai an management ya Bunge
 
Back
Top Bottom