BoT Saga Unfolding: Ballali ni Kafara

Shomile:
Mbona unalidhalilisha jina lako bwana!
Wewe ni 'Nsomile' halafu unatuwekea habari kama mtu ambaye hakwenda shule?

Kichwa cha habari ulivyokiweka hakiendani kabisa na habari uliyoitoa. Kwa mfano, ni vyanzo vipi vya uchunguzi; na huku unatuwekea udaku wa mtu aliyepewa mtaji aanzishe biashara?

Ni nani aliyefanya 'uchunguzi' unaouzungumzia na kwa sabau zipi?
Kwa nini huyomwenye kutoa hizo habari asimpeleke huyo mchunguzi wa habari kwa chanzo chenyewe halisi, yaani kwa Balali mwenyewe ili apate nafasi ya kujisafisha jina lake na kuwasuta wabaya wake waliomtakia kifo.

Kwa ujumla, umeifanya habari iwe ya udaku zaidi jinsi ulivyoileta, hata kama ndani yake kuna hata chembe ndogo ya ukweli.

Halafu, mbona umeibandika mara mbili hapa hapa kwenye jamvi la siasa?
 
Mimi sisemi habari hizi ni za uongo zote kwa sababu
Mafia wote Duniani mambo yakiwazidia wanaua na mara nyingi wanapenda kuua kwa Sumu ili usife karibu nao kuogopa ushahidi.

Kumbukeni ile ya KGB kule UK.

Kam kawa ya SISIEMU jamaa alipewa sumu kifuko kimejaa kwa tabia ya kupunja waliyo nayo SISIEMU akaamua kumpunja Dozi mlengwa. Matokeo yake Mzee tunAye mpaka leo.

Wakati mwingine usione wanmwua ili Mgao wake wagawane wao.

Zamani zile niliwahi kusoma kitabu cha series za JAMES HADLAY CHASE.

What is better than Money? ....LIFE.
 
Quote:-

All this is a very far cry from Mr. Balali's humble beginnings. The Governor was one of the first Tanzanians to win a scholarship to study in the United States, where he studied at Harvard, after making his first trip by boat across the Atlantic Ocean.

This is something, huyu mkuu nina wasi wasi kuwa kuna mengi anayajua maana mtu mwenye elimu nzito hivi hawezi kufanya mambo kijinga jinga tu, apone ajitokeze aweke mambo sawa!

Swali la nje kidogo. Hivi huyu mzee alikuwa na Doctorate au alikuwa na Masters tu? Nauliza hivi kwa sababu pale BOT alikokuwa akiongoza hawam-address kama Dr. Ballali, bali wanasema Mr. Balali wakati kwa Rashid wanasema Dr. Rashid na kwa huyu mpya wanasema Prof Ndulu.
 
Zalendohalisi,
Kuna mengi ya ukweli ambayo ukiyasikia yanaonekana vigumu kuaminika. Sometimes truth is more stranger than fiction.
 
Wazee karibu wote waliofanya kazi kubwa katika mashirika mengi makubwa ya umma Tanzania wanajua kuwa mwaka wa uchaguzi lazima waje watu wa CCM/Ikulu kuchota hela. Hii ni siri iliyo wazi.

Muda umefika chama/ serikali kujiondoa katika mambo ya kuchota pesa na kuingilia utendaji.

Hii ya BOT kuna hela ilichukuliwa na CCM kwenye uchaguzi na nyingine ilichukuliwa na "wazee".
 
Jasusi,
Nakubaliana nawe, ila kwangu mimi hii habari ilivyoelezwa na "Nshomile" haina kichwa wala mkia.

Kama mimi ningekuwa Balali, siwezi kukubali kupewa sumu na watu tuliokula nao yamini au walioniacha kwenye mataa na nikakubali kufa na tai shingoni na hali wao wnadunda .. NO WAY. Lakini kama ulivyosema, mengine hayaeleweki!
 
Zalendohalisi,
Unachosema ni kweli. Tuvute subira. Time will tell.Kama nilivyosema awali kwingineko, tumwombe Mwenyezi Mungu amlinde mgonjwa apone.
 
Wazee karibu wote waliofanya kazi kubwa katika mashirika mengi makubwa ya umma Tanzania wanajua kuwa mwaka wa uchaguzi lazima waje watu wa CCM/Ikulu kuchota hela. Hii ni siri iliyo wazi.

Muda umefika chama/ serikali kujiondoa katika mambo ya kuchota pesa na kuingilia utendaji.

Hii ya BOT kuna hela ilichukuliwa na CCM kwenye uchaguzi na nyingine ilichukuliwa na "wazee".

Point nzuri hii. Wakati wa uchaguzi CCM wanakuwa kama hawana akili nzuri na sijuhi kawa walishawahi kuwa na akili nzuri.

Rafiki yangu alikuwa anafanya kazi tumbaku Morogoro na Mwekezaji alihamua kuwapa bonasi wafanyakazi wake kwa kazi nzuri.

Mzungu wa watu wakati anaanda kulipa bonus akaletewa invoice ya CCM kumtaka achangie uchaguzi. Alichokifanya ni kuchukua bonasi ya wafanyakazi wake na kuwapa CCM katika shughuli za siasa.

Tukirudi kwenye mada hivi matatizo ya BOT yametokea katika kipindi cha JK akiwa madarakani au matatizo ya muda mrefu?
 
Kama yatakuwa yametokea ndani ya miaka miwili ya utawala wa JK itakuwa imevunja rekodi.
Nadhani ambacho tunatakiwa tujue je huu ubadhirifu umetokea wakati wa kipindi cha Balali ofisini au naye aliukuta?
 
Habari za weekend wana JF.
Habari za kuaminika kutokana na mtu ambaye yuko karibu na balali na anaishi hapa US zinasema kuwa mzee huyo alipewa sumu huko Tanzania. Pmoja na utata uliopo juu ya ugonjwa wake ambayo ni kweli anaweza kuwa amukwa ugonjwa mkuu, lakini kwa hali hasa iliyomleta hosptali hapa US ni kwasababu washikaji zake mbao wako serikalini baada ya kusikia soo linakuwa gumu walitaka kummaliza maana wanajua angetoa siri. Watu wenyewe ni viongozi wetu ambao kwa ujumla wanhusishwa moja kwa moja na scandal ya BOT (Usisahau akina Lowassa kwa kuanzia) Sasa baada ya huyu mze kuumwa Tumbo sana, Dr. wake akamshari huyu mzee akimbizwe hapa US. nNgoma hiyo inasemekana alichanganyiwa somewhere huko bongo, lakini yule aliyepewa hiyo kazi ya kuchanganta sumu hakuweka dose yote ndio maana balali ameshinda kifo na ha kwa kuwahishwa kufanyiwa surgery ya tumbo kusafisha tumbo lake. Ugonjwa wake ulikuwa ni siri mno hasa baada ya kugundulika kuwa alipea sumu na wabongo. Huyu mzee ana siri za watu wengi akiwemo Rais wetu. Na hawa wote ni washikaji ake walikula pamoja.
Sasa kwa taarifa ni kwamba balali yuko hotelini ni hoteli ndogo sana ambayo haina misifa ndio maana watu wameshindwa kumjua yuko wapi. Mwanafamilia huyu aliendelea kusema kuwa Mzee huyu ni vigumu kurudi Tanzania kwani ameshajiweka sawa hapa. na huo mkwala wa Kikwete kutengua cheo chake amefanya hivyo akijua kabisa jamaa hatarudi.
Kwa hiyo ndugu zangu suala la BOT, bado ni kitendawili na kumbe kuwa viongozi wa juu sana huko TZ walishirikiana naye na ndio hao walitaka kummmaliza ili asiwataje. Na kwa hali ilivyo huneda asiwe na mda wa kuwataja. Habari kamaili ni kwamba surgery yake ilienda vizuri na yuko hotelini kwa mapumziko na anafatilia habari za ukaribu.
Mwanafamilia huyu anaendesha biashara yake nzuri tu hapa US na mtaji alipewa na Balali.

Najua kwenye hii forum wapo madaktari wa binadamu pia, hebu tusaidieni. Hivi ni sumu gani hiyo ambayo mtu akilishwa inabidi atibiwe kwa operesheni? Hata ile Polonium-210 aliyolishwa kachero Litvinenko wa Urusi haikumpasa kufanyiwa operesheni, au madaktari walikosea? Sisi wengine huko vijijini mtu akinywa sumu huwa tunamtapisha kwa kutumia mayai mabichi au majani ya mti fulani wenye harufu mbaya, na wanapona bila operesheni. Kwa hiyo Nshomile unatuambia Balali alipewa sumu, ambayo matibabu yake ni kufanyiwa operesheni? Au walimwagia asidi huko tumboni (sijui walipitisha wapi!) kama alivyomwagiwa Saeed Kubenea machoni?

Mawazo yangu, ambayo nitayafuta yatakapothibitishwa kuwa sivyo ni kwamba Balali haumwi chochote, amejichimbia sehemu anakula nchi, hadi hapo hali itakapokuwa shwari ndipo arejee mtaani. Na ninatabiri kuwa ataandika kitabu kuhusu hili sakata ambacho kitakuwa bestseller.
 
Shomile:
Mbona unalidhalilisha jina lako bwana!
Wewe ni 'Nsomile' halafu unatuwekea habari kama mtu ambaye hakwenda shule?

Kichwa cha habari ulivyokiweka hakiendani kabisa na habari uliyoitoa. Kwa mfano, ni vyanzo vipi vya uchunguzi; na huku unatuwekea udaku wa mtu aliyepewa mtaji aanzishe biashara?

Ni nani aliyefanya 'uchunguzi' unaouzungumzia na kwa sabau zipi?
Kwa nini huyomwenye kutoa hizo habari asimpeleke huyo mchunguzi wa habari kwa chanzo chenyewe halisi, yaani kwa Balali mwenyewe ili apate nafasi ya kujisafisha jina lake na kuwasuta wabaya wake waliomtakia kifo.

Kwa ujumla, umeifanya habari iwe ya udaku zaidi jinsi ulivyoileta, hata kama ndani yake kuna hata chembe ndogo ya ukweli.

Halafu, mbona umeibandika mara mbili hapa hapa kwenye jamvi la siasa?

TEH TEH TEH TEH
Mbona wewe unaanza mambo ya ubaguzi wa kikabila ,mambo gani tena haya ndugu yangu ??? haya ni mambo ya wana nigeria wakikutana tu cha kwanza je wewe ni IBO??

Kwa vile una utata wa majina haya ngoja nikuelezee kidogo ili siku nyingine usipate changanya mambo hii ni kwa faida yako na kwa kutumia advantage hiyo utapata elewa asili yangu ila mimi kabila langu ni MTANZANIA

SHOMILE ni watani wetu na kwa bahati nzuri jina hilo wote tunalitumia kwa maana ile ile yani CHIEF ila kinachotofautisha ni phonetic na jinsi linavyoandikwa

shomile wao wanaandika hivi hili jina OMUKAMA ama MUKAMA
Wajita wanaindika hivi MKAMA .Angalia hizo tofauti.
Harafu kingine unauhakika gani kama nimenda shule??
 
mafisadi mafisadi mpaka inafikia point unaanza kuamini mtu mweusi ana less IQ,report yamepewa lakini sitashangaa wakishindwa prosecution na kuishia majungu kama haya tunayoongelea hapa
 
[/B]

TEH TEH TEH TEH
Mbona wewe unaanza mambo ya ubaguzi wa kikabila ,mambo gani tena haya ndugu yangu ??? haya ni mambo ya wana nigeria wakikutana tu cha kwanza je wewe ni IBO??

Kwa vile una utata wa majina haya ngoja nikuelezee kidogo ili siku nyingine usipate changanya mambo hii ni kwa faida yako na kwa kutumia advantage hiyo utapata elewa asili yangu ila mimi kabila langu ni MTANZANIA

SHOMILE ni watani wetu na kwa bahati nzuri jina hilo wote tunalitumia kwa maana ile ile yani CHIEF ila kinachotofautisha ni phonetic na jinsi linavyoandikwa

shomile wao wanaandika hivi hili jina OMUKAMA ama MUKAMA
Wajita wanaindika hivi MKAMA .Angalia hizo tofauti.
Harafu kingine unauhakika gani kama nimenda shule??

Mkamap au Nshomile?:

Nina hakika kuwa Nshomile ameenda shule kwa vile tafsiri ya jina lake ni 'Nimesoma' na sina sababu yoyote ya kunifanya niamini kuwa anatumia jina hilo kama utani tu! Inajulikana hivyo nchi nzima kutokana na baadhi ya wananchi wa mkoa fulani kujitangaza hivyo. Sielewi dhana ya ubaguzi wa kikabila wewe umeitoa wapi, kwani hakuna nilipoionyesha katika maandishi niliyoyabandika.

Mkamap, unazidi kutuchanganya unapotumia majina mengi humu JF. Kuna sababu zipi za mhimu zinazokufanya mara uwe Mkamap, mara uwe Nshomile? Hii tabia itatufanya tusiamini hata hayo mambo ya mhimu ya 'uchunguzi' unayotuwekea hapa.
 
Wan JF.
Msipoamini habari nilizoandika kuhusu poision aliopewa huyu bwana balali hiyo ni shauri yenu. Lakini ukweli uko pale pale na ndio hicho kilichotokea.Aliyenipa hizi habari ni mwanafamilia wa Balali na unajua tena hawezi wenda indeep more that that maana naye hajui kama mimi nilikuwa namchota ili nilete habari au la! Lakini kwa kuwa ninaishi hapa na nimejiahidi kuyasaka yale nayoweza kuyapata kutoka kwa ndugu wa balali aliyeko hapo. Lakini tatizo la JF kuna ka-tabi ka kudhalilishana. Ukiniuliza maswali eti kwa nini hawakumpa maziwa mara baada ya kugundua amepewa sumu...sasa mimi unataka nikujibu nini. Ninachojua ni kwamba hiyo sumu iliharibu sehemu za utumbo wako kama nilivyoeleza ndio maana akafanyiwa operashion. Tuwe tunaheshimu mchango wa mawazo ya wenzetu kuliko kukandia na kuingiza ukabila kwa waota habari kama baadhi ya memmbers hapa mlivyonishambulia. Ukweli utakuja julikana na mimi naamini nilichokisema kitaibuka kuwa cha kweli na hakuna yeyote hapa atakayekubali kwamba nilishakisema. Mimi nitaendelea kudondosha habari kila nitakavyozipata.
"BALALI YUKO KWENYEHOTEL NDOGO YA MTAANI NA SI RAHISI KUMPATA KWASABABU HOTEL HIYO SI POPULAR SANA" hayo ni kati ya niliyoyataja kwenye thread yangu ya awali na yametoka kwa huyo mwanafamilia wake. Tuache ubishi usio na sababu bali tudadisi.
 
Basi, ndugu yangu Nshomile, tukushukuru kwa kurudi kwako na kuitetea hoja ya Balali kulishwa sumu. Hilo linawezekana, hatukatai. Endelea kudodosa hiyo 'source' yako ili tupate mengi zaidi yatakayoweza kutusaidia kufumbua kitendawili hiki walichotutega wakubwa. Binafsi siamini kamwe kuwa Balali ndie mwizi pekee katika ufisadi huu, na ni yeye pekee ndiye mwenye uwezo akitaka, wa kumwaga kila kitu kiwe wazi, na pengine kusafisha jina lake.

Kuhusu sumu kuharibu utumbo bila kumuua, inawezekana kabisa, na hili halitegemei ni kiasi gani cha sumu aliyolishwa, ila aina na uwezo wa sumu hiyo kuingia kwenye damu na kusambazwa kwenye viungo vya mwili vinavyodhurika zaidi na haraka na madhara ya hiyo sumu.

Nshomile, kama unayotuambia hapa yana ukweli wowote, basi wewe ni miongoni mwa watu wachache sana hapa walio na 'contacts' hata kama ni za mbali na huyu binaadam. Tunakutakia mafanikio mema.
 
Kalamu AM sorry
unajua hii thread amechanganya thread mbili yangu na ya Nshomile sasa ulipojibu mie sikwenda dipu kufahamu kulikoni,
maana mie niliadhisha thread hii kumbe na Nshomile naye kaanzisha hii harafu wakazichanganya.

Sasa nilidhani dongo umenigeia mie kwa kuhusisha jina Mkama na shomile ila hapa inabidi nikubali NIMEKURUPUKA KUJIBU Am sorry once again

Nshomile na Mkamap ni watu wawili tofauti na wala hawafahamiani nahisi Nshomile yupo US wakati Mkamap yupo mashariki ya mbali .Samahani mkubwa
 
Swali la nje kidogo. Hivi huyu mzee alikuwa na Doctorate au alikuwa na Masters tu? Nauliza hivi kwa sababu pale BOT alikokuwa akiongoza hawam-address kama Dr. Ballali, bali wanasema Mr. Balali wakati kwa Rashid wanasema Dr. Rashid na kwa huyu mpya wanasema Prof Ndulu.

balali anayo phd..kuna makala moja nimepata kusoma..inamtaja balali kama moja ya reliable eminent economist waajiriwa wa IMF..ambapo yeye akiwa na wenzake wanne walitumwa na world bank kwenda kusaidia reform policy zilizoifanya MALAYSIA kuwa tiger asia leo hii....na pia kwenye jarida hilo alitaja mikakati ambayo inaweza kuipaisha nchi kama tanzania kama ikifuatwa....sijui kwa nini watanzania wanaoheshimika nje wanashindwa kuwa msaada nyumbani..may be tuna wa misuse..

kuhusu phd alisema kule IMF hawapendi kujiita dr..simply kwa sababu karibu wote wenye ngazi ya juu na wa kati wengi ni phd holder...kwa hiyo wanaamua kurahisisha ..la kila mtu angeitwa dr..dr...ikumbukwe kuwa balali aliazimwa na mkapa toka IMF akaaza kwa kumshauri kidogo alipoingia 1995 kabla hajampa ugavana...kutokana na familia yake kuwa newyork aliishi new africa hotel kwa karibu mwaka mmoja,kabla ya kuhamia kwenye nyumba yake na baadaye kidogo kumuoa ms muganda..baada ya kuwa amemdivorce mkewe ulaya...ON SECONDMENT...nadhani ajira yake kule bado ipo...pamoja na huu wizi uliotokea mwishoni mwa mwaka 2005...sera za kiuchumi za balali walizokuwa wakimshauri mkapa pamoja na yule raia wa ghana ..zilifanikiwa..kwa kiasi fulani...

kwa reference ya gazeti la mtanzania daima...ndugu yake aliyehojiwa anasema balali ameandikisha maelezo ya anachojua yeye kuhusu ufisadi..akitaka kusafisha jina lake kwa kuonekana a sole player..na imeelezwa kuwa hii kashfa chanzo chake ni watu wazito zaidi yake..maelezo yamehifadhiwa kwa wakili asiyejulikana..na kuna ndugu zake wameshapewa maelezo kuwa if anything happens kabla hajaweza kuyatoa mwenyewe ..basi yatolewe for public consumption.....
 
Dr. ni kitu kidogo sana nashangaa huku nyumbani bongo inakuwa deal sana. Hawa ma-Dr. ndio mafisadi nambari moja, tena wanataka waogopwe. Mimi naona ma-Dr. wote Valuta waende kwenye nyanja zao wakaendeleze huko na wawaachie wanasiasa nyanja yao.
 
Swali langu lilikuwa ni kutaka kuelewa tu backgorund yake na wala halikuwa linalenga kupima chochote juu ya uwezo wake. PM kajibu swali langu pale pale nilipokuwa natafuta kuhusu huyu bwana; niliwahi kusoma somewhere kuwa alikuwa instrumental sana katika kukuza uchumi wa nchi za Asia.
 
PM,
Yule Mghana unayemsema ni Dr. Kwaku. Kwa sasa ameamua kuishi Dar. Nshomile, nimekuvulia kofia. Habari ulizozipata kwa ndugu zake Balali zinashabihiana na zile nilizosikia mimi. Kuna taarifa kuwa baada ya kula chakula na mheshimiwa mmoja, gavana alianza kutapika aliporudi nyumbani, na siku hiyo hiyo alikuwa anaondoka kwenda Marekani. The rest ni kama ulivyoelezea. Kuna wanaosema kuwa kule kutapika kulisaidia sana ama sivyo leo tungekuwa tunasema lugha tofauti. But I am glad this info is slowly coming out.
 
Back
Top Bottom