BoT Saga Unfolding: Ballali ni Kafara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BoT Saga Unfolding: Ballali ni Kafara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Jan 12, 2008.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kutokana na usiri uliopa wa ungonjwa wake na hosptali anayouguzia
  mie nashawishika kusema Balali ni mzima wa afya njema


  Dk. Slaa: Nina siri nyingine nzito

  na Peter Nyanje


  WAKATI Watanzania wakitafakari hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali kutokana na kashfa ya akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), muasisi wa tuhuma zilizosababisha uchunguzi wa akaunti hiyo, Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na siri nyingine kuhusu tuhuma za ufisadi wa viongozi walio serikalini.

  Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi, Dk. Slaa alisema kuwa anayo majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao walishiriki kuhujumu fedha za nchi kupitia kampuni nyingine kubwa zaidi ya zile zilizotajwa katika ripoti ya Ernst & Young iliyochunguza akaunti ya EPA.

  “Nimesikiliza kilichotangazwa, kwanza si ripoti ya uchunguzi wa Ernst & Young kama tulivyoambiwa. Tunachotaka waitoe ripoti nzima kama walivyoahidi.

  “Walichokitangaza ni kitu kidogo sana katika ripoti hiyo. Wameficha wanayotaka kuficha na kutangaza wanayotaka kutangaza… haya mambo ni makubwa sana na wameamua kutangaza madogo madogo na kuacha yake makubwa,” alisema Dk. Slaa.

  Aliliambia gazeti hili kuwa, ingawa serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa hadharani ripoti hiyo ya uchunguzi, yeye anayo majina na kampuni kubwa zilizofanya ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.

  Pamoja na majina ya kampuni hizo, Dk. Slaa alilithibitishia gazeti hili kuwa, anayo pia majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao wanahusika katika kampuni hizo.

  “Wao si wametaja kampuni 22, zile ni za watu wadogo sana, hata ukichunguza utagundua kuwa ni za watu wadogo. Kuna kampuni kubwa za watu wakubwa zimefichwa… Tunataka watueleze kuhusu Deep Green, Meremeta na Tangold, huko ndiko kwenye vigogo,” alisisitiza Dk. Slaa.

  Alisema kuwa anayafahamu mambo hayo, iwapo serikali isipotoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ernst & Young, yeye atayataja majina ya viongozi hao, kampuni wanazohusika nazo na tuhuma zinazowakabili.

  Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alifichua kwa gazeti hili kuwa, taarifa alizozitumia kuibua ufisadi huo alizipata pia kutoka kwa maofisa waandamizi kutoka katika idara nyeti ndani ya serikali, ambao wana uchungu na ufisadi wa kutisha unaofanywa ndani ya asasi za umma.

  “Huwa tunafanya utafiti, tunasoma na kuperuzi kwenye mitandao. Ndio maana ukiwa pale bungeni utaona kuwa ofisi ya kambi ya upinzani inafanya kazi mpaka saa 8:00 usiku, tunatafuta vitu kama hivi.

  “Lakini baada ya kuweka wazi majina ya mafisadi katika mkutano wa hadhara pale Mwembe Yanga mwezi Septemba, Watanzania wengine wenye uchungu na nchi yao, wenye dhamira hai na wanaipenda nchi yao, wakiwemo watumishi wa idara nyeti za serikali, walituletea taarifa nyingi.

  “Si kwamba walikuwa wanavujisha siri, hizi si siri, ni ufisadi, kwa hiyo hawabanwi na ile sheria ya siri za serikali… kiongozi huwezi kuwa mwizi serikalini halafu mtu akatoa taarifa hizo, na wewe ukamshitaki eti ametoa siri za serikali,” alifafamua.

  Dk. Sla alisema kuwa taarifa nyingine alizipata kwenye mtandao wa intaneti, na kusema hilo limekuwa ni pigo kwa serikali lililotokana na matendo yake yenyewe.

  Akifafanua, alisema kuwa wakati sheria ya kuruhusu ushahidi kutoka kwenye mtandao ilipoletwa bungeni, yeye aliipinga, lakini kutokana na uwingi wao, wabunge wa CCM waliipitisha.

  “Leo hii sheria hiyo hiyo inahalalisha madai tunayoyatoa na nadhani wanaona ubaya wa walichokipitisha,” alisema.

  Kuhusu ripoti ya Ernst & Young, Dk. Slaa alisema kuwa wataendelea kudai itolewe hadharani kwa sababu serikali yenyewe iliahidi kuianika.

  Alisema madai yao hayo yatalenga kuwawezesha Watanzania kufahamu kila kitu kilichomo kwenye ripoti hiyo, kwani hatua ya rais kutengua uteuzi wa gavana ni nzito na inathibitisha kuwa kuna kasoro nyingi zilizobainika.

  “Rais na serikali si wamiliki wa rasilimali za nchi. Wanapewa dhamana ya kuongoza, si waamuzi wa mwisho, wanatakiwa kuwajibika kwa Watanzania ambao ndio wanaotakiwa kuwa na uamuzi wa mwisho,” alisema.

  Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alisisitiza kuwa, kuondoka kwa Balali nchini, ilikuwa ni njama mahsusi zilizopangwa ili kuficha baadhi ya mambo.

  “Nina taarifa za uhakika nilizozipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa serikali kuwa, Balali alishauriwa aondoke baada ya sisi kufichua ufisadi ili asitoe siri. Nitataja ni nani aliniambia wakati muafaka utakapofika,” alisema.

  Alipoulizwa iwapo hana wasiwasi na maisha yake kutokana na mambo yanayotokea hivi sasa, Dk. Slaa alisema kuwa yeye alishayavulia maji nguo na ni lazima ayaoge.

  “Ninafanya hivi kutekeleza wajibu wangu kama mwakilishi wa wananchi, wao ndio mawakili wangu, na hivi sasa nimekuwa nikifanya mikutano ya hadhara na kuwaambia siri zote ninazozifahamu ili hata kama kitatokea kitu chochote wananchi wajue ni nini nilikuwa nacho,” alisema.

  source freemedia.co.tz yani tz daima
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alisisitiza kuwa, kuondoka kwa Balali nchini, ilikuwa ni njama mahsusi zilizopangwa ili kuficha baadhi ya mambo.

  Huu ndio ukweli wenyewe na hapa aifa hili litauwawa na hawa watu wanafiki kiasi cha kutisha .

  hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe na kila boriti litaondolewa kwenye huo mlolongo wa kuifilisi hii nchi yetu tukufu.

  Hapa nawatahadharisha sana hao wanaompa Kikwete kuwa amefanya mapinduzi waache mara moja kwani kuna siku watakuja kujuta sana na kujiona kuwa ni wajinga wa mwisho .

  JF tusikubali kujiingiza kwenye mkenge wa kupongeza kuwa JK kafanya kitu cha maana kumbe ni kiiini macho tuu kwa taifa la wadanganyika hawa.
   
 3. RR

  RR JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Balali kuchukua bil 133, bila backup ni kitu kisichowezekana. Balali ni msomi anayeelewa kwamba kungekua na ukaguzi wa hesabu. Hawezi kukwapua bila kuhakikishiwa protection... naamini kwa dhati aliagizwa kuchukua fedha hizo.. then kuzideliver mahali fulani.
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Si mumeona hata hapa kuna watu wanamjua Ballali kwa karibu lakini hakuna anayeweza kusema yuko wapi. Hii ni jambo la ajabu kabisa.

  Itabidi tumtafute Ballali mpaka tumpate, wakishindwa kumrudisha basi wananchi tumtafute.

  Nafikiri kama Watanzania tunaruhusiwa hata kumfungulia mashitaka huko huko USA. Tunaweza kuchanga hata dola mia mia ili jamaa afunguliwe mashitaka. Tukipata hiyo report tu basi ni ushahidi tosha.
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  Jan 12, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145

  Wanatuambia eti watasema yuko wapi wakati ukifika, ni wakati gani huo, kama nasi hatuendelezi ubabaishaji huohuo wa akina JK?
   
 6. M

  Mwendapole Old JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2008
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 249
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda tungefahamishwa tu, yuko hai au amekufa?
   
 7. d

  davykol New Member

  #7
  Jan 12, 2008
  Joined: Dec 20, 2006
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata jina la Hospitali hakuna. Nahisi kuna jambo tusubiri tuone.
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Au kuna picha linachezwa nini??

  Yani watasema jamaa kafariki na linazikwa maiti ya mtu mwingine wakati yeye yupo mzimaaaa anakandamiza ugali swafiiiiiii

  Harafu ikitokea mtu mmoja akikutana naye live wanasema oo ni miujiza bwana jamaa nimekutana naye kimiujizaa wakati jamaa alishafariki siku nyingiiiiiiiii
  Teh teh teh teh teh teh teh teh teh kiding
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwendapole,

  Kwi kwi kwi!!! unanifurahisha kweli. Ballali angelikufa JK na CCM yake wangefanya sherehe.

  Jamaa mzima tu na anafaidi mabilioni aliyochota. Akiamua kutolewa kafara, atakuwa mjinga kweli kweli. Inabidi awataje tu wote akina Mkapa na kundi lake.

  Jamaa ameukata kweli, maana kapumzishwa USA, tena hotelini, wakati ndugu yetu Mwafongo, kapumzishwa migombani ili ale ndizi na makatapera.
   
 10. K

  Keil JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Akina nani?
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Amefichwa US ili asitoe siri- hiyo kuugua ni geresha tu! Kwa nini augue baada ya tuhuma hizi kuibuka?
   
 12. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hivi, ni kweli kuwa Daudi ni raia wa US? plz anayejua amwage news hapa
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Jan 13, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli Balali ni Mtanzania? Isiwe kuwa jamaa huyu ni mmarekani mwenye asili ya Kitanzania. Je kuna mwenye taarifa kamili kuhusu uraia wake?

   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Quote:-

  All this is a very far cry from Mr. Balali’s humble beginnings. The Governor was one of the first Tanzanians to win a scholarship to study in the United States, where he studied at Harvard, after making his first trip by boat across the Atlantic Ocean.

  This is something, huyu mkuu nina wasi wasi kuwa kuna mengi anayajua maana mtu mwenye elimu nzito hivi hawezi kufanya mambo kijinga jinga tu, apone ajitokeze aweke mambo sawa!
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Dr. Ballali katolewa kafara, kafara kweli...

  Muda aliobakiza hapa duniani hauna maana tena...

  Maisha ya huko Marekani bila marafiki wake wa WB au ma associate wake wote aliofanya nao kazi hayatakuwa ya maana tena.

  Jina lake ambalo lilikuwa na sifa za kupendeza hivi sasa ni jina lililotapakaa matope.

  Ni matope ya kujipaka mwenyewe. Angeweza kabisa kuyasema yote yaliyomo moyoni na yaliyotokea BOT kabla ya 'mission' ya kumfukuza kutolewa kwenye vyombo vya habari.

  Hivi sasa wote aliofanya nao kazi huko majuu wanamjua yeye kama ni mwizi.

  Credibility yake kama doctor katika nyanja yake haina maana tena.

  Hawezi kwenda kwenye vikao au kuhudhuria function fulani hivi bila kunyoshewa kidole na kusemwa yule ndiyo mwizi wa mabilioni ya Tanzania.

  Raha iko wapi katika hii kafara? Je ni kafara aliyo jua inakuja au wenzake wamemgeuka dakika za mwisho?

  Ameyataka mwenyewe? kwanini hakwenda kwenye vyombo vya habari na kuwa wahi (wajanja wenzake) kabla ya report kutolewa?

  Angalia Media za kimataifa zilivyomsema, hapa chini. Je udaktari wake na utu wake una maana tena?

  Yaliyo andikwa kwenye vyombo vya habari, Kutoka :Bloomberg.com
  Kutoka: Fin24.co.za
  Kutoka: BBC.co.uk
  Kutoka: Yahoo.com

  Kutoka: VoA News.

  Kutoka: Portifolio.com

  Kutoka: Forextv.com
  Kutoka:Netnewspublisher.com
  Kifupi, dunia nzima inajua kuwa kuna deal zimefanyika bongo na mtu mmoja anayeitwa Dr. Ballali amehusika kinamna moja au nyingine kulipotezea Taifa mabilioni ya pesa, pesa ambazo nyingi zinatokana na misaada.

  SteveD.
   
 16. N

  Nshomile Member

  #16
  Jan 13, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za weekend wana JF.
  Habari za kuaminika kutokana na mtu ambaye yuko karibu na balali na anaishi hapa US zinasema kuwa mzee huyo alipewa sumu huko Tanzania. Pmoja na utata uliopo juu ya ugonjwa wake ambayo ni kweli anaweza kuwa amukwa ugonjwa mkuu, lakini kwa hali hasa iliyomleta hosptali hapa US ni kwasababu washikaji zake mbao wako serikalini baada ya kusikia soo linakuwa gumu walitaka kummaliza maana wanajua angetoa siri. Watu wenyewe ni viongozi wetu ambao kwa ujumla wanhusishwa moja kwa moja na scandal ya BOT (Usisahau akina Lowassa kwa kuanzia) Sasa baada ya huyu mze kuumwa Tumbo sana, Dr. wake akamshari huyu mzee akimbizwe hapa US. nNgoma hiyo inasemekana alichanganyiwa somewhere huko bongo, lakini yule aliyepewa hiyo kazi ya kuchanganta sumu hakuweka dose yote ndio maana balali ameshinda kifo na ha kwa kuwahishwa kufanyiwa surgery ya tumbo kusafisha tumbo lake. Ugonjwa wake ulikuwa ni siri mno hasa baada ya kugundulika kuwa alipea sumu na wabongo. Huyu mzee ana siri za watu wengi akiwemo Rais wetu. Na hawa wote ni washikaji ake walikula pamoja.
  Sasa kwa taarifa ni kwamba balali yuko hotelini ni hoteli ndogo sana ambayo haina misifa ndio maana watu wameshindwa kumjua yuko wapi. Mwanafamilia huyu aliendelea kusema kuwa Mzee huyu ni vigumu kurudi Tanzania kwani ameshajiweka sawa hapa. na huo mkwala wa Kikwete kutengua cheo chake amefanya hivyo akijua kabisa jamaa hatarudi.
  Kwa hiyo ndugu zangu suala la BOT, bado ni kitendawili na kumbe kuwa viongozi wa juu sana huko TZ walishirikiana naye na ndio hao walitaka kummmaliza ili asiwataje. Na kwa hali ilivyo huneda asiwe na mda wa kuwataja. Habari kamaili ni kwamba surgery yake ilienda vizuri na yuko hotelini kwa mapumziko na anafatilia habari za ukaribu.
  Mwanafamilia huyu anaendesha biashara yake nzuri tu hapa US na mtaji alipewa na Balali.
   
 17. N

  Nshomile Member

  #17
  Jan 13, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za weekend wana JF.
  Habari za kuaminika kutokana na mtu ambaye yuko karibu na balali na anaishi hapa US zinasema kuwa mzee huyo alipewa sumu huko Tanzania. Pmoja na utata uliopo juu ya ugonjwa wake ambayo ni kweli anaweza kuwa amukwa ugonjwa mkuu, lakini kwa hali hasa iliyomleta hosptali hapa US ni kwasababu washikaji zake mbao wako serikalini baada ya kusikia soo linakuwa gumu walitaka kummaliza maana wanajua angetoa siri. Watu wenyewe ni viongozi wetu ambao kwa ujumla wanhusishwa moja kwa moja na scandal ya BOT (Usisahau akina Lowassa kwa kuanzia) Sasa baada ya huyu mze kuumwa Tumbo sana, Dr. wake akamshari huyu mzee akimbizwe hapa US. nNgoma hiyo inasemekana alichanganyiwa somewhere huko bongo, lakini yule aliyepewa hiyo kazi ya kuchanganta sumu hakuweka dose yote ndio maana balali ameshinda kifo na ha kwa kuwahishwa kufanyiwa surgery ya tumbo kusafisha tumbo lake. Ugonjwa wake ulikuwa ni siri mno hasa baada ya kugundulika kuwa alipea sumu na wabongo. Huyu mzee ana siri za watu wengi akiwemo Rais wetu. Na hawa wote ni washikaji ake walikula pamoja.
  Sasa kwa taarifa ni kwamba balali yuko hotelini ni hoteli ndogo sana ambayo haina misifa ndio maana watu wameshindwa kumjua yuko wapi. Mwanafamilia huyu aliendelea kusema kuwa Mzee huyu ni vigumu kurudi Tanzania kwani ameshajiweka sawa hapa. na huo mkwala wa Kikwete kutengua cheo chake amefanya hivyo akijua kabisa jamaa hatarudi.
  Kwa hiyo ndugu zangu suala la BOT, bado ni kitendawili na kumbe kuwa viongozi wa juu sana huko TZ walishirikiana naye na ndio hao walitaka kummmaliza ili asiwataje. Na kwa hali ilivyo huneda asiwe na mda wa kuwataja. Habari kamaili ni kwamba surgery yake ilienda vizuri na yuko hotelini kwa mapumziko na anafatilia habari za ukaribu.
  Mwanafamilia huyu anaendesha biashara yake nzuri tu hapa US na mtaji alipewa na Balali.
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Say Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?
   
 19. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  duh habari nzito...ngoja niangalie NE Pats kwanza.
   
 20. Zalendohalisi

  Zalendohalisi Senior Member

  #20
  Jan 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ama kweli wabongo tunajua kuzua umbea. Hiyo lugha yenyewe haileweki! Balali amaeondoka bongo almost six months ago. Sasa baada ya kuenguliwa rasmi ndipo siri inatolewa kuwa over six months ago alipewa sumu Tanzania. Na alayeleta habari hizo ni aliyepewa mtaji na Balali. Tena huyu ndugu yake Balali anajua kuwa Balali anazo siri za wengi tu hata rais wetu aliyemfukuza kazi.

  Kama mimi ni Balali na ninajua nimepewa sumu na wale ninaowafichia siri; je nitanyamaza na kufa na hizo siri? Unless mimi ni mshiriki wa hizo siri, na kama ni hivyo then nitakufa kiume bila kuwa msaliti; na kwa hivyo ulalamishi wa kupewa sumu ni irrelevant.

  Na bado tutasikia mengi mwaka huu ili mradi wakubwa have been caught with pants down!

  Jaguars 7
  Patriots 0
   
Loading...