BoT: Kutunzana fedha katika sherehe kufuate kanuni

BoT: Kutunzana fedha katika sherehe kufuate kanuni

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,602
Reaction score
22,707
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imewataka watanzania wanaopeana zawadi kwa njia ya kutunzana pesa taslimu katika sherehe mbalimbali nchini, waelekeze utaratibu huo kwa njia mifumo ya malipo ya kidijitali.

Hayo yamesemwa leo, Agosti 4, 2026 na Ofisa Mwandamizi (BoT) Fredriki Mwakuu, alipokuwa akifanya mahojiano na NipasheDigital, mkoani Dodoma.

Mwakuu amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika malengo ya kupunguza matumizi ya pesa taslimu.

“Tunaona sasa hivi watu mbalimbali hususani akinamama wana tabia za kutunzana katika sherehe na kupelekea pesa kumwagika chini, ile haiko sawa BoT tumejipanga kuandaa mwongozo maalum kuhusiana na hilo,” amefafanua

Mchambuzi Mwandamizi Mifumo ya Malipo ya Taifa (BOT) Doto Namkaa, amesema mifumo ya malipo imegawanyika katika malipo makubwa na madogo bila kujali matumiaji awe na akaunti yoyote kutoka benki.

Nipashe
 
Hii mifumo ya kijiditali adui yake mkubwa ni makato. Nikitaka kutuma pesa kutoka NMB kwenda M-PESA ili nifanye malipo kwa lipa namba makato yake si rafiki kwa hiyo nachofanya nikwenda ATM kutoa cash.
Naona serikali bado haina nia thabiti ya kutufanya wananchi tutumie mifumo ya kidijitali
 
Hii mifumo ya kijiditali adui yake mkubwa ni makato. Nikitaka kutuma pesa kutoka NMB kwenda M-PESA ili nifanye malipo kwa lipa namba makato yake si rafiki kwa hiyo nachofanya nikwenda ATM kutoa cash.
Naona serikali bado haina nia thabiti ya kutufanya wananchi tutumie mifumo ya kidijitali
Hayo makato ndio wanayataka
 
hilo bado sana, siyo tu Bot, bali Afrika nzima, Afrika na usimamizi bora wa sheria ni 0+0
Nadhani tungejikita na matatizo ya Tanzania na si Afrika maana Mwalimu JK Nyerere alijikita na matatizo ya Afrika ambayo leo hayana faida kwa Watanzania..
BOT hawajawahi kutoa tamko kuhusu taarifa ya CAG ambayo kuna upotevu mkubwa wa fedha wao wapo busy na hela za kutunzana kwenye harusi..
 
Kuna maswala mengi mno muhimu ya kuyaaddress kama mikopo nafuu kwa vijana graduates na sio pesa za maharusini .
Wewe jamaa upo sawa sana sema ukiingiza siasa ndio tatizo mambo mengi nakuona upo vizuri.
 
Back
Top Bottom