BoT kuanzisha mfumo wa Crypto Currency

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,766
21,763
Benki Kuu ya Tanzania imetoa taarifa ya muelekeo wa kuanzisha mfumo wa pesa za kidigitali Yani Crypto Currency. Fedha hizo zitatolewa tu na benki Kuu na sio chanzo kingine.

Benki Kuu tayari imeshakaa na mabenki yote Tanzania na kuangalia namna Bora ya kuendesha mfumo wa fedha hizo. Fedha hizo zitafahamika Kama Central Bank Digital Currency.

Na Fedha hizo zitakuwa halali kutumika kwenye soko na ni benki kuu pekee ndio yenye ruhusa na mamlaka ya kutoa fedha hizo.

Hivyo tuchangamkie fursa ya crypto currency nchini Tanzania.
 
mfumo wa pesa za kidigitali Yani Crypto Currency.
Hivyo tuchangamkie fursa ya crypto currency nchini Tanzania.
Hizi ni kauli tatanishi.

Maelezo yalipaswa kuishia kwenye Central Bank Digital Currency (CBDC) tu.

Hilo neno crypto currency futa, halina mantiki hapo, maana taarifa inakuwa ya uongo.
=
Je unafahamu tofauti ya Cryptocurrency na CBDC?
=

"Cryptocurrency is a decentralized digital currency that uses cryptography for security, and is not controlled by any government or institution.

While CBDC is a digital version of a country's fiat currency, issued and backed by the country's central bank, intended to coexist with cash and bank deposits and to be used for various transactions, such as paying bills and making purchases."
 
Benki Kuu ya Tanzania imetoa taarifa ya muelekeo wa kuanzisha mfumo wa pesa za kidigitali Yani Crypto Currency. Fedha hizo zitatolewa tu na benki Kuu na sio chanzo kingine...
Asante hatua nzuri

Bado swala la Kuruhusu PayPal watanzania kuruhusiwa kupokea pesa kwa biashara za mtandaoni kupitia PayPal wakiuza kitu mtandaoni

Nasisitiza kupokea sio kulipa.Kulipa kwa PayPal Tanzania kunaruhusiwa.Kupokea hapana kwa nini? Kwa nini kulipa kupitia PayPal ruksa lakini kupokea hapana?

Waruhusu na kupokea
 
Hizi ni kauli tatanishi.

Maelezo yalipaswa kuishia kwenye Central Bank Digital Currency (CBDC) tu...

Mimi sijajitungia mkuu, taarifa imeonesha wazi Ni CBDC na wakonesha kwenye ufafanuzi crypto currency
 
Asante hatua nzuri

Bado swala la Kuruhusu PayPal watanzania kuruhusiwa kupokea pesa kwa biashara za mtandaoni kupitia PayPal wakiuza kitu mtandaoni...

Kweli mkuu inabidi waruhusu vyote viwili. Kulipa na kupokea.
 
Mimi sijajitungia mkuu, taarifa imeonesha wazi Ni CBDC na wakonesha kwenye ufafanuzi crypto currency
Basi tatizo liko kwa mtoa taarifa / mleta thread, kwa kushindwa kubainisha tofauti y7a crypto na CBDC.

Kimsingi hii sio habari mpya.

Iko tangu mwaka jana mwezi may /June

Hivyo hata heading ya thread inapaswa kuwa na neno CBDC. na sio neno crypto. Ukiweka neno crypto maana yake hujui kitu unachokitolea meleezo trust me

1673758863517.png

=
 
Basi tatizo liko kwa mtoa taarifa / au hili bandiko.

Kimsingi hii sio habari mpya.

Iko tangu mwaka jana mwezi may /June

Hivyo hata heading ya thread inapaswa kuwa na neno CBDC. na sio neno crypto. Ukiweka neno crypto maana yake hujui kitu unachokitolea meleezo trust me

View attachment 2481562

Najaribu kuupload taarifa. Inagoma. BoT wamefafanua vizuri kuhusu Crypto. Ingawa wao ndio watairegulate. Hivyo Kuna mechanisms watazitumia kutofautisha crypto yao na zingine. Crypto ya Central Bank itakuwa regulated.
 
Hizi ni kauli tatanishi.

Maelezo yalipaswa kuishia kwenye Central Bank Digital Currency (CBDC) tu.

Hilo neno crypto currency futa, halina mantiki hapo, maana taarifa inakuwa ya uongo.
=
Je unafahamu tofauti ya Cryptocurrency na CBDC?
=

"Cryptocurrency is a decentralized digital currency that uses cryptography for security, and is not controlled by any government or institution.

While CBDC is a digital version of a country's fiat currency, issued and backed by the country's central bank, intended to coexist with cash and bank deposits and to be used for various transactions, such as paying bills and making purchases."
Nilitaka kushangaa.

Digital currency ni tofauti na crypto currency.

Kwenye crypto bado sana maana hata nchi nyingi zilizokua zinatumia sasa zimeanza kupiga marufuku.

Pili sisi bado sana kwenye hayo mambo.
 
Ingawa wao ndio watairegulate.
Umeona sasa unazungumzia CBDC

Lakini unatumia neno crypto, hapo ndipo ulipo mgogoro baina yangu nawe,

Crypto ni decentralized, hakuna serikali duniani wanao i_regulate ( Cryptocurrency is a decentralized digital currency that uses cryptography for security, and is not controlled by any government or institution. )
 
Mbona kwenye document wamesema bado wanaendelea na utaratibu?
Hiyo haitaanza leo wala miaka 10 ijayo
 
Najaribu kuupload taarifa. Inagoma. BoT wamefafanua vizuri kuhusu Crypto. Ingawa wao ndio watairegulate. Hivyo Kuna mechanisms watazitumia kutofautisha crypto yao na zingine. Crypto ya Central Bank itakuwa regulated.
Haya maelezo ni sahihi, kwa mlengo wa CBDC

Hivyo, kila penye neno crypto weka neno CBDC. 👇🏼👇🏼👇🏼
=

"Najaribu kuupload taarifa. Inagoma. BoT wamefafanua vizuri kuhusu CBDC. Ingawa wao ndio watairegulate. Hivyo Kuna mechanisms watazitumia kutofautisha CBDC yao na zingine. CBDC ya Central Bank itakuwa regulated."
 
Back
Top Bottom