BOT achaneni na noti ya 10,000/-

Huku mtaani hakuna kitu kinasumbua kama chenji.
Watu hawauzi kisa kakosa chenji au auzunguke wee.
5000 na 10000 ni shida,

Mbadala wa efu kumi mprinti 2000 na noti mpya ya 3000 ziwe nyingi za kutosha bila kusahau 500 na 1000.
Chenji ni tatizoo.
Yaani we jamaa, unataka watu tutembee na milioni 1 kwenye sandarusi sasa
 
Au nyanya moja 500? Andazi au kitumbua kimoja 500? Fungu moja la mchicha 500? Acheni hizooo...
uliwahi kununua nyanya moja moja mia tano wapi? ukizitoa mia na mia mbili kwenye mzunguko, automatically bidha za mia na mia mbili zitakuwa ni 500
 
Bila shaka unataka uifanye nchi yetu kuwa kama Zimbabwe wewe. Bora kuondoa 0 moja kwenye noti zetu (kama ingewezekana) lakini siyo huo ushauri wako wa kuondoa matumizi ya fedha nyingine ndogo ndogo kwenye mzunguko. Watu wa ccm hamjawahi kuitakia nchi yetu mema hata siku moja.

Miaka ya 1970's, dola moja iliwahi kuwa sawa na shilingi 5 tu! Tangu hapo mnachokifanya kwenye uchumi wa nchi hii mnakijua wenyewe! Mbwembwe tu nyingiii za uchumi kukua kwa 7% halafu wananchi walio wengi wakiendelea kuishi kwenye dimbwi la umaskini uliokithiri.
yaani uondoe zero kwenye kila hela, ni nani ataitumia hiyo hela kufanya exchange. Yaani 10000 iwe buku tu, kama ni hivyo kwa nini usiseme 2000, 5000 na 10000 zitolewe ibaki 1000, 500, 200, 100 na 50.

yaani mzungu na dola zake 100 apewe 20000 tu akicheji. Dola 100 ni pesa kubwa sana si tu kwa bongo hata ulaya, ila leo utampa 20000 tu pesa ambayo ni ndogo sana. ni nani atakubali exchange ya hivyo?
 
yaani uondoe zero kwenye kila hela, ni nani ataitumia hiyo hela kufanya exchange. Yaani 10000 iwe buku tu, kama ni hivyo kwa nini usiseme 2000, 5000 na 10000 zitolewe ibaki 1000, 500, 200, 100 na 50.

yaani mzungu na dola zake 100 apewe 20000 tu akicheji. Dola 100 ni pesa kubwa sana si tu kwa bongo hata ulaya, ila leo utampa 20000 tu pesa ambayo ni ndogo sana. ni nani atakubali exchange ya hivyo?
Kwani unadhani ni mzungu ndiye alisema tuwe na elfu kumi???
 
tatizo si uwepo wa elfu 10, tatizo ni uwepo wa mia , mia mbili na mia tano nyingi sana katika mzunguko wa fedha kuliko mzunguko wa elfu 1, 2 na 5 na hivyo kufanya upatikanaji wa 10 kuwa mdogo sana na hata upatikanaji wa cheji kuwa wa shida kwa elfu 10 kwa sababu pesa za kuicheji elfu 10 zinakuwa zina mzunguko mdogo.
suluhisho
1. serikali ingeanza utaratibu wa kupunguza mia 1, 2 na 5 kwenye mzunguko ili zibaki hizo nyingine ndo ziwe nyingi.
2. bidhaa zingeanza kuuzwa kuanzia mia 5, kwa maana ya kwamba uwepo wa bidhaa za mia moja zinafanya mzunguko wa mia tano tu wenyewe kuwa wa shida sembuse 10000
3. watu wanatakiwa kufundishwa kuijua thamani ya elfu 10 kuliko thamani ya mia moja, hii itasaidia watu kuachana na mia na kutafuta na kutumia elfu 10
Kama ndo ukiteuliwa kua mshauri wa uchumi wa rais UTAIINGIZA NCHI KWENYE JANGA KUBWA! kwa huu ushauri wako!! Yani bidhaa zianzie Mia 5 😁😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
zinatengenezwa pakiti za mia tano na kuachana na hizi za mia mia, kwa maana kwamaba hiyo pakiti ya miatano inakuwa na ujazo sawa na pakiti za mia mia tano
Halafu MTU asiye na uwezo wa kupata Mia tano ya kununua majani asinywe chai? Kumbuka kipato Cha mtanzania kwa siku ni chini ya 2500
 
Duhh!! Wewe ndiyo zero mwingine!! Kwa hiyo bidhaa ama huduma za mia mia zifutwe zibaki za 1000 hadi 10,000 tu?au nauli zetu hizi za 400 tuzipandishe hadi 2000 ili kubana mzunguko wa mia mia?
Hahahahahahaha! Yani huyu jamaa Ni TABULARASA KUBWA! Kisa noti ya 10k ndo ufanye mageuzi makubwa hvo yatakayomaliza kabisa uchumi
 
Huku mtaani hakuna kitu kinasumbua kama chenji.
Watu hawauzi kisa kakosa chenji au auzunguke wee.
5000 na 10000 ni shida,

Mbadala wa efu kumi mprinti 2000 na noti mpya ya 3000 ziwe nyingi za kutosha bila kusahau 500 na 1000.
Chenji ni tatizoo.
Labd iwe mbadala ya 5k yani noti ya 5000 na iwepo ya 2000 na 3000.
 
wakipunguza sifuri moja kwa kila noti itakuwa kama ifuatavyo:-
10,000=1000
5,000=500
2,000=200
Tatizo itabidi tutembee na magunia ya hela na noti kiukweli zitachakaa mno.Sababu hela yetu dhidi ya dola iko chini.Kwa muktadha huo noti ya elfu10 na elfu5 haiepukiki especially for big transaction.
Noti inapoondolewa 0 moja inamaana kua uwezo wa manunuzi wa sh 10000 utafanywa na sh 1000 so hakutakua na haja ya kutembea na mabunda Kama usemavyo! Hio ni kawaida kiuchumi na si kitu kigeni! Mf mshahara wa milion 1 unakua laki 1
 
una pointi ya msingi na ni kitu kilichofanywa na zambia, walifanya 'currency rebasing' (haiitwi kupunguza sifuri, wanaita currency rebasing)
yani waondoe shilingi hii, kisha walete shilingi mpya ya kitanzania ambayo, kwenye kubasilishiwa ukipeleka benki sh 2000 ili upewe noti mpya basi unapewa pesa mpya ya noti ya ya 200 yenye thamani sawa na hiyo buku mbili
serikali inaweza kufanya hivyo, ila naona wanaona sio lazima maana ukipanda daladala ukalupa 500 kesho ukapewa hela mpya ukalipa 50 haumaanishi umeimprove llolote, maana ule mshahara wako wa 50,000 nao sasa utasoma 5000 hivyo ukali wa maisha uko palepale
faida pekee ni kwenye kuimport, tunakuwa na strong currency, wasomi wa uchumi wanajua zaidi
Mtu wa kijiweni anaweza bisha mpk asubuhi anahisi Hilo haliwezekani mkuu! Hata humu naona layman wengi hawaelew hii kitu Bora ulivowaelimisha!
 
Wana coins mkuu hiyo cent 50 ni coin
AHSANTE.
Mfano Tanzania
Coins Ni sh 50-500
je,kwa USA coins inaanzia cent ngapi Hadi wapi?

Lakini pia,
kwa Tz Noti inaanzia
1000-10000
je,kwa USA noti inaanzia Dola/Cent ngapi?

Msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom