BOT achaneni na noti ya 10,000/-

BOT achaneni na noti ya 10,000/-

... someni katikati ya mistari mtamwelewa mleta uzi.
 
Duhh!! Wewe ndiyo zero mwingine!! Kwa hiyo bidhaa ama huduma za mia mia zifutwe zibaki za 1000 hadi 10,000 tu?au nauli zetu hizi za 400 tuzipandishe hadi 2000 ili kubana mzunguko wa mia mia?
Mwenye 1000 anataka apate sukari ya 500 majani ya 100 na vitumbua vi4 utamsaidiaje
soma ukiwa umetulia, kichwa chako kinafanya kazi vizuri
 
Ukiprint hela nyingi sana ukaziingiza kwenye mzunguko lazima uchumi ushuke. Why?

Kwa sababu watu watakuwa na hela nyingi mkononi wakati kiwango cha huduma na bidhaa bado ni kile kile.
 
tatizo si uwepo wa elfu 10, tatizo ni uwepo wa mia , mia mbili na mia tano nyingi sana katika mzunguko wa fedha kuliko mzunguko wa elfu 1, 2 na 5 na hivyo kufanya upatikanaji wa 10 kuwa mdogo sana na hata upatikanaji wa cheji kuwa wa shida kwa elfu 10 kwa sababu pesa za kuicheji elfu 10 zinakuwa zina mzunguko mdogo.

suluhisho
1. serikali ingeanza utaratibu wa kupunguza mia 1, 2 na 5 kwenye mzunguko ili zibaki hizo nyingine ndo ziwe nyingi.

2. bidhaa zingeanza kuuzwa kuanzia mia 5, kwa maana ya kwamba uwepo wa bidhaa za mia moja zinafanya mzunguko wa mia tano tu wenyewe kuwa wa shida sembuse 10000

3. watu wanatakiwa kufundishwa kuijua thamani ya elfu 10 kuliko thamani ya mia moja, hii itasaidia watu kuachana na mia na kutafuta na kutumia elfu 10
huoni kuwa huo ni inflation isiyo ya lazima
 
Tuuze kwa wingi huduma (utalii-usafiri wa ndege, matibabu, mikutano, michezo, fukwe, mbuga, elimu, utafiti, muziki) na bidhaa nje. ****Tuingize pesa ya kigeni nyingi.
Inabidi kuanza kuwekeza kwa matrilioni kabla ya kuanza kuuza.
 
Nenda benji yoyote kachukue chenji.
Ina maana sisi tunaouza mil 3 kwa siku tutakuwa na mabunda mangapi.
2k x ....?
 
Huku mtaani hakuna kitu kinasumbua kama chenji.
Watu hawauzi kisa kakosa chenji au auzunguke wee.
5000 na 10000 ni shida,

Mbadala wa efu kumi mprinti 2000 na noti mpya ya 3000 ziwe nyingi za kutosha bila kusahau 500 na 1000.
Chenji ni tatizoo.
Nimetoka petrostation kuomba change mda c mrefu
 
unajua hata inflation ni nini? inflation ni pale ambapo unanunua kitu cha mia kwa mia tano bila kitu hicho cha mia kufikia ujazo stahiki wa kuuzwa mia tano. nisome taratibu ndio utanielewa
unapoondoa hizo mia mbili moa moja si pia unafanya vitu vya mia mia mbili kwenda kuuzwa kwa buku na kendelea, ama sivyo
 
unajua hata inflation ni nini? inflation ni pale ambapo unanunua kitu cha mia kwa mia tano bila kitu hicho cha mia kufikia ujazo stahiki wa kuuzwa mia tano. nisome taratibu ndio utanielewa
halafu karejee kusoma sababu za inflation, moja kati ya sababu ni kupungua kwa fedha kwenye mzunguko, maana sasa vitu vya bei chee itabidi viuzwe kwa bei juu, maana hamna tena vile visarafu kukidhi haja katika ununuzi
 
unajua hata inflation ni nini? inflation ni pale ambapo unanunua kitu cha mia kwa mia tano bila kitu hicho cha mia kufikia ujazo stahiki wa kuuzwa mia tano. nisome taratibu ndio utanielewa
na pia utakuwa unaua ile sifa ya fedha, kuwa a good money should be divisible, 'divisibilitu of money'

wanauchumi wenyewe wanasema pesa nzuri ni ile ambayo imegawanywa kwenye viuniti ili kufanya ufanisi katika ununuzi, yani lazima hivyo visarafu na vinoti vidogo viwepo na hayo manoti makubwa yawepo kwa sababu za msingi kabisa
 
halafu karejee kusoma sababu za inflation, moja kati ya sababu ni kupungua kwa fedha kwenye mzunguko, maana sasa vitu vya bei chee itabidi viuzwe kwa bei juu, maana hamna tena vile visarafu kukidhi haja katika ununuzi
Nadhan umeongea kinyume... moja kati ya sabab za inflation ni kuongezeka (kuskoendana na ukuaji wa uchumi) kwa fedha kwenye mzunguko
 
tatizo si uwepo wa elfu 10, tatizo ni uwepo wa mia , mia mbili na mia tano nyingi sana katika mzunguko wa fedha kuliko mzunguko wa elfu 1, 2 na 5 na hivyo kufanya upatikanaji wa 10 kuwa mdogo sana na hata upatikanaji wa cheji kuwa wa shida kwa elfu 10 kwa sababu pesa za kuicheji elfu 10 zinakuwa zina mzunguko mdogo.

suluhisho
1. serikali ingeanza utaratibu wa kupunguza mia 1, 2 na 5 kwenye mzunguko ili zibaki hizo nyingine ndo ziwe nyingi.

2. bidhaa zingeanza kuuzwa kuanzia mia 5, kwa maana ya kwamba uwepo wa bidhaa za mia moja zinafanya mzunguko wa mia tano tu wenyewe kuwa wa shida sembuse 10000

3. watu wanatakiwa kufundishwa kuijua thamani ya elfu 10 kuliko thamani ya mia moja, hii itasaidia watu kuachana na mia na kutafuta na kutumia elfu 10

Bila shaka unataka uifanye nchi yetu kuwa kama Zimbabwe wewe. Bora kuondoa 0 moja kwenye noti zetu (kama ingewezekana) lakini siyo huo ushauri wako wa kuondoa matumizi ya fedha nyingine ndogo ndogo kwenye mzunguko. Watu wa ccm hamjawahi kuitakia nchi yetu mema hata siku moja.

Miaka ya 1970's, dola moja iliwahi kuwa sawa na shilingi 5 tu! Tangu hapo mnachokifanya kwenye uchumi wa nchi hii mnakijua wenyewe! Mbwembwe tu nyingiii za uchumi kukua kwa 7% halafu wananchi walio wengi wakiendelea kuishi kwenye dimbwi la umaskini uliokithiri.
 
Hiki kitu ni kweli chenji zina usumbufu nna biashara ya MPESA Sehemu aisee ni shida hadi bank kupata pesa ndogo ndogo
 
Nadhan umeongea kinyume... moja kati ya sabab za inflation ni kuongezeka (kuskoendana na ukuaji wa uchumi) kwa fedha kwenye mzunguko
hiyo ni short run ina pelekea defation, ila in long run inapelekea inflation maana,

kukiwa na deflation uzalishaji unapungua, japo bei zitabaki chini ila kadri bei zinavyopungua watu wanaanza kuacha kuzalisha na matokeo yake kufanya vitu muhimu kuwa adimu kwenye uchumi na kupelekea kupanda vitu bei kwa kasi, kwasababu mahitaji ni mengi kuliko uzakishaji

hicho ndicho kilichotokea miaka ya themanini,

sera za kijamaa zilipunguza uzalishaji, kwaaababu ya deflatiin matokeo yake uzalishaji na ununuzi na biashara zikapunguza uzalishaji na matokeo yake mahitaji yakazidia supply na kupelekea inflation iliyopitiliza

ndicho kilichotokea zimbabwe, uzalishajo kwenye mashamba ya wazungu ulpopungua ikapelekea upungufu wa uzalishaji, mahitaji yakazidi supply ikapelekea inflation

kwahiyo karejee vitabu ndugu yangu, moja kayi ya athari za deflation ni hupelekea inflation in a long run
 
Nkwe2RG

yani kama unavyoona saaa serikali inagoma kuachia pesa, kuwa inapambana na inflation ila kiuhalisia tunaingia kwenye deflation ndio maana bei za mazao zinashuka, halafu pesa inapungua katika mzunguko, na wakulima wataacha kulima mazao kwa wingi kwa kuwa hamna faida na kulima ni gharama, wafanyabiashara watafunga biashara kwasababu hakuna faida ya kuvutia

in long run, kutakuwa na shortage in supply, bidhaa muhimu zitakuwa zinauzwa kwa uchache na wakulima hawazalishi sana

in long run, vitu vitapanda bei

hivyo iambieni serikali yenu inavyopinga hiyo inflation kwa nguvu zote wawe makini wasituletee deflation maana mwishowe, vitu vikizalishwa na kuuzwa kwa uchache kutaibuka inflation ya zimbabwe

na hiyo ni somo la economics la form six tu.
 
Back
Top Bottom