Bora Veta au Vyuo vya kati kwa form 4?

Bora Veta au Vyuo vya kati kwa form 4?

Soul21

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
195
Reaction score
329
Wanafunzi wanaokosa kwenda kidato cha tano na sita huwa wanapangiwa vyuo.
1000458224.jpg

Picha: Daily News

Ila nilichogundua mkakati huu unalundika wanafunzi wengi kusoma koz nyingi ambazo hazina athari ya moja kwa moja kwenye maisha yao zaidi baada ya kuhitimu wanakuja kuwa na mawazo ya ajira. Mfano, mipango, Au biashara.

Watoto wengi wanatoka familia za chini huku wakitumia gharama kubwa.

kwa nini wasiende VETA kupata ujuzi ambao siku akihitimu hawezi kukosa elfu tano na kama maarifa ya biashara apewe akiwa VETA.

China wanachofanikiwa si kwamba wana akili sana bali wanatumia ujuzi wa mikono na akili kuzalisha bidhaa ambazo mwenye unaona za hovyo.

Lakini kupitia veta za ushonaji, ujenzi, uchomeleaji tunaweza kuzalisha bidhaa ambazo tunaagiza china tena hazina ubora.

Hitimisho, Angalia koz unayoenda kusoma uchague kati ya kuenda kumeza taarifa na kupata ujuzi wa moja kwa moja ni kipi bora.
 
Veta ina nafuu japo ina madhaif yake ila watu wanaotoka hapo hawachagui kaz sana kama hawa wa vyuo vya kati
 
VETA vikiendlea kuboreshwa zaidi ki teknolojia ni sehemu nzuri kwa mwanafunzi kwenda kupata ujuzi wa moja kwa moja utakao tatua changamoto nyingi zinazotuzunguka..
 
Yule mzambia sijui mmalawi aliyetengeneza gari inayotumia radio wave hivi amefikia wapi?

Nimetoa huo mfano kuuliza kama mazingira sahihi yamewekwa ili kuwawezesha hawa vijana wabunifu waliotoka veta?
 
Back
Top Bottom