Bora nikate tamaa ili niwe salama

“ kuna wakati maisha yanakosa maana”
Exactly my feelings right now!!
Jus tryna dig deep n get myself outta this shit!Ila ni ngumu asikwambie mtu!
 
We jamaa upo vizuri kinoooooma yaaan umeteremka kisomi na kueleweka sana...hii ndio inaitwa akili kubwa inayotakiwa katika jamii zetu maana wengi wetu tunapitia vipindi vigumu sana katika maisha (binafsi now napambana na colon cancer) so watu wenye positive mindset kama wewe ndio haswa mnatakiwa na in that case hata mhusika was tatizo anajikuta anapona kwa ushauri wako kuliko kujiassociate na watu wenye negative mindset ni kujirudisha nyuma na kukata tamaa jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yetu haya
Ubarikiwe sana kwa maneno haya ya kutia moyo mkuu
Mkuu kwanza nikupongeze

Kuna watu wengi umewazidi kifikra.

Kila mtu ana Ulemavu wa aina yake katika maelezo yako pale juu mwenyewe umejionea kwa tafiti za haraka wengi hatujawin kimaisha pamoja na uzima wa viungo kwa hiyo hapo umejifunza hali si kitu, mwaka unaisha wengi hatujatimiza hata nusu ya plans hivyo, mwenye masikitiko hauko peke yako tupo wengi kuna ulemavu wa tabia ambao huu unatibika kwa aina yake na mtu ukiwa na tabia flani pia kutusua ni issue, sasa kumbe wagonjwa tupo wengi tofauti ni namna tunavyoamua kuangalia na kutazama vitu.

Kuna dada anaitwa Wakonta instagram na wengine wapo nchi mbalimbali jaribu kupitia page zao hivi kuna mtazamo unaweza upata.

Pia yule daktari uliyeshauriwa fanya bidii mtafute, tafuta options kama ni kula vitu flani hivi kwa ajili ya viungo vimazoezi au massage kidogo,na kuna vitabu umeshauriwa vidownload visome vitakuongezea kitu kikubwa sana.

Usiweke matarajio makubwa yenye kupita uwezo, weka lengo lisilosumbua na halisi linaloendana na mazingira , watu wanaoweza kukusaidia ila yaweke tu ikiwa umeamua kubadilisha mtazamo wako jinsi unavyofikiri na unapofanikiwa kwa vitu vidogo vifurahie usilaumu saana unapofail kumbuka everyone blame so much few wins many lose only believeing will make you one of the winners.

ukijishughulisha na mtazamo positive then from nowhere positive things will come to you usiiangalie hali uliyonayo ndipo unapojiumiza na ndipo ugonjwa hasa ulipo,good vibes attract good things so as bad vibes....attract ....

Mtu ni akili na si kingine ukiamua kuweka imani na kutazama akili yako utafurahia mengi, sasa hivi base sana nakuandika vitu kama huu uzi una wachangiaji wengi sana kuna nyuzi zimeanzishwa nyingi hazina wachangiaji so this shows that you have something in you.

soma vitabu, then andika vitu unavyoweza ukitulia kuna namna mawazo flani hivi yatakujia, mtu ni vile anavyofikiri nakuwaza na tunawaza kwa ubongo na si kingine, halafu furahia sana vitu vidogovidogo unaweza kuona ni vyakawaida lakini si vyakawaida.

Furaha ya moyo ni vidonge tosha sana kwenye mwili ukijilaumu na kuweka uchungu ni sumu zaidi ya kumi umezimeza kwa mpigo.

Inawezekana ni mlemavu wa viungo lakini kwa uwezo wako unaweza kushauri Kundi la wataalamu na likapiga step

Jiweke sana na makundi yanayokupa moyo siyo yenye kukukatisha tamaa nakufanya uyalaumu maisha,
mawazo yako na yale yawatakaokuzunguka ndo yatakayokufanya uwe na mtazamo fulani

magonjwa mengi yanaumiza kwakuwa tumeamua kuyatazama kwa jinsi tunavyoyaogopa na jamii ya watu wengi inavyoyaangalia.

Ukipewa chance yakufanya kitu unachoweza fanya the best usiangalie hali yako sababu hali yako si wewe, watu wengi wengine wanamafanikio yakipesa lakini wana hali zao mbalimbali zipo kansa kisukari na mengine mengi lakini mtazamo wako ndo utafanya hiyo hali isikuumize kichwa.

Tafuta councellors wazuri watakusaidia sana unaweza ukajishangaa.

Ikiwezekana pia watu wanaokuzunguka /(au unaotaka kudeal nao kama ni biashara au shughuli yoyote) waoneshe hii page watapata namna flani katika fikra.

When things get tough be the toughest....things may then opt to be soft with you.



NOTA BENE: Mtafute Doctor Othman uliyeshauriwa na Cappitano
Ushauri wote humu upangie mkakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha hayatakaa yatosheleze. Hivyo ni budi na kushukuru kwa ulichonacho. Those who are the happiest never did have everything, but they are thankful for everything they do have.

When you learn to appreciate the little you have, then the big things are soon to happen. Please learn to be grateful.

Anza kwa kushukuru na kufurahia pumzi uliyonayo, shukuru kwa amani, shukuru kwa kila kitu huku ukijilinganisha na wasio nacho kabisa na utapata amani ya moyo sana.

Then, lower or have less expectations from someone and you will never be disappointed. If you love someone, then don't expect to be loved back. If you give, don't expect the return. If you help, don't expect a thankful hand. On whatever you do to others, have no expectations. You will have peace within you.
I like what you have written!!
 
Mzeebaba itakuwa hujanielewa tu, yaani natamani sana kupambana lakini kuna ugonjwa umeniweka ndani aisee daaah yaani nikiwaona wanaopambana huko nje nahisi kupasuka maana namimi ningekuwa mmoja wao na hakika ningetoboa lakini ugonjwa umenipiga kabali ndomaana hata nataka nikate tamaa nisifocus tena yanayoendelea huko nje just niwe kama sipo vile nikubali tu kuwa siwezi kuwa kama nyinyi wazima
Hapa sasa mkuu ndio nimekuelewa hukoo juu kote sikukupata hata kidogo nikata nikupe ushauri kwamba "kajiue tu".

ILA KAMA ISSUE NI UGONJWA mzee wa kazi pole sana sana.Mungu akusaidie.Kuna mambo ambayo huwa yako nje ya uwezo wetu na unapaswa kukubaliana na hali amd let the situation be.Huko hakuitwi kukata tamaa bali unakubakiana na hali halis na kuomba aliye juu ya uwezo wote yy ndio aingilie kati..Pole sana mzee..kama ni ugonjwa pole sana..Nakuombe uwe mzima tena.Afya ndio kila kitu mengine yanafuata.get well soon.
 
Nlipokuwa mdogo (before 20yrs) ilikuwa kila nikitaka kitu nikapima na kuamini naweza kuwa ama kupata basi ilikuwa ni lazima nifanikishe ningeacha vyote nifocus na hicho tu mpaka ieleweke. Sasa nimekuwa mkubwa bado ni mtu wa strong desires yaani nikitaka nimetaka akili yangu itaumia kutafuta namna ya kufanikisha ninachotaka kwa nguvu zote lakini mambo yamekuwa magumu mno hayaji kirahisi na si tu kirahisi bali hata kwa nguvu zote ninazoapply ambazo nilipima nikaona inawezekana lakini mambo hayawezekani.

Maisha yangu ni kama yamesimama, mateso yanaongezeka , changamoto hazivumiliki (ugonjwa/ulemavu) nimeshindwa kufanikisha nilivyofikiri itawezekana lakini nashindwa kupotezea na kumuachia Mungu. Msemo wa Mungu hachelewi wala hawahi haufanyi kazi kwangu, siwezi kabisa vumilia zaidi kuendelea na maisha ya hivi lakini nifanye nini sielewi, nikweli ninayoyataka yapo nje ya uwezo wangu, mengine nje ya uwezo wa binadamu lakini napata machungu kuona kwanini isiwe yaani milango yote imefungwa sasa nitokee wapi, halafu kwanini iwe mimi tu?

Agrrrh... Nahisi kuchanganyikiwa! hii strong desire ya kuwa mtu fln kuishi katika level fln licha ya hali yangu sasa inanitesa vilivyo. Nikikaa kutwa nzima kichwa kinawaka moto nifanya nini na kila ninachoamini nikijaribu sifanikiwi, sitakiwi kuwa hapa nilipo, sitakiwi kuishi hivi, Huu ni mtihani mzito sana kwangu. Nawaza pengine uzito hasa unakuja kutokana na aina ya mtu niliye. Bora ningekuwa mtu nisiyeamini katika mafanikio, kama ningekuwa mtu wa kukubali kushindwa walahi nisingeteseka hivi pengine ningekuwa cool nimemwachia Mungu lakini kiukweli nimeshindwa kukata tamaa.

Nimejaribu kujiwekea miiko kwamba No social networks hasa hasa FB, whatsap groups labda zinaniongezea anxiety kwasababu kule wengi ninaowahamu naona ni kama wote wameridhika wanafurahia maisha yao. Nikiwaza hivi kweli namimi niridhike na hali hii BIG NO! Nikasema wacha niachane na mambo ya Inspirations, Motivations huko IG nikiingia watu wanafanya big moves, hata wauza sura wanaoshine kwa kufake life still wanaEnjoy life, wakina Ontario kila siku kutusema tunaosindikiza maisha, Quote yake moja anasema "Maisha hayajawahi kuwa selective, hayajui kama baba yako ni maskini au wewe ni kilema, kipofu, yatima. Maisha ni kama mvua ikinyeesha haiangalii kama kuna mtu kaanika mpunga, kuna mtu anajenga nyumba, kuna mtu anaanika nguo, haiangalii chochote same as life.

Ni jukumu lako kuwa na mwamvuli " Basi nikiona hivyo moyo unauma sana naona bora nihamie kwenye kushabikia udaku na story za kina Mondi kusogeza siku lakini nazo zinachosha big times. Sina rafiki, sina mpenzi wala sidhani kama nataka kuwa nao kwasasa maana hata marafiki niliokuwa nao hatumatch tena kama zamani na urafiki umefifia. Sifurahii kabisa kuishi hivi, bila kuwa ninavyotaka seriously sijioni kuumaliza mwaka 2020.

Nimekosa alternative ya vipi nibadili attitude niliyonayo, niiambie nini nafsi yangu ili iridhike akili yangu itulie just to be calm and patient nisisumbuke tena kujiwazia chochote. Kama kuhold endurance nimehold sana nimefika mwisho kabisa sasa nahisi hata naweza kujifanyia kitu kibaya. Two times this year nilichukua hatua kadhaa toward self suicide lakini nikaghairi na kuishia kutokwa na machozi, nilimfikiria mtu mmoja anayenipenda sana lakini hana namna ya kuweza kunisaidia. Nahisi nguvu kubwa inanivuta kwenye self suicide kwakuwa seriously sioni care wala love kutoka kwa watu wanaopaswa kunicare na mimi ni mzigo wao.

Lakini siyo makosa yao pengine wanahisi I'm strong to handle the situation by myself. Should I tell them I need more love and care from them than this how they take me for granted now? Masculinity feelings stops me. Nahisi mwanaume sitakiwi kuomba mtu anipende wala siwezi kulazimisha mtu anijali. Is this right? How can I change this attitude. I feel worthless hilo halipingiki na tatizo langu hasa ni kutambua hilo. How can I fix this? Haya mawazo yasije kuniletea brain tumor ni bora nikubali kushindwa, nikate tamaa lakini nawezaje? Nitaweza kweli kujitenga na kila kitu, kila mtu? Si ndo mwisho wa siku nitajua mimi .

Lakini nitaweza kweli kuassociate na society katika hali tofauti nikiwa mtu wa chini ninayehisi kupoteza thamani niliyokuwa nayo mwanzo ? Sipendi kuwa looser, well nimekuwa looser lakini sipendi kuonekana kama looser, sipendi kuwa worthless hivi. Dah, masikini mimi... Bora nikate tamaa!
#badmood #disabilityfeelings #poverty
Pole sana maisha yana changamoto zake hivyo Huna budi kukabiliana nazo
 
We jamaa upo vizuri kinoooooma yaaan umeteremka kisomi na kueleweka sana...hii ndio inaitwa akili kubwa inayotakiwa katika jamii zetu maana wengi wetu tunapitia vipindi vigumu sana katika maisha (binafsi now napambana na colon cancer) so watu wenye positive mindset kama wewe ndio haswa mnatakiwa na in that case hata mhusika was tatizo anajikuta anapona kwa ushauri wako kuliko kujiassociate na watu wenye negative mindset ni kujirudisha nyuma na kukata tamaa jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yetu haya
Ubarikiwe sana kwa maneno haya ya kutia moyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Oooh mkuu pole sana! nimeona hiyo colon cancer moyo umeshtuka sana kwakuwa mimi pia nina bowel dysfunction ambayo pia mwisho wa siku inaletaga colon cancer. Nataman kujua unakabiliana vipi na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uboya kamanda unaniangusha.

Ili upate pesa lazima ujifunze kuuza.

Mengine yote ni blah blah

Jifunze kuuza utaona pesa haipungui mfukoni

Cheers 🥂


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
We jamaa upo vizuri kinoooooma yaaan umeteremka kisomi na kueleweka sana...hii ndio inaitwa akili kubwa inayotakiwa katika jamii zetu maana wengi wetu tunapitia vipindi vigumu sana katika maisha (binafsi now napambana na colon cancer) so watu wenye positive mindset kama wewe ndio haswa mnatakiwa na in that case hata mhusika was tatizo anajikuta anapona kwa ushauri wako kuliko kujiassociate na watu wenye negative mindset ni kujirudisha nyuma na kukata tamaa jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yetu haya
Ubarikiwe sana kwa maneno haya ya kutia moyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi Mkuu unaendeleaje?
 
Back
Top Bottom