Bora nikate tamaa ili niwe salama

Bora nikate tamaa ili niwe salama

Mkuu kwanza nikupongeze

Kuna watu wengi umewazidi kifikra.

Kila mtu ana Ulemavu wa aina yake katika maelezo yako pale juu mwenyewe umejionea kwa tafiti za haraka wengi hatujawin kimaisha pamoja na uzima wa viungo kwa hiyo hapo umejifunza hali si kitu, mwaka unaisha wengi hatujatimiza hata nusu ya plans hivyo, mwenye masikitiko hauko peke yako tupo wengi kuna ulemavu wa tabia ambao huu unatibika kwa aina yake na mtu ukiwa na tabia flani pia kutusua ni issue, sasa kumbe wagonjwa tupo wengi tofauti ni namna tunavyoamua kuangalia na kutazama vitu.

Kuna dada anaitwa Wakonta instagram na wengine wapo nchi mbalimbali jaribu kupitia page zao hivi kuna mtazamo unaweza upata.

Pia yule daktari uliyeshauriwa fanya bidii mtafute, tafuta options kama ni kula vitu flani hivi kwa ajili ya viungo vimazoezi au massage kidogo,na kuna vitabu umeshauriwa vidownload visome vitakuongezea kitu kikubwa sana.

Usiweke matarajio makubwa yenye kupita uwezo, weka lengo lisilosumbua na halisi linaloendana na mazingira , watu wanaoweza kukusaidia ila yaweke tu ikiwa umeamua kubadilisha mtazamo wako jinsi unavyofikiri na unapofanikiwa kwa vitu vidogo vifurahie usilaumu saana unapofail kumbuka everyone blame so much few wins many lose only believeing will make you one of the winners.

ukijishughulisha na mtazamo positive then from nowhere positive things will come to you usiiangalie hali uliyonayo ndipo unapojiumiza na ndipo ugonjwa hasa ulipo,good vibes attract good things so as bad vibes....attract ....

Mtu ni akili na si kingine ukiamua kuweka imani na kutazama akili yako utafurahia mengi, sasa hivi base sana nakuandika vitu kama huu uzi una wachangiaji wengi sana kuna nyuzi zimeanzishwa nyingi hazina wachangiaji so this shows that you have something in you.

soma vitabu, then andika vitu unavyoweza ukitulia kuna namna mawazo flani hivi yatakujia, mtu ni vile anavyofikiri nakuwaza na tunawaza kwa ubongo na si kingine, halafu furahia sana vitu vidogovidogo unaweza kuona ni vyakawaida lakini si vyakawaida.

Furaha ya moyo ni vidonge tosha sana kwenye mwili ukijilaumu na kuweka uchungu ni sumu zaidi ya kumi umezimeza kwa mpigo.

Inawezekana ni mlemavu wa viungo lakini kwa uwezo wako unaweza kushauri Kundi la wataalamu na likapiga step

Jiweke sana na makundi yanayokupa moyo siyo yenye kukukatisha tamaa nakufanya uyalaumu maisha,
mawazo yako na yale yawatakaokuzunguka ndo yatakayokufanya uwe na mtazamo fulani

magonjwa mengi yanaumiza kwakuwa tumeamua kuyatazama kwa jinsi tunavyoyaogopa na jamii ya watu wengi inavyoyaangalia.

Ukipewa chance yakufanya kitu unachoweza fanya the best usiangalie hali yako sababu hali yako si wewe, watu wengi wengine wanamafanikio yakipesa lakini wana hali zao mbalimbali zipo kansa kisukari na mengine mengi lakini mtazamo wako ndo utafanya hiyo hali isikuumize kichwa.

Tafuta councellors wazuri watakusaidia sana unaweza ukajishangaa.

Ikiwezekana pia watu wanaokuzunguka /(au unaotaka kudeal nao kama ni biashara au shughuli yoyote) waoneshe hii page watapata namna flani katika fikra.

When things get tough be the toughest....things may then opt to be soft with you.

NOTA BENE: Mtafute Doctor Othman uliyeshauriwa na Cappitano
Ushauri wote humu upangie mkakati.
 
sawa nakubaliana na unachosema ila iko hivi, nilipofikisha miaka 20 nikapooza miguu mwaka 2014 mpk leo nipo ndani mlemavu haitoshi nikaanza kupata changamoto zingine za kiafya. Nimeishi siku zote nikivumilia matumaini yangu nitapona na dalili zilikuwepo lakini haijawa hivyo, nje na kesi ya ulemavu nikajaribu kuendesha biashara na mambo mengine mengi madogo madogo kwa kutumia watu wengine, almost kila kitu kinafeli thus why nikaona labda nisifanye tena chochote, nisiwe na malengo yoyote wala matumaini yoyote nibaki tu kujiuguza kwasababu ninapojipa matumaini na hakuna kinachofanikiwa siponi na mambo yote ni kama hayaendi sasa hii kitu inaumiza zaidi
Mkuu pole sana,siyo kana kwamba nina underestimate situation yako,hapana ni sawa kabisa kujisikia ulivyo kwani yote hayo umeyapata at your 20s. Sasa basi ushauri wangu mkuu,Mungu hawezi kukuacha kamwe,ila binadamu watakudiscourage sana,omba usiache mkuu. Mungu hakupi jaribu likushinde mkuu,jitahidi sana kuishi kwa kuomba,ipo siku mkuu mimi na wewe hatuijui.
 
hii logic ya maisha hupangwa na Mungu ngumu sana kuelewa,tunafundishwa kwamba Mungu anachukia maovu,je kama ni hivyo kwa nini anapanga watu wafanye maovu?au kaandaa moto kutukomoa??watu wengi wanaingia kwenye maovu sababu kuu ikiwa ni Mungu,mtu anamuomba Mungu miaka na miaka hamjibu,mtu anaona bora aende kwa shetan tu ambapo atapata majibu kwa muda huo huo,na hapo ndio mwanzo wa maovu!!
Mkuu utendaji wa Mungu ni wa kipekee sana. Kwa kifupi Mungu hashindani na mwanadamu kabisa,hilo kalizungumzia baada ya gharika kitabu cha Mwanzo katika Biblia. Mkuu unaamini kuna nyakati Mungu anapitisha baraka za wengine kupitia wewe,yani unakuwa kama daraja. Ni kweli kabisa kwa kuwa tupo katika hii dunia kufanikisha mipango ya Mungu ila siyo yetu wanadamu. Sasa basi kinachotutesa sisi wanadamu ni mipango na malengo ambayo tunajipangia,ambayo ukipita upepo yasitimie tunaanza kutafuta mchawi ni nani.
 
Pole sana ndugu yangu, hayo ni mapito tu na changamoto za dunia na mwisho wa siku Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa mwisho wa kila jambo, tunahitaji kumuomba sana na shikilia sana kwenye ibada siijui imani ila Muombe Mungu usiku na mchana akufanyie wepesi kila pahala nasi pia kwa imani zetu tunakuombea pia..
 
Kwa hali uliyonayo jambo la kwanza kubali uko na hali hiyo lakini usisite kutafuta tiba popote inapowezekana ikiwa pamoja na ibada, ukipata wakati soma majalida au peruzi mitandao inayoelezea matatizo mbalimbali ya kiafya pamoja na kuomba msaada wa matibabu kwenye forum mbalimbali kama hizi JF na nk, jaribu kufanya mawasiliano na taasisi mbalimbali ndani na nje kuangalia uwezekano wa matibabu yako lakini huku ukiendelea na shughuli ndogo ndogo nitaainisha chini hapo..
 
Unaweza kufanya shughuli ndogo ndogo hapo ulipo kwa maana biashara kama duka, genge, mgahawa nk..

Usiamini kila anayekuja kwako na kujifanya mwema, hapana watanzania tulio wengi hatupo smart kwenye mambo ya watu wengine hata kama yanaweza kukuingizia kipato, Fikilia biashara ambayo 70-90% utasimama mwenyewe na hiyo 30% itakuwa kutuma wengine with no big effect..

Sijui kiuchumi una nguvu gani, kama uko vizuri unaweza kumiliki vifaa vinavyokodishika na ukakodisha kwa watu kwa malipo kabisa kwenye akaunti yako na ukawa na msimamizi tu mmoja mtu wako wa karibu, vitu kama vifaa vya music, vifaa vya ujenzi, magari nk...
 
Mhubiri:9.11
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Asante kwa kunukuu ni neno zuri sana linafariji, pengine nisingetafuta bibilia nisome lakini umefanya jambo jema kuliweka hapa neno hili (thanks)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unataka kufa na misamiati yako kibao ya kingereza sio?
Relax jikite kwenye kufight bila kuwa selective huku ukijipa moyo hizo kazi ni za mpito utafika unapotarget.
Wewe una potential kubwa mno ya kufanikiwa sema bado hujakutana na right button to press.
KINGINE JUA SITUATION MBOVU ZA MAISHA KWA SASA INA SABABISHWA NA MTU MMOJA NAE ATAONDOKA TU PATARELAX ALAFU MAGUMU HAYAKUUMIZI WEWE TU TUPO WENGI MNO KWA SASA TZ SEMA TUMECHIL TUNAMCHORA ANASEMA ANATUNYOOSHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kasema anatunyoosha so usijiona unanyooshwa peke yako tupo wengi.KITENDO CHA KUAMINI TUPO WENGI TULIOKANDAMIZWA NA PASI YAKE NI FARAJA TOSHA PIA NI SOURCE YA TUMAINI JEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna time katika maisha utatamani ungeumbwa perfect na kuinjoi maisha kama wengine.. inaeleweka na ni kawaida kwa binadamu.. you are not exceptional, IT'S NORMAL

Wafupi wanatamani kuwa warefu,

wanaoitwa wabaya wanaomba siku moja waamke na sura za kuvutia

Wenye vibamia na mabwawa nao wanatamani siku waamke wakiwa na viungo ambavyo havidhihakiwi

Walio walemavu wanatamani siku moja waamke wakiwa na uwezo wa kuona, kusikia, kutembea na kutumia mikono yao perfectly...

walio failure katika maisha kama elimu na kipato nao wanaomba siku moja wawe na mafanikio ili waheshimike

Ninachomaanisha ni kuwa "UNACHOKIONA KWA NJE SI KILA MARA KINA UHALISIA WA 100%, WATU WENGI WANA VITA ZA NDANI KWA NDANI AMBAZO WEWE HUWEZI KUZIFAHAMU ILA ZIPO..

KINACHOTAKIWA NI MABADILIKO, kama hali yako inaweza kubadilika just ifanyie kazi, kama viungo vilivyobakia vinaweza kukufanya uwe useful na kuishi , work on that... Nothing less Nothing more brother"

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks alot bro! Hakika JF ni rafiki bora sana kwangu. Kwa maneno yenu najihisi kupona, napata nguvu na tumaini jipya. You're the best friends I have

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa wewe sio looser,wewe ni mtu wa thamani kubwa,na uliyoyaandika haya yanasadifu

Japo Mimi sio mlemavu,lakini nishawahi kufikia hatua kama yako,ndio...hatua ya kutohitaji mtu yeyote,yaani Giza likiingia ukafumba macho...unatamani kusikuche...nguvu ya kusali inakufa...inafikia hatua hata ukijikwaa...unalaumu jiwe...

Lakini nikiwa nimemaliza nguvu zangu kabisa...nililia...nkasema Mungu nisaidie ...Sina na wala sijui hata maneno mazuri ya kuleta shida yangu kwako...lakini najua upo na unajua mateso yangu...nkawaza...hata Kama ningekukashifu haraka ungenirudi...sikusali sala niliofundishwa na mtu...nilisali maneno yangu na Mungu...baada ya hapo nilifunga bila wala kusali maneno mengi,zaidi ni kutafuta uwepo wake,katika muda na watu ambao see kudhania ,Alinijibu ..Sasa nimekosa shukrani Tena...Mara nyingi naangukia upotofu...namwomba Anipe nguvu/neema ya kuishi maisha ya utakatifu Kama shukrani

Usikate tamaa Kaka...unapoishia ,ndipo Mungu anaanzia...muombe patience...ntakukumbuka pia katika sala yangu...mateso/maumivu hutukomaza kiimani

Mungu na Akakuinue

Sent using Jamii Forums mobile app
Amen, asante kwa ushuhuda mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza nikupongeze

Kuna watu wengi umewazidi kifikra.

Kila mtu ana Ulemavu wa aina yake katika maelezo yako pale juu mwenyewe umejionea kwa tafiti za haraka wengi hatujawin kimaisha pamoja na uzima wa viungo kwa hiyo hapo umejifunza hali si kitu, mwaka unaisha wengi hatujatimiza hata nusu ya plans hivyo, mwenye masikitiko hauko peke yako tupo wengi kuna ulemavu wa tabia ambao huu unatibika kwa aina yake na mtu ukiwa na tabia flani pia kutusua ni issue, sasa kumbe wagonjwa tupo wengi tofauti ni namna tunavyoamua kuangalia na kutazama vitu.

Kuna dada anaitwa Wakonta instagram na wengine wapo nchi mbalimbali jaribu kupitia page zao hivi kuna mtazamo unaweza upata.

Pia yule daktari uliyeshauriwa fanya bidii mtafute, tafuta options kama ni kula vitu flani hivi kwa ajili ya viungo vimazoezi au massage kidogo,na kuna vitabu umeshauriwa vidownload visome vitakuongezea kitu kikubwa sana.

Usiweke matarajio makubwa yenye kupita uwezo, weka lengo lisilosumbua na halisi linaloendana na mazingira , watu wanaoweza kukusaidia ila yaweke tu ikiwa umeamua kubadilisha mtazamo wako jinsi unavyofikiri na unapofanikiwa kwa vitu vidogo vifurahie usilaumu saana unapofail kumbuka everyone blame so much few wins many lose only believeing will make you one of the winners.

ukijishughulisha na mtazamo positive then from nowhere positive things will come to you usiiangalie hali uliyonayo ndipo unapojiumiza na ndipo ugonjwa hasa ulipo,good vibes attract good things so as bad vibes....attract ....

Mtu ni akili na si kingine ukiamua kuweka imani na kutazama akili yako utafurahia mengi, sasa hivi base sana nakuandika vitu kama huu uzi una wachangiaji wengi sana kuna nyuzi zimeanzishwa nyingi hazina wachangiaji so this shows that you have something in you.

soma vitabu, then andika vitu unavyoweza ukitulia kuna namna mawazo flani hivi yatakujia, mtu ni vile anavyofikiri nakuwaza na tunawaza kwa ubongo na si kingine, halafu furahia sana vitu vidogovidogo unaweza kuona ni vyakawaida lakini si vyakawaida.

Furaha ya moyo ni vidonge tosha sana kwenye mwili ukijilaumu na kuweka uchungu ni sumu zaidi ya kumi umezimeza kwa mpigo.

Inawezekana ni mlemavu wa viungo lakini kwa uwezo wako unaweza kushauri Kundi la wataalamu na likapiga step

Jiweke sana na makundi yanayokupa moyo siyo yenye kukukatisha tamaa nakufanya uyalaumu maisha,
mawazo yako na yale yawatakaokuzunguka ndo yatakayokufanya uwe na mtazamo fulani

magonjwa mengi yanaumiza kwakuwa tumeamua kuyatazama kwa jinsi tunavyoyaogopa na jamii ya watu wengi inavyoyaangalia.

Ukipewa chance yakufanya kitu unachoweza fanya the best usiangalie hali yako sababu hali yako si wewe, watu wengi wengine wanamafanikio yakipesa lakini wana hali zao mbalimbali zipo kansa kisukari na mengine mengi lakini mtazamo wako ndo utafanya hiyo hali isikuumize kichwa.

Tafuta councellors wazuri watakusaidia sana unaweza ukajishangaa.

Ikiwezekana pia watu wanaokuzunguka /(au unaotaka kudeal nao kama ni biashara au shughuli yoyote) waoneshe hii page watapata namna flani katika fikra.

When things get tough be the toughest....things may then opt to be soft with you.

NOTA BENE: Mtafute Doctor Othman uliyeshauriwa na Cappitano
Ushauri wote humu upangie mkakati.
Asante sana mkuu, hakika nimepata kitu kikubwa hapa. Nahisi kupona na kuanza upya nikiwa na tumaini jipya katika maisha yangu. Mungu awabariki sana wanaJF kama wewe mliojawa maneno yenye kutia nguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unataka kufa na misamiati yako kibao ya kingereza sio?
Relax jikite kwenye kufight bila kuwa selective huku ukijipa moyo hizo kazi ni za mpito utafika unapotarget.
Wewe una potential kubwa mno ya kufanikiwa sema bado hujakutana na right button to press.
KINGINE JUA SITUATION MBOVU ZA MAISHA KWA SASA INA SABABISHWA NA MTU MMOJA NAE ATAONDOKA TU PATARELAX ALAFU MAGUMU HAYAKUUMIZI WEWE TU TUPO WENGI MNO KWA SASA TZ SEMA TUMECHIL TUNAMCHORA ANASEMA ANATUNYOOSHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha dah! sawa mkuu ngoja nivumilie tuisome nmb mpk asepe mzeebaba labda tutapata ahueni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kufanya shughuli ndogo ndogo hapo ulipo kwa maana biashara kama duka, genge, mgahawa nk..

Usiamini kila anayekuja kwako na kujifanya mwema, hapana watanzania tulio wengi hatupo smart kwenye mambo ya watu wengine hata kama yanaweza kukuingizia kipato, Fikilia biashara ambayo 70-90% utasimama mwenyewe na hiyo 30% itakuwa kutuma wengine with no big effect..

Sijui kiuchumi una nguvu gani, kama uko vizuri unaweza kumiliki vifaa vinavyokodishika na ukakodisha kwa watu kwa malipo kabisa kwenye akaunti yako na ukawa na msimamizi tu mmoja mtu wako wa karibu, vitu kama vifaa vya music, vifaa vya ujenzi, magari nk...
Nakupata vyema mkuu asante sana kwa mawazo yako mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana...

Unatumia nguvu na muda mwingi Kuwaza, kufikiri na kutamani kuliko kutenda ndiyo maana unafeli...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom