Bora nikaoe Tanga

Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongee kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo kutoka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule mlimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke akimtwaa fulani.

Wakilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni,
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, hiyo yangu tamaduni.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule Mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate furahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.



MPWA WANGU
Imeshapita miaka,toka liposhika peni
Lile jambo solitaka,naona lipo mezani
mtunzi atiririka,kwa beti ziso kifani
kijana mwana wa kaka,tanga wenda fata nini?

yanishangaza barua,ndefu uliyoandika
akili ukazuzua,kwa misemo kusikika
tanga bahari ya nzoa,kwa huba yasifika
bure utajisumbua,nenda oa lipotoka

limekudatisha pishi,au kanga za mwilini
wajuvi tushirikishi,mpwa wangu watakani
ni viuno tetemeshi,wawapo huko ngomani
au memfata mishi,mwanangwa wa chumbageni

wataka kwenda korogwe,ukatafute mwandani
akili ikavurugwe,umletapo mjini
mchuzi kutiwa ngogwe,si utamu wa chumbani
kwa mganga ukarogwe,hayo ndo mapenzi gani

siku hizi si wa stara,wake wa tanga mjini
wanayabana madera,wakivaa na vimini
midomo wanaifura,ati watoto wa pwani
utajapata hasara,ututie lawamani

naona mesema mengi,na wino menishia
ila jambo la msingi,fata nilokuusia
ata maji yana rangi,ila huwezi ijua
kaka yangu majimengi,salam tampatia
 
MPWA WANGU
Imeshapita miaka,toka liposhika peni
Lile jambo solitaka,naona lipo mezani
mtunzi atiririka,kwa beti ziso kifani
Hahahahahahaha ahsante sana naona shairi limetulia :):):)
 
Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongee kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo kutoka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule mlimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke akimtwaa fulani.

Wakilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni,
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, hiyo yangu tamaduni.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule Mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate furahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
Kaoe tanga ujute, na kilio cha hudhuni
Nyingi Pesa utafute, zinaishia ugangani
limbwata uje upate, akuingie akilini
Familia uifute, usahau kwenu nyumbani
Tanga kuzuli kuoa ila ujipanga mawazoni
 
Tanga mkoa pekee, kwa warembo tashtiti
Kwengine sikosee, moyo taupiga kibiriti
Iwe wachaga wahehe, au wale wamang'ati
Ugomvi kangojee, kikosa pesa ya vyapati
Na ukiwa pedeshee, takunyonga kwa shati
Ila Tanga utastarehe, hata kama riziki hupati
Taitwa bwanshee, mapajani tawekwa kati
Kwa mahaba akulee, kwa huba ya dhati
Na heshima akuletee, hata kwenye umati
Maji akutengee, yanukia mahanjumati
Chooni akupelekee, kuonyesha mahabati
Na ukitoka akupokee, sabuni na mswaki
Kisha dozi akugee, mpaka utetemeke magoti
Kwenu usirejee, na wala hukuoti.
 
Back
Top Bottom