Bora kumkimbiza Rais nchi nzima kuliko Mwenge

Bora kumkimbiza Rais nchi nzima kuliko Mwenge

Ingekuwa ukitoa hoja ya ajabu unakufa watu wengi sana wangekuwa marehemu.
 
Mwenge badala ya kuhamasisha wananchi kuhusu ukimwi mwenge umekua ni sehemu ya kuamasisha ngono na kufungua nyumba za watu binafsi kama guest house nakadhalika. NAUNGA MKONO HOJA.
 
Bado hujapona

Nitaponaje wakati hospitali za jk hazina dawa na sina hela ya kwenda India? Ndio maana napendekeza Fastjet atembezwe mpaka kwenye zahanati zetu ajionee majanga yanayowapata wapigakura wake. Sio kupeleka mwenge usio na macho. Kwani wananchi wakiuona mwenge tu wanapona magonjwa yao?

Badala ya kutoa povu la huba kwa ccm,mshauri jk apeleke madawa kwenye zahanati zetu badala ya mwenge na mabox ya kondom.
 
anazungumzia rais wa kanisa yaani padre muasi na mvunja ndoa za watu
Hapana mkuu anamzungumzia yule jamaa mwenye kifafa, na naona siku hizi dawa zimemkubali, au anaanguka chumbani. Hata hivyo sidhani kama anaweza akamaliza vijiji vya Tanzania, atarudi kweli, ataanguka huko huko.
 
Mwenge ni alama ambayo ndani yake inapaswa kuwa tafsiri ya maisha ya mtanzania na binadamu. ni falsafa ya maisha ya mtz. tatizo ni kwamba umefanywa kama toi. watu hawaoni tena ile asili yake utadhani wanaenda kutambika. Ingefaa shuguli hii isimamishwe kwanza tuanze kufukuzana na wauza unga, wezi, wabakaji, mafisadi n.k. watu wasomeshwe kwanza wapate ufahamu hapo watataka wenyewe kuukimbiza mwenge. hoja yako kuntu. naunga mkono
 
Bora mara elfu kuliko mwenge rais atajua matatizo ya kila wilaya na kuonana na wananchi wake
 
Mwenge unapokimbizwa hata virusi vinaongezeka. ndoa zinasalitiwa, wizi na ulaghai, ufisadi, kazi zinalala amani inapungua kwa sababu kuna watu wanachangishwa kinguvu. SIO ULE MWENGE ALIOUSEMA MWALIMU. tukimbizapo mwenge tuimbe!

sisi tumekuja kuleta mwenge
tumekuja kuletaa mweenge
kuleta mwenge x 2
ili ulete matumaini ....
 
Wakuu naomba anayejua gharama za mwenge toka unafika wilayani na kuondoka kwenye wilaya husika, anisaidie.
 
Samahani Wakuu,

Mimi napendekeza kuwa ni bora kumtembeza Rais wetu kila kijiji ajionee mwenyewe hali ya wananchi wake kuliko kuukimbiza Mwenge ambao hauna macho wala mdomo.

Rais anaweza kupata walau fursa ya kujibu maswali ya wananchi kwa kukumbushwa ahadi alizotoa wakati wa kampeni

Vile vile atapata fursa ya kukiaminisha chama chake kikongwe kwa wenye akili kongwe.

Haaahaa nimeipenda.
Ila Mwenge ooooh mwenge mbio mbio ,
Mwenge tunaukimbikiza Mbio, mbio,
Hadi makao Makuu mbio mbio,
Umulike Mabepari Mbio mbio,
Umulike wanyonyaji mbio mbio,
Umulike Wazururaji mbio mbio. Mwenge tunaukimbikiza Mbio. Nakumbuka Enzi za TANU YOUTH LEAGUE hakika mwenge ulieweka. Ila siku hizi naona Moshi unafuka tuu. Sio tunganganie kila Mila hata kama imepitwa na Wakati. Wakati ni huu wa Kujirekebisha na kukumbatia Mila zenye TIJA.
 
Sikumtambua vizuri ni nani ila alitoa post kwamba kuliko kukimbiza mwenge ni bora kumkimbiza rais kila kijiji ili aone hali mbaya raia wake waliyonayo kiuchumi na kijamii,aone umaskini uliokithiri,vifo vya akina mama na watoto,usafiri ulvyo tabu,madawa hakuna,shule hazina vifaa etc etc,pengine ufisadi unaweza kupungua ili fedha iende kuhudumia wananchi...big up sana mkuu
 
Ni kweli.mii mwenyewe naunga mkono asilimia mia Mnyika njoo chukua maoni haya upeleke,Dodoma.
 
Last edited by a moderator:
mmh jf kuna vichwa hadi basi!hata mie naunga mkono wazo hili.
 
ahsante kijana kwa pongezi zako.
ni mimi ndiye niliyetoa ujumbe huo!
nimeamini,
"kufikiri kisiri-siri ni sawa na safari ya mbwa"
 
Sikumtambua vizuri ni nani ila alitoa post kwamba kuliko kukimbiza mwenge ni bora kumkimbiza rais kila kijiji ili aone hali mbaya raia wake waliyonayo kiuchumi na kijamii,aone umaskini uliokithiri,vifo vya akina mama na watoto,usafiri ulvyo tabu,madawa hakuna,shule hazina vifaa etc etc,pengine ufisadi unaweza kupungua ili fedha iende kuhudumia wananchi...big up sana mkuu
Kumkimbiza? ikiwa mtatumia modaliti ya mbio za mwenge je huyo rais mtambeba kwenye machela au kwenye kiti kama magavana wa kikoloni?
 
Back
Top Bottom