Boni Yai: Mbowe kunyamaza kimya nyakati kama hizi sio sawa

Boni Yai: Mbowe kunyamaza kimya nyakati kama hizi sio sawa

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu kama Boni Yai, amesema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, ana haki ya kuchagua kupumzika kwenye siasa, lakini si sahihi kwake kubaki kimya kuhusu masuala makubwa ya kitaifa yanayoikumba nchi.

Soma pia: Mwenyekiti msaatafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe Yuko wapi?



Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, Jumanne Desemba 23, 2025, Boni Yai amesema mawasiliano yake ya mwisho na Mbowe yalihitimishwa na kauli kwamba anaamua kupumzika na kuelekeza nguvu zake kwenye biashara, hali ambayo amesema ni uamuzi wa binafsi unaopaswa kuheshimiwa.

“Ukiniuliza- uhuru wa yeye kukaa nje ya siasa ni haki yake lakini kukaa labda kimya kwenye mambo ya kitaifa, hiyo hawezi kuwa sahihi, hayuko sahihi", amesema Boni Yai.
 
Ili kufuta ile kesi yake ya ugaidi, lazima kuna maagano yalifanyika kati ya mh. Mbowe na CCM.
 
Akae tu kimya, hata akisema ataytukanwa sana na wanachama wenye msimamo. Kikubwa alitakiwa kustaafu kabla ya uchaguzi wa ndani hakika heshima yake ingekuwa kubwa kuliko mpinzani yoyote kwenye siasa zwgu za vyama vingi.
 
Aongee nini kwani nyie nyumbu hamna midomo?
 
Back
Top Bottom