Bongo movie walikosea hapa

HIVI YALE MAANDAMANO YAO YAMEISHIA WAPI..MBONA HIZO CD ZINAUZWA TU....au walikuwa wanasaka kiki

KWISHA HABARI YAO
 
Mungu atuepushie dhahama.
Yaani unaota kuwa mwalimu!!!!
 
Pilau watapata wateja si unajua tena hali imebana watu wanakula kwa picha a.k.a punyere.
 

Kwa mtazamo mwingine, ni kwamba umeme kwa sehemu kubwa upo mjini na kwenye majiji (2012 census report), sehemu kubwa ya TV ownership ipo mjini na kwenye majiji (2012 census report) halafu upinzani unakubalika kwenye maeneo hayo (NEC election results 2015). Sasa walichoshindwa kuelewa ni hizo takwimu na kufahamu soko lao liko wapi na wateja hasa wapo wapi.

Hata kama ni Internet, bado ni kama TV na kwenye umeme.
 
Acha kubwabwaja hawa jamaa hawana jipya tokea tu walipovaa kijani
 
Kwa hiyo isingekuwa wameingia kwenye siasa ungenunua hizo bongo movie, na sio bidhaa kuwa mbaya, jamani hii ni Tanzania yetu mi naona ishue ni movie kuwa chini ya kiwango, ni kueleweshana,
 
mbona diamond anapiga pesa na alipigia kampeni chama kubwa ccm
bongo movie kazi mbovu ndio zimesababisha kudolola kwa soko lao
eti nisinunue movie kali kisa aliyeigiza alipigia kampeni ccm kila mtanzania ana haki kushabikia chama chochote
hapo hamjishika nchi je mkishika si mtataka TANZANIA yote tuwe CHAGADEMA
 
Nashukuru kuendelea kunisaidia kuelezea mkuu
 
Kwa hiyo isingekuwa wameingia kwenye siasa ungenunua hizo bongo movie, na sio bidhaa kuwa mbaya, jamani hii ni Tanzania yetu mi naona ishue ni movie kuwa chini ya kiwango, ni kueleweshana,
Ningenunua ili kusapoti kwakua najua hicho kidogo kingeweza kuwasaidia kuboresha kazi zao ila walipojiunga na ukijani sio mimi tu hata watu kadhaa nnaowafaham wameacha kabisa kununua na sio kununua tu na kutoangalia kabisa
 
Inatakiwa utofautishe kati ya movie na kaimba
 
Sidhani kama mtu mwenye akili zake timamu anaweza angalia uchafu wa bongo movie..Mipicha haina ubunifu, sound zero bora niangalie cartoon kuliko hayo matakataka ..
 
Nimenunua into the bad land kwa buku tu na ni bonge la movie na inavyoonekana imetumia hela nyingi kutengenezwa sasa leo hii ninunue movie iliyotengenezwa na watu waliokaa kijiweni kwa laki tano eti mtu anaoga na nguo si ujinga huo
Halafu wanarekodi kwa iphone
 
Nyimbo inapewa coverage kubwa sana tofauti na movie nyimbo inaweza kupigwa karibia kila kituo cha redio nchini na TV ila sio movie.
Nyimbo hata usipoipiga wewe ataipiga jirani yako utaiskia na unaweza ukaipenda pia kwakua kuna baadhi ya nyimbo unaweza kuipenda ukiiskiliza mara moja na kuna nyingine hadi uirudie kuisikia mara kadhaa na soko lake lipo karibu kila kona licha ya soko lake mziki pia upo kila kona ila siyo movie ambazo mtu akiamua kuipotezea inapotea jumla.
Sasa kitendo cha bongo movie kutojua soko lake liko wapi na kwenda tofauti na wale waliokuwa wanaisapoti kiasi kikubwa imewafikisha hapa.
 
bongo movie kilichowaua sio kuisapoti ccm kwani wote walisapoti ccm mbona nao kazi zao zinadolola kikubwa ni ubovu wa kazi zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…