Skiza, namba moja kushika sio kwa kasi ya Kobe/
Maji yakimwagika usizoe utazoa tope/
Mwenzako akisali, sali kabla ujaswaliwa/
Pandisha morale, morani aliyetahiriwa/
Mistari si haba vina vinajaza kibaba/
Medani za shaba nnapo simama kama langa/
Mc's wachanga wanajivika usupasta/
Kimbilia suti na nepi bado ujavaa/
Mali imepata daftari, hupotea bila khabari/
Nimechoka kuunguza utambi naunguza hadi kibatari/
Kwa mgongo wa chupa mafuta usinipake/
Mdomo usiwe mtumwa uliyeponzwa na ulimi wake/
Hivi ndivyo nnanyofanya/
Mama unayemlea Mwana kumkemea sio kumkanya/
Raaf, ninayezikosha namba/
Kwenye Giza siwezi kupotosha mwanga./
Hahahaha the best vibe all the time ..l like rap/hiphop aise!!!