Bongo fleva na watoto wetu

Endangered

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
922
228
Habari wadau, jpili imekwendaje?
Anyway jana jmos nilikuwa naskiza Radio One kipindi cha watoto.
Kama kawaida moderator naye ni mtoto. Ikawa kipindi cha methali, katoto kamoja kakapiga.
Methali Methali.
Wote wakamjibu, 'methaliii'.
Then akanimaliza kabisa alipouliza, 'LA KUCHUMPA?'
Na hapo wote wakamjibu bila hata kunyoosha mikono.
Moderator pamoja na kwamba alikuwa mkali kidogo hapo alichoka!
Nikabaki najiuliza, hizi bongo fleva zinapeleka wapi jamii yetu? Labda mwenzangu una jibu aisee.
 
Back
Top Bottom