β¦οΈBiashara sio sio kazi kuanzisha, kazi ni kuisimamia na kukupa faida
β¦οΈBiashara ya chakula ina cha changamoto sana.
β¦οΈWapo watu waliojaribu na kukosea kidogo wameishia kuweka store mavifaa ya garama waliyonunua wakidhani ndio yatakayofanya wateja wajae kwenye migahawa yao
β¦οΈ Kumbuka mtu anayeacha kula kwake au anahama sehemu aliyokuwa anakula kuna vitu vingi vya kumvutia
π Wapo wa wanaokuja kutokana na urembo wa wahudumu , wao hawaangalii ubora wa chakula, garama wala quantity
π Wapo waliofuata chakula bora kilichoandaliwa vizuri
π Asilimia kubwa kwa bongo wanafuata quantity ( chakushiba) hivyo ukimuweka mpakuaji mchoyo anawapiga panga watakukimbia mmoja mmoja utabaki na mavyombo yako
π Wapo wanaofuata bei, kuna wale matawi wanafuata sehemu ya bei ya juu ila ni wachache , asilimia kubwa ukitaka faida balance ili upate idadi ya kutosha ya wateja kila siku