Bondia Mfaume Mfaume na ujasiriamali : Afungua Naccoz Restaurant and Catering

Lady Mwali

Senior Member
Nov 15, 2018
147
332
Katika kujiongezea kipato cha ziada mbali na mapambano ya ngumi nje na ndani ya nchi bondia huyu kutoka Gym ya Naccoz ameamua kujikita pia katika ujasiriamali.

Hivi majuzi ameanza ujasiriamali kwa kufungua mgahawa unaoitwa Naccoz maeneo ya Mabibo Makutano,
Ubungo,Dar es Salaam.

Amewaomba wadau wa ngumi na wapenzi wake waje kwa wingi kupata huduma ya chakula kilichoandaliwa na wapishi wa kimataifa na bei nafuu ili kuenda sambamba na hali ya uchumi ya wananchi.

Ukija mgahawani kwangu utapata huduma ya vyakula vya kila aina, kama pilau,biriani,
ugali,ndizi,supu za kila aina na vitafunwa.

Pia napokea oda mbalimbali kama katika harusi, sherehe na hafla mbalimbali.

Siku ya sherehe ya uzinduzi wa mgahawa wangu natarajia kuwaalika wadau mbalimbali wa ngumi na mashabiki wangu
kutakuwa na mgeni rasmini Waziri wa Michezo au mbunge wa Ubungo'' alisema bondia huyo anayejiandaa na fight dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri ,Julai 10.

Matarajio yangu siku ya mbele nitanue biashara yangu ya mgahawa Tanzania nzima kuwe na matawi ya Naccoz restaurant and Catering.

Changamoto kwa sasa mtaji,
naomba serikali na wadau wa ngumi wanipe support hata ya mkopo au msaada wa kifedha ili nitimize ndoto zangu kwani ngumi zinamwisho wake, kuna kustaafu,alisisitiza bondia huyo.
 
♦️Biashara sio sio kazi kuanzisha, kazi ni kuisimamia na kukupa faida

♦️Biashara ya chakula ina cha changamoto sana.

♦️Wapo watu waliojaribu na kukosea kidogo wameishia kuweka store mavifaa ya garama waliyonunua wakidhani ndio yatakayofanya wateja wajae kwenye migahawa yao

♦️ Kumbuka mtu anayeacha kula kwake au anahama sehemu aliyokuwa anakula kuna vitu vingi vya kumvutia

🕗 Wapo wa wanaokuja kutokana na urembo wa wahudumu , wao hawaangalii ubora wa chakula, garama wala quantity

🕗 Wapo waliofuata chakula bora kilichoandaliwa vizuri

🕗 Asilimia kubwa kwa bongo wanafuata quantity ( chakushiba) hivyo ukimuweka mpakuaji mchoyo anawapiga panga watakukimbia mmoja mmoja utabaki na mavyombo yako

🕗 Wapo wanaofuata bei, kuna wale matawi wanafuata sehemu ya bei ya juu ila ni wachache , asilimia kubwa ukitaka faida balance ili upate idadi ya kutosha ya wateja kila siku
 
Watu kama wewe ni kero kwenye jamii,kila mtu ana namna yake ya biashara na melengo we ushaanza oooh ina changamoto ,ooh mtu anafuata kizuri ,oooh .

Watu kama we mwisho wa siku mnakaa tu bila maendeleo maana kila kitu unaona ina changamoto
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom