Mandonga atambulisha ngumi yake mpya katika maonesho ya Sabasaba

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Bondia Machachari Bw. Karim Said maarufu Mandonga Mtu kazi ametembelea banda la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo ametangaza ngumi mpya iitwayo "Kingugi" anayotarajia kuitumia kwenye mchezo wa marudiano na Bondia Daniel Wanyonyi kutoka Kenya.

Mandonga ametangaza ngumi hiyo Juni 29, 2023 kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa Sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Mandonga ameishukuru Serikali kwa kusimamia vema michezo hatua iliyomfanya ajulikane kimataifa na kuhamasisha vijana kupenda michezo ili kuendesha maisha yao.

Akimkaribisha bondia Mandonga Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo ya 2023, Bi Zahara Guga amesema Wizara ni mlezi wa masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hivyo, Mandonga ni miongoni mwa Wadau wake yupo kwenye ofisi yake ya kazi.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imejikita kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuhamasisha wadau hao kurasimisha kazi zao ambazo ni ajira ya kujipatia kipato kwa kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

IMG-20230629-WA0112.jpg
 
View attachment 2673531
Hiki kijamaa kishirikina balaa
 
Back
Top Bottom